Jane Kiarie: ''Mama alijaribu kuniua lakini alitoka akilia''

Jane Kiarie alitelekezwa na mama yake mzazi punde tu baada ya kuzaliwa. Mama yake kijana ambaye kulingana na yeye hakuwa tayari kupata mtoto, akipata ujauzito wa Kiarie alikuwa na umri wa miaka 17 pekee yaani bado kijana na wakati huohuo, alikuwa akifanyakazi kama yaya. Alibeba ujauzito wa Kiarie hadi miezi minane lakini mambo yalimzidi na hapo akaamua kuavya mimba hiyo akiwa peke yakk

e katika nyumba ya dadake alimokuwa anaishi. Baada ya kuona mtoto aliyemuavya ametoka akiwa mzima na analia, akaamua kukimbia na kumuacha mtoto alipoangukia. Dada yake aliporudi jioni baada ya pilk apilka za siku akakutana na mtoto nyumbani kwake akiwa peke yake, na alichoamua kufanya ni kumpeleka kwa bibi yake. Masaibu ya Kiarie hayakuishia hapo kwa sababu mama yake mzazi alirejea tena miaka minne baadaye wakati huo akiwa na miaka 21 na mtoto mwengine wa kike mgongoni. Safari hii mama alionekana kuwa na mpango madhubuti na watoto wake kwasababu mara kwa mara aliwatembelea na kuwaletea viatu, pesa za matumizi na maisha yakaendelea. Penzi hilo, lilidumu kwa miaka miwili tu. 'Namshukuru mama yangu kwa sababu aliamua kubeba ujauzito wangu badala kuitoa nikiwa na miezi kidogo tumboni mwake.' Baada ya kimya cha muda mrefu, bibi yake Kiarie akapata taarifa kuwa mtoto wake amefungwa jela. 'Wakati huo mama yangu alikuwa akifanya biashara yake katika soko la Gikomba viungani mwa Nairobi, na siku moja watu wakaiba viatu katika duka moja la muhindi usiku'' Watu walioiba viatu hivyo wakamuuzia mama yake. Msako ulifanywa na viatu vyenye namba sawia na vilivyoibwa vikapatikana kwake. Mama yake akifungwa, Kiarie alikuwa amekamilisha darasa la nne na bibi yake hakuweza kupata karo ya shule na kulazimika kuachia hapo. 'Mama aliachiliwa huru baada ya kuhudumia kifungo chake lakini akarejea akiwa mtu tofauti.' Mama yake Kiarie alikuwa anaumwa kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu na hakukuwa na dawa za kumnunulia dawa. Baada ya kumuona mama yake akiteseka, Kiarie aliamua kufanya kazi ya yaya akiwa na miaka 10 ili niweze kusaidia familia yangu kifedha. 'Sikuwa naweza kupika lakini jukumu langu lilikuwa kumuangalia mtoto na kumlisha na kuosha nguo'. 'Nilikuwa nikilipwa shilingi elfu moja ya Kenya na wakati huo ilinisaidia pakubwa.' Katika kipindi cha miaka miwili, mshahara wake ulikuwa unakwenda moja kwa moja kwa bibi yake ili mama yake apate matibabu. 'Uwoga wangu ulikuwa ni kwamba mama hataweza kurejea katika hali yake ya kawaida.' Kipindi mama yake alikuwa hoi kitandani, ndoto aliyokuwa akiisimulia bibi yao ni moja tu, kuona watoto wake warudi shuleni. Lakini kwa bahati mbaya mama yake aliaga dunia muda mfupi baadaye. Kukabiliana na kifo cha mama yangu. 'Haikuwa kazi rahisi kwa sababu kwanza sikuwa nimejaaliwa kuishi naye, na miezi mitano tu baada ya yeye kurejea na kuanza kujenga uhusiano wa mama na mtoto, akaaga dunia'. Hawakuwa na baba na hivyo basi waliachwa na bibi yao. Bibi yake anatoka jamii ambayo inaamini ni lazima kutimiza wosio wa mtu aliyekufa hivyo basi alifanya juu chini kuhakikisha kwamba wajukuu wake wanarejea shuleni. Alijiunga na darasa la tano huku dadake akiingia darasa la tatu. Changamoto za maisha ziliendelea kuongezeka kila uchao. Hawakua na uwezo wa kukimu mahitaji yao, pesa za kulipa karo ama kununua sare ya shule. Changamoto nyengine aliyokumbana nayo shuleni ni kukutana na watoto wa familia aliyokuwa akiwafanyia kazi. ''Nikiwa darasa la nane kuna pesa zilizokuwa zinahitajika, shilingi 550 kwaajili ya mtihani wa mwisho wa darasa la nane na sikuwa na mtu wa kunilipia. Nilichofanya ni kwenda kwa mkuu wetu wa shule na kumuomba nilime shamba lake kwa Jumamosi nne kuanzia asubuhi mpaka jioni na yeye anilipie mtihani,'', anasema Jane. Japo alipita mtihani wake, alikosa mtu wa kumsongesha mbele na kuamua kurejea kufanya kazi ya nyumbani. Ni kipindi gani maisha yalianza kubadilika? Kiarie alianza kuishi na shangazi lake aliyeamua kumpeleka shule ya kutengeneza nywele. Alifanikiwa kuanza kufanya kazi kwenye saluni japo mshahara ulikuwa mdogo sana. Lakini kasisi wa kanisa ambalo walikuwa wanaabudu, alifahamu simulizi yao na kuanza kuwahurumia hasa baada ya kufahamu kwamba Kiarie na dadake ni watoto yatima. 'Dadangu hakumaliza darasa la nane kwa sababu ya ukosefu wa karo.', anasema Jane Kiarie. Kasisi wao aliamua kumchukua Kiarie kama mtoto wa familia hiyo na huo ukawa mwanzo wa maisha yake. Familia hiyo ilimtafutia usaidizi kwa wahisani na hatimaye Kiarie akafanikiwa kurejea shuleni. Februari mwaka 2001 wakati alipojiunga kidato cha kwanza katika shule ya upili ya Juja. Safari yake haikuwa rahisi kwasababu ya malimbikizi ya madeni lakini utawala wa shule ukamruhusu kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2004. Kiarie alipona vipi? Mwaka huo baadaye, Kiarie alikutana na wamishonari wawili waliokuja kanisani mwao. Baada ya kufurahishwa na muziki wake, walimpa shilingi 42,000 za kenya kujiunga na shule ya muziki na pesa zilizosalia wakazitumia kumalizia ada ya shule aiokuwa anadaiwa. Kiarie aliolewa mwaka 2008 akiwa mtu wa pili katika familia yake kufanya harusi na kila mtu alitaka kujua kama ni ukweli anaolewa. Akapata mtoto wa kwanza 2011, lakini kwa bahati mbaya miezi kumi baadaye akapata homa kwa siku mbili na kuaga dunia. Akapata tena ujauzito lakini mimba ikatoka akiwa na miezi miwili. Mola akamjalia mtoto wa kike ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 6. Msingi wa Kikirsto umekuwa nguzo yake, hakuwahi kuvunjika moyo. Pia amefungua mradi wake wa kufundisha watoto wasiojiweza na kwa sasa amefanikiwa kusomesha watoto 3 wa kike kama njia moja ya kurejesha shukrani kwa jamii

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?