Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 18.12.2019: Pogba, Haaland, Ancelotti, Ronaldo, Kante

Manchester United hawatamruhusu kiungo wao Mfaransa Paul Pogba, 26, kuihama klabu hiyo katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Mail)

United inaamini kuwa itamsajili mshambuliaji nyota wa Red Bull Salzburg na timu ya taifa ya Norway Erling Braut Haaland kwa kitita cha pauni milioni 76 mwezi Januari - na endapo wataruhusu mchezaji huyo asalie kwa mkopo Salzburg mpaka mwisho wa msimu. (Sun)

Hata hivyo klabu ya Red Bull Leipzig pia wamempatia ofa mpya kwa minajili ya kumshawishi mshambuliaji huyo mwenye 19 kusalia klabuni hapo. (Kicker, via Mail)

Carlo Ancelotti atambakiza kocha wa muda wa Everton Duncan Ferguson kama sehemu ya benchi la ufundi kama atateuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo. (Telegraph)

Ajenti wa Cristiano Ronaldo, bwana Jorge Mendes amedokeza kuwa nyota huyo mwenye miaka 34 huenda akamaliza maisha yake ya kandanda katika klabu ya Juventus. (Sky Sports, via Goal)

Manchester City wamewapiku Manchester United katika mbio za kutaka kumsajili beki kinda wa Barcelona Juan Larios, 16, mwezi Januari. (Record)

Barcelona hawana mipango ya kumsajili kiungo mkabaji wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa N'Golo Kante, 28. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Klabu za Ligi ya Primia Liverpool, Manchester United na Chelsea wamepatwa na pigo baada ya winga raia wa Ujerumani Kai Havertz, 20, kubainisha kuwa anataka kubaki katika klabu yake ya Bayer Leverkusen inayoshiriki ligi ya Bundesliga. (Sky Sports)

Crystal Palace wataendelea kumthaminisha mshambuliaji wao raia wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari. (Mail)

Kocha wa zamani wa Newcastle na Liverpool Rafa Benitez, ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Uchina ya Dalian Yifang, amesema ipo siku atarejea Ligi ya Primia. (The Athletic)

Manchester City wamekerwa na mchakato wa Arsenal kumfuatilia kocha wao msaidizi Mikel Arteta na wameionya Arsenal kuwa itawapasa watoe donge nono ili wamnyakue kocha huyo. (Mirror)

Arteta anatarajiwa kukutana na kiongozi mkuu wa Arsenal Josh Kroenke Jumatatu usiku kwa ajili ya kufanya usaili wa tatu na wa mwisho huku akikaribia kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Unai Emery aliyetimuliwa mwezi uliopita. (Mail)

Mlinzi raia wa England Ashley Young, 34, anatarajia kuihama klabu ya Manchester United mwishoni mwa msimu na yupo tayari kuanza mazungumzo na vilabu mbalimbali kuanzia mwezi ujao. (ESPN)

Kocha wa zamani wa Chelsea, AC Milan, Real Madrid na Napoli Carlo Ancelotti amefikia makubaliano ya jumla kuwa kocha wa klabu ya Everton. (Sky Sports)

Kocha Unai Emery amekataa ofa ya kuifundisha Everton akiamini bado ni mapema kufundisha klabu nyengine ya Ligi ya Primia baada ya kufurushwa na Arsenal mwezi uliopita. (Marca)




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?