Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 07.12.2019: Pogba, Van de Beek, Dembele, Cavani, Zaha

Kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba yuko tayari kuondoka katika klabu hiyo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari , huku klabu ya Real Madrid ikiwa na matumaini ya kuanzisha mazungumzo ya kupunguza bei ya Man United ya £126.4m ili kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa huku akiingia miezi 12 ya mwisho katika kandarasi yake. (L'Equipe via AS)

Tottenham imeendeleza hamu yake ya kutaka kumnunua mchezaji wa Ajax Donny van de Beek , lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 na raia wa Uholanzi anataka kuhamia Real Madrid, ambao wanajiandaa kutoa dau la £46.2m (De Telegraaf via FourFourTwo)

Manchester City na Chelsea wamekuwa na mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji wa Barcelona Ousmanne Dembele mwenye umri wa miaka 22 (Eldesmarque via Sun)

Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard anaweza kupata zaidi ya £150m kutumia baada ya marufuku ya uhamisho ya klabu hiyo kupunguzwa huku ikiwalenga winga wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, pamoja na beki wa kushoto wa Leicester City na Uingereza Ben Chilwell, 22.. (Mail)

Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye amesalia na miezi 18 katika kandarasi yake amejiondoa katika mazungumzo ya kumuongezea kandarasi na yuko tayari kuondoka msimu ujao.. (Mirror)

Mkufunzi wa Leicester City Brendan Rodgers anatumai kwamba mkataba mpya aliotia saini utawashinikiza wachezaji nyota kusalia katika klabu. (Times - subscription required)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kwamba klabu hiyo ingekuwa imemuuza kiungo wa kati wa wales Harry Wilson, ambaye yupo katika mkopo katika klabu ya Bournemouth, iwapo haiamini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atasalia katika klabu hiyo. (Guardian)

Kocha wa Leicester Brendan Rodgers

Klopp anasema kwamba Liverpool inaweza kumsaini mshambuliaji mwenye umri wa miaka 19 raia wa England Rhian Brewster ambaye ataondoka kwa mkopo mwezi Januari.. (Liverpool Echo)

Mkufunzi wa wa England Gareth Southgate alisagfiri hadi Itali ili kumtazama beki wa Man United aliyepo kwa mkopo katika klabu ya Roma Chris Smalling, 30, akiichezea klabu yake dhidi ya Inter Milan. (Mail)

Crystal Palace imewasiliana na AC Milan kuhusu uwezekano wa kumsaini mshambuliaji wa zamni wa Liverpool Fabio Borini kwa mkopo. (Evening Standard)

Mkufunzi wa Napoli manager Carlo Ancelotti na mkufunzi wa zamani w a Tottenham Mauricio Pochettino ni miongoni mwa wale wanaotarajiwa Marco Silva Everton.

Mshambuliaji wa Brazil Gabriel Barbosa, 23, ambaye alifunga magoli 43 katika mechi 56 akiwa kwa mkopo katika klabu ya Flamengo kutoka Inter Milan, akisema kwamba angependelea kuichezea (Mail)

Atletico Madrid in mpango kumnunua mshambuliaji wa Paris St-Germain Edinson Cavani baada ya mchezaji huyo wa Uruguay 32 kutochezeshwa mara kwa mara katika klbau hiyo ya Paris. (ESPN)

TETESI ZA SOKA IJUMAA

,Leicester imeanza mazungumzo na kocha Brendan Rodgers kuhusu mkataba mpya ili kuiwekea ukuta nia ya Arsenal kumnasa kocha huyo. (Telegraph)

Kocha wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino hatakuwa kocha wa Bayern Munich.(Bild)

Kocha wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri amesema hatarejea kuwa meneja mpaka kipindi cha majira ya joto lakini anafanya mafunzo ya kiingereza kutokana na kuhusishwa na timu za ligi kuu ya England. (ESPN)

Manchester United bado wana matumaini ya kumsajili kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 27, mwezi Januari baada ya mchezaji huyo kuwakataa.(Mirror)

Mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na timu ya taifa ya Norway Erling Braut Haaland, 19, anaweza kuuzwa kwa kitita cha pauni milioni 17 mwezi Januari kwa mujibu wa mkataba wake.(Manchester Evening News via Bild)

Chelsea wana mpango wa kumsajili mshambualiaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 27, kipindi kijacho cha majira ya joto.(Independent)

,Mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud, 33, hataiacha klabu hiyo mwezi Januari huku vilabu vinavyomtaka vikiamua kusubiri mpaka mchezaji huyo atakapopatikana kwa uhamisho wa bure. (Sun)

Borussia Dortmund wana mpango wa kumbakisha mshambuliaji Jadon Sancho, 19 mpaka mwishoni mwa msimu.(Telegraph)

Kocha wa zamani wa Leicester Nigel Pearson amehojiwa kwa ajili ya nafasi ya ukocha katika klabu ya Watford. (Times)

Kocha wa zamani wa West Ham, Newcastle na West Brom Alan Pardew amesema anapenda kuifundisha Everton lakini amesema kocha wa zamani wa Everton David Moyes 'anafaa kwa nafasi hiyo'.(Mail)

Wakala wa mshambuliaji wa Barcelona KOusamne Dembele,22, amekutana na uongozi wa Chelsea na Manchester City. (El Desmarque - in Spanish)

West Ham watajaribu kumuuza mlinda mlango Roberto mwezi Januari na kutengana na mkurugenzi wa michezo aliyemuingiza kwenye klabu hiyo.(Guardian)

Mshambuliaji wa miaka 17 Ansu Fati ametia saini mkataba mpya wenye kipengele ambacho kitamfanya anunuliwe kwa Pauni milioni 337.5. (FC Barcelona)







Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?