UN - COP 25: Mazungumzo ya hali ya hewa yagonga mwamba

Mataifa ya ulimwengu yamegawanyika katika matabaka ya matajiri na masikini kuhusiana na ufadhili wa mabadiliko ya hali ya hewa na sheria za ushirikiano wa kimataifa.

Marekani, India, China na Brazil zimelaumiwa kwa kukosa muelekeo katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.  Mkutano wa mazingira wa COP 25 wa Umoja wa Mtaifa uliofanyika mjini Madrid, Uhispania na uliotarajiwa kumalizika jana Ijumaa, umeongezewa muda hadi leo Jumamosi ili kujadili zaidi masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Wawakilishi kutoka mataifa 200 wanakutana mjini Madrid kumalizia muongozo wa kuhusu hali ya hewa kwa mujibu wa mkataba wa Paris ea mwaka 2015, ambao unapendekeza upunguzaji wa joto la dunia hadikufikia kiwango cha chini ya digrii 2 Celsius.

Umoja wa Mataifa umesema ili kulipunguza joto kwa nyuzi 1.5 ulimwengu unahitaji kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa zaidi ya asilimia 7% kila mwaka hadi kufikia 2030. Wanasayansi wameonya kwamba dunia inakabiliwa na kasi isiyoweza kuzuilika ya ongezeko la joto duniani.

Kiwango cha joto duniani tayari kimeongezeka kwa nyuzi 1 Celsius, na kinaelekea kuongezeka kwa nyuzi zingine mbili au tatu ifikapo mwaka 2100.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?