Boeing yatangaza kuacha kuzalisha kwa muda ndege za 737 Max kuanzia Januari

Kampuni ya Boeing itasimamisha kwa muda uzalishaji wa ndege zake zilizokumbwa na matatizo za 737 Max mwezi Januari.

Utengenezaji wa ndege hizo ulikuwa ukiendelea licha ya ndege za chapa hiyo kuzuiwa kupaa kwa mezi tisa baada ya kuhusika katika ajali mbili zilizosababisha vifo vya mamia ya watu.

Zaidi ya watu 300 walipoteza maisha wakati ndege mbili za 737 Max zilipoanguka katika nchi za Indonesia na Ethiopia baada ya kuripoti matatizo katika mfumo wake mpya.

Boeing imekua ikitumaini kuwa ndege hizo zitarejea tena angani kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo wasimamizi wa safari za anga nchini Marekani wamesema wazi kuwa ndege hizo hazitapewa kibali cha kurejea angani katika siku za hivi karibuni.

Kampuni ya Boeing, yenye makao yake Seattle, Washington ni moja ya wauzaji wakubwa zaidi wa ndege duniani.

Kampuni hiyo imesema katika taarifa yake kwamba haitawafuta kazi wafanyakazi wanaofanya kazi na 737 Max, lakini kusimamishwa kwa utengenezaji zake kunaweza kuwaathiri wasambazaji na uchumi kwa ujumla.

"Kurejea kwa huduma salama za safari za 737 Max ni kipaumbele chetu cha juu," ilisema kampuni hiyo, "Tunafahamu mchakato wa huduma za 737 Max , masharti ya mafunzo yanayohitajika, lazima yatekelezwe kwa usahihi, kuhakikisha wasimamizi wetu, wateja na umma unaosafiri wana imani na 737 Max ."

Wiki iliyopita kikao cha Bunge la Wawakilishi la Marekani kiliambiwa kuwa wasimamizi wa safari za anga nchini Marekani walikua wanafahamu kuwa baada ya ajali ya kwanza kutokea nchini Indonesia Oktoka 2018 kulikua na hatari ya kutokea kwa ajali nyingine zaidi.

Uchunguzi wa shirika la safari za ndege nchini Marekani ulionesha kuwa zinaweza kutokea ajali nyingine zaidi ya kumi na mbili za ndege za 737 Max ikiwa hakuna mabadiliko yatakayofanyika kwenye muundo wake.

Licha ya hayo, 737 Max hazikuzuiwa kufanya safari hadi baada ya ajali ya pili nchini Ethiopia mwezi Machi 2019.

Boeing inabadilisha upya muundo wake wa mfumo wa uuongozaji wa ndege ambao unaodhaniwa kuwa ndio chanzo kikuu cha ajali za ndege zake.

Mchambuzi wa sekta ya usafiri Henry Harteveldt alisema kuwa uamuzi wa kusitisha utengenezaji ulikuwa sio wa kawaida na huenda usiwe na ''athari kubwa kwa Boeing, wasambazaji wake na ndege ".

"Kusema ukweli italeta vurugu kiasi kwa ndege ambazo zinahusikakatika hili na pia kampuni mia sita hivi ambazo nio sehemu ya wasambazaji wa 737-Max na d Boeing yenyewe."

Kuzuiwa kwa safari za 737 Max tayari kumeiga Boeing takriban $9bn (£6.75bn; €8.07bn). Hisa za Boeing zilishika kwa zaidi ya 4% siku ya Jumatatu wakati kukiwa na tetesi kuwa kampuni hiyo ya ndege itatangaza kuahirisha safari zake.

Watengenezaji wanasema ilikua na ndege 400 za 737 Max kwenye akiba yake na walikua wanajiandaa kuzifikisha kwa wateja. Huku kampuni nyingi duniani zilikua zimeagiza, walikatazwa kuziwasilisha ili kuwaruhusu wahandisi wa Boeing kutengeneza mfumo wake wa uongozaji wa ndege.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?