Wanawake Uingereza kununua tembe za kuzuia ujauzito madukani

Wanawake na wasichana wanastahili kupataka dawa za kuzuia ujauzito bila ya ushauri kutoka kwenye maduka maalum ya dawa na kuuzwa duka lolote tu, asema mtaalam wa afya ya uzazi.

Ripoti iliyotolewa na chuo cha madaktari bingwa wa afya ya uzazi cha Royal College nchini Uingereza kimependekeza kidonge kinachomezwa kama hatua ya dharura ya kuzuia mimba baada ya kushiriki tendo la ndoa bila ya kinga kuuzwa madukani kama kondomu.

Kuna masharti mengi sana linapokuja suala la kupata huduma za afya ya uzazi kwa wanawake nchini Uingereza, Ripoti hiyo imesema.

Na mahitaji yao yanastahili kupewa kipaumbele.

Ripoti hiyo kwa jina maslahi bora kwa wanawake, inatoa wito kwa wanawake kuruhusiwa kuchukua dawa ya kwanza ya kuzuia mimba wakiwa majumbani, pamoja na ile ya pili, iwapo watakuwa na uhakika kwamba ujauzito ni wa chini ya wiki 10.

Ripoti hiyo mpya ya chuo cha madaktari bingwa wa masuala ya afya ya uzazi ijuliakanayo kwa kifupi kama RCOG, inasema wanawake wanapaswa kuwa na uwezo wa kupata ushauri wa daktari wanapotaka miamba ama kwa njia ya simu au kupitia Skype.

Ripoti hiyo pia inapendekeza uwepo wa mtandao wa kliniki za afya ya wanawake zinazotoa huduma zote katika eneo moja kama vile uchunguzi wa ugonjwa wa saratani, upangaji wa uzazi na utoaji ushauri.

Kwa sasa, wanawake na wasichana wanahitajika kupata ushauri kutoka kwa mwanafamasia kabla ya kupata dawa za dharura za upangaji uzazi, ambazo zinatakikana kutumiwa ndani ya siku tano baada ya kushiriki ngono bila kinga.

Jambo ambalo linaweza kufanya"wasiwe huru, wahisi aibu ama kuhukumiwa", ripoti hiyo inasema.

Wanapendekeza kwamba dawa za dharurua za uzuiaji wa mimba, vipimo vya uja uzito na kondomu zipatikane katika maduka ya kawaida tu.

Nilihisi kusalitiwa nilipojaribu kupata tembe za kuzuia mimba'

Jane mwenye umri wa miaka 25, kutoka West Midlands, alifukuzwa na mwanafamasia wa kwanza baada ya kutaka apewe dawa za kuzuia mimba kwasababu hakuwa na miadi na siku hiyo.

Baada ya kuzua vurugu, aliruhusiwa kuonana na mwanafamisia huyo na hatimaye akapata dawa alizohitaji lakini hilo lilifanikiwa baada ya maswali mengi.

Jane, anasema alihisi kana kwamba ametenda jambo baya.

"Nilihisi kuhukumiwa kweli. Nina uhakika alisema kitu kama, 'huo ulikuwa ujinga wako," Jane anasema.

"Baada ya hapo nilihisi vibaya kwamba wanawake wanapitia haya yote ili hali kuna njia rahisi ya kupata suluhu."

Dawa za kuzuia ujauzito zinapatikana bure tena bila cheti cha daktari katika maduka yote ya kuuza dawa ya Scotland na Wales.

Nchini Uingereza, huduma za mpango wa uzazi zinapatikana katika vituo vya afya vinavyotoa huduma ya magonjwa yanayoambukizwa kingono, na upasuaji lakini huwa hazitolewe bure.

Chuo cha madaktari bingwa wa afya ya uzazi cha Royal College kinasema kwamba kupunguzwa kwa bajeti ya afya ya umma kumefanya iwe vigumu kwa wanawake kupata huduma wanazohitaji huku utafiti uliofanywa na BBC mwaka jana, ukionyesha kuwa karibu nusu ya la baraza wabunge wa Uingereza walikuwa wamepanga kupunguza fedha zinatumiwa kwa huduma za upangaji uzazi.

Na hili huenda lilisababisha kuongezeka kwa kiwango cha ujauzito na uaviaji wa mimba miongoni mwa wanawake wazee baada ya kupata mimba zisizotarajiwa, ripoti hiyo inasema.

Mwaka 2018 zaidi ya watu 205,000 waliavia mimba katika nchini za Uingereza na Wales.

Ripoti hiyo ya chuo cha madaktari bingwa wa afya ya uzazi cha Royal College, inasema kidonge cha kuzuia mimba kinastahili kumezwa mara moja kwa siku, na pia kipatikane katika maduka ya kawaida badala ya uwepo wa ulazima wa kuwa na karatasi ya daktari.

Ripoti hiyo inasema wasichana na wanawake wanastahili kuweza kuagiza dawa mtandaoni kama bidhaa nyengine yoyote.

Ripoti hiyo inapendekeza yafuatayo:

Njia za upangaji uzazi kwa muda mrefu zinastahili kujadiliwa mara tu baada ya mama kujifungua.

Kuimarishwa kwa huduma za utoaji wa mimba kwa wanawake wote.

Kufunguliwe vituo afya ya uzazi venye uwezo wa kutoa huduma zote na pia vifunguliwe wikendi na nyakati za jioni vilevile.

Huduma zote za kutungisha mimba nje ya tumbo la uzazi zinastahili kutolewa kwa wanawake wote wanaoishi kihalali nchini Uingereza.

Muda wa kukutana na daktari unastahili kuongezwa hadi dakika 15.

Matumizi ya tembe za dharura za kuzuia ujauzito yanapaswa kuwa ya tahadhari:

Ripoti hiyo inasema idadi kubwa ya wanawake wanaishi kwa machungu na karaha kwasababu muda wa kuonana na daktari ni mfupi mno na kuna watu wengi wanaotaka kuzungumza nao.

Profesa Lesley Regan, rais wa chuo cha madaktari bingwa wa afya ya uzazi cha Royal College, amesema: ''Vidonge vya kuzuia mimba ni salama zaidi na maelezo ya daktari kabla ya kuanza kuvitumia ni jambo lisilokuwa na ulazima''

"Tunataka kuhakikisha asilimia 51 ya idadi ya watu imewezeshwa na kuwa na afya njema kadiri inavyowezekana na kwamba hakuna anayeachwa nyuma," Amesema Profesa Regan.

Hata hivyo Simon Kigondu kutoka nchini Kenya, daktari bingwa wa afya ya uzazi anasema dawa zote zinastahili kupendekezwa na daktari ambaye amehitimu anayejua zinavyostahili kutumiwa kwa sababu dawa zote zina madhara.

"Dawa za kuzuia mimba kama Postinor-2 maarufu kama P2 pia zinastahili kupendekezwa na mtu aliyehitimu."

Bwana kigondu anasema hatari iliyopo ya kununua dawa kama hizi bila ushauri wa daktari ni kwamba huenda uko katika hali ambayo inaweza kukusababishia madhara unapokunywa dawa hizi bila kufanyiwa uchunguzi wa kiafya. Lakini kulingana na daktari Simon Kigondu bado hatujafika kiwango cha dawa hizi kuruhusiwa kuuzwa katika maduka ya kawaida tu na kumezwa majumbani.

Ni vizuri kwenda kwa daktari kwasababu, huenda mama amepata mimba inayojitunga nje ya tumbo la uzazi, na hili hawezi kulifahamu hadi wakati atakapoanza kutoka damu ndani ya tumbo, anasema daktari kigondu. Rais wa chuo hicho cha Royal College, Profesa Regan, amesema cha msingi ni kuhakikisha huduma zinapatikana kwa wepesi na ziwe zinazolingana na mahitaji ya wasichana na wanawake.

Unaweza pia kusikiliza:


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?