Tetesi za soka Ulaya Jumatatu tarehe 16.12.2019: Ljungberg, Nuno, Pellegrini, White, Maja, Coutinho

Meneja wa muda Freddie Ljungberg amewataka wakuu wa Arsenal kuamua haraka mtu wanaemtaka kuwa wao meneja ajae. (Sun)

Hatahivyo, Arsenal bado hawajawasiliana na Wolves kupata ruhusa ya kuzunguza na Nuno Espirito Santo juu ya kazi yao ya umeneja. (Express and Star)

Akikabiliwa na shinikizo meneja Manuel Pellegrini anatarajiwa kuendelea kuiongoza
 Ham kwa kemu yao ijayo  ya Crystal Palace itakayochezwa Alhamisi ya baada  Krismasi. (Guardian

Chelsea wanaangalia uwezekano wa kumhamisha mshambuliaji wa Nigeria anayechezea klabu ya Ufaransa Bordeaux Josh Maja, mwenye umri wa miaka 20, zamani akiichezea Sunderland mwezi Januari. (90min.com)

Chelsea pia wamemuweka mlizi wa Brighton Muingereza Ben White, mwenye umri wa miaka 22, ambaye amewafurahisha wengi akicheza kwa deni katika Leeds, katika orodha yao wachezaji watakaonunuliwa kwa pauni milioni 25 wakati dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa Januari. (Sun)

Wachezaji wa Bayern Munich wamewaomba wakuu wa klabu hiyo wasaini mkataba na mchezaji nyota wa zamani wa Liverpool Philippe Coutinho, ambaye anacheza kwa mkataba wa mkopo kutoka Barcelona, wakitaka apewe mkataba wa kudumu baada ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 27 kuonyesha mchezo mzuri katika mechi dhidi Werder Bremen Jumamosi. (Mirror)

Meneja wa mpito wa Everton Duncan Ferguson atafanya mazungumzo na Moise Kean, mwenye umri wa miaka 19, baada ya kumuondoa uwanjani baada ya kucheza dakika 19 - wakidai mshambuliaji huyo wa Kitaliano alihangaishwa na kasi ya Manchester United. (Telegraph)

Liverpool wamejipanga kufaulu kinyang'anyiro cha kusaini mkataba na Sam McCallam -kiungo wa nyuma-kushoto wa Coventry kutoka mwezi Januari kabla ya timu nyingine hasimu za Primia Ligi na kumuajiri kwa mkopo Sky Blues kwa kipindi kilichosalia cha msimu. (90min.com)

Meneja wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps amemtaka mshambuliaji wake wa kimataifa Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 33, kuondoka Chelsea mwezi ujao wa Januari lakini mazungumzo na Inter Milan yamekwama. Giroud atakamilisha mkataba wake msimu ujao.(Mirror)

Real Madrid wanaendela kumfuatilia kwa karibu winga wa Valencia Muhispania Terran Torres, mwenye umri wa miaka 19. (AS)

Makocha wanaopigiwa upatu kumrithi Unai Emery katika uwanja wa Emirates wanazuiwa na hali ya klabu hiyo kutotaka kununua wachezaji wapya katika dirisha la uhamisho.. (Express)


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?