Je, Chama cha upinzani kushinda uchaguzi ni ishara ya demokrasia?

 mwandishi wetu,Mbelechi Msoshi

Historia nyingine iliandikwa kwa taifa la Jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo tarehe 29 Januari 2019.

Kwa mara ya kwanza rais mpya kutoka chama cha upinzani ,Felix Tshisekedi aliapishwa mbele ya maelfu ya raia wa Kongo na rais mstaafu Joseph kabila.

Katika tukio hilo rais mstaafu Joseph Kabila alimkabidhi Felix Tshikedi bendera ya taifa na nakala ya katiba.

Maelfu ya wafuasi wa Tshisekedi, walisherehekea tukio hilo la kihistoria nje ya Ikulu ya Taifa, makaazi ya Rais, mjini Kinshasa.

Baada ya miezi saba, serikali ya muungano ilioundwa, baina ya chama cha kabila na chama cha rais mpya Tshisekedi, vyama viwili ambavyo vilipingana kwa kipindi cha muda mrefu vilikubaliana kufanya kazi kwa pamoja, lakini baada ya siku chache tu mvutano ulianza kati ya vyama hivyo.

Baadhi ya wafuasi wa chama cha Tshisekedi walianza kususia ushirikino huu, huku wakiwashutumu wafuasi wa chama cha kabila kumzuia rais mpya kutekeleza ahadi zake.

"Kitu ninachotaka ni kuona baba anafanya juhudi zake na wezi wasiwe tena karibu yake, huu ni muda wakufurahisha wakongomani, wawe na furaha, wapo wanaoweka mitego ili wakati akishindwa kazi wasema hebu muone ameshindwa kazi, ndo maana sisi tutakuwa makini kufuatialia kwa karibu kwa sababu Kongo ni ya wakongomani na wanapaswa furahi wote," Adophe Amisi kiongozi wa kundi la vijana wa chama cha UDPS.

Utawala wa Muungano wa Rais aliyeondoka madarakani una zaidi ya nusu ya viti vya bunge, na demokrasia inamtaka yule anayekuwa na kura nyigi ndiye anaongoza zaidi, kwa mujibu wa Justin Bitakwira , mmoja wa viongozi wa muungano unaomuunga mkono rais mstafu Joseph Kabila.

Ni vigumu rais mpya kufanya kazi bila mchango wa rais mstaafu kabila.

"Ulishakaona watu ambao wanaongoza kufanya tena maandamano barabarani, hao ndio wanapaswa kusaidia rais mpya, ni sisi pia FCC

tunaungana naye. Lakini yeye ndiye Taasisi na sisi tuko nyuma, kweli chama

cha Kabila kinapata wafuasi wengi, lakini sio rais tena"

Kwa mujibu wa Delphin kapaya , mchambuzi wa masuali ya kisiasa , anasema kuwa sasa wafuasi wa chama cha Kabila hawajaiminia.

Kweli raia walipokea ushindi wa rais mpya na huu muungano kati ya vyama hivyo viwili lakini nia ni kuona mafanikio sasa na kujitenga na vitendo vya uovu, ambavyo wanaotuhumiwa ni wafuasi wa rais mstaafu.

Ni matumaini ya wengi kuona madiliko makubwa, Bienvenu Matumo ni mwanaharakati wa kundi la muungano wa vijana walioshinikiza rais kabila kuondoka madaraka.

"Ziara za rais Felix Tshisekedi zilikuwa pia miongoni mwa taarifa zilizozungumziwa zaidi mwaka elfu mbili kumi na tisa.

Raia wengi walimkosoa kusafiri kila mara, wakati kila ziara yake ina gharama ya maelfu ya dola za Marekani zinazotoka ndani ya mfuko wa serikali" anasema Bienvenu Matumo.

Adolphe Amisi ni miongoni mwa viongozi wa chama cha rais Felix Tshisekedi wa chama cha UDPS, anahisi kwamba ziara za rais zilichangia kufanikisha miradi ya maendeleo ukiwemo wa elimu ya bure katika shule za msingi kutokana na misaada aliyopewa kutoka mataifa ya magharibi na anayepinga ziara hizo, ni adui wa maendeleo.

 kufahamu vipi wanachukulia ziara hizo za rais felix, nimemuuliza Bienvenu Matumo naye anaeleza mtazamo wake juu ya umuhimu wa ziara za nje kwa raia.

"Lusenge Bonne Année, ni mbunge, na mtalam wa masuala ya kidiplomasia. Nadhani anahisi kwamba vyema kusafiri lakini anapaswa kuangalia pia mambo ya ndani jinsi yanavyondelea".

Aliongeza pia..."Wapinzani wake wanahisi, kipaumbele kwa sasa ni kuangalia namna gani wanaweza kumaliza vita katika eneo la mashariki badala ya kusafiri kila mara wakati ana waziri wa mambo ya nje".

Kama anavyonieleza Nyama Ngyokwe ni kiongozi wa chama cha UNLC.

Katika ziara yake nchini Ufaransa hivi karibuni Rais Tshisekedi aliwaambia raia wa Congo wanaoishi Ufaransa kwamba, tangu alipoanza ziara zake, hajawahi kutumia dola milioni hamsini za Marekani, lakini amepata msaada wa dola bilioni moja na nusu, pesa ambazo zitasaidia inchini.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?