Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 27.12.2019: Xhaka, Rabiot, Draxler, Gueye, Volland, Sane, Hazard

Chelsea inamtaka winga a PSG na Julian Draxler, 26, na kiungo wa kati wa Senegal mwenye umri wa miaka 30 Idrissa Gueye. (Star)

Ajenti wa kiungo wa kati wa Arsenal Xhaka nasema kwamba mchezaji huuyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Uswizi amekubali uhamisho wa kuelekea katika klabu ya Ujerumani ya Hertha Berlin. (Blick, via Mirror)

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anataka kumsaini kiungo wa kati wa Adrien Rabiot, 24, kwa mkopo kutoka klabu ya ligi ya Seria A Juventus imwezi Januari. (Times - subscription required)

Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard anasema kwamba winga wa Brazil Willian 31 ameanza mazungumzo na klabu hiyo kuhusu kuongeza kandarasi yake ambayo inakamilika mwisho wa msimu huu.. (Mail)

Bayer Leverkusen itazuia jaribio lolote la Arsenal la kujaribu kumsaini winga wa Ujerumani Kevin Volland, 27, kutoka kwao. (Mail)

Winga wa Manchester City Leroy Sane, 23, atasalia katika klabu hiyo hadi mwisho wa msimu huu lakini raia huyo wa Ujerumani anatarajiwa kuhamia Bayern Munich katika dau la £85m mwisho wa msimu huu . (Star)

Man City inachunguza hali ya beki wa Villareal Pau Torres, 22, pamoja na beki wa Portugal Ruben Dias, 22. (Telegraph)

Kiungo wa kati wa Dinamo Zagreb na Uhispania Dani Olmo, 21,wamehusishwa na uhamisho wa Manchester City na Manchester United na anasema anataka kuchukua hatua nyengine katika kazi yake.. (Manchester Evening News)

Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema kwamba anataka kuwasajili wachezaji wanne au watano katika dirisha dogo la uhamisho la mwezi Januari. (Mail)

Babake kiungo wa kati wa Arsenal Mohamed Elneny anasema kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Misri ambaye yuko katika klabu ya besikitasa kwa mkopo ameanza mazungumzo kuhusu uhamisho wa kuelekea AC Milan. (Express)

Mshambuliaji wa Real Madrid Eden Hazard, 28, huenda akaendelea kuuguza jeraha hadi mwezi januari ama mwanzo wa Februari baada ya raia huyo wa Ubelgiji kupata jeraha hilo mwisho wa mwezi Novemba. (Marca)

Kiungo wa kati wa Real Madrid Martin Odegaard, abaye alijiunga na Real Sociedad kwa mkopo kwa miaka miwili anatarajiwa kuitwa na klabu hiyo ya Bernabeu mwezi 2020. (AS)

Barcelona itajaribu kumsaini mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 27, katika dirisha dogo la mwezi Januari. (Goal)

Chelsea inafikiria uhamisho wa mwezi Januari wa mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 23. (Express)

Kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba, 26, anataka kuondoka katika klabu hiyo na kurudi katika klabu yake ya zamani J

Mario Mandzukic amemaliza uvumi uliokuwa ukienea baada ya kukamilisha uhamisho wake katika klabu ya Qatari ya Al-Duhail licha ya Man United kuonyesha hamu ya kumsajili kutoka Manchester United. (Mail)

Manchester United inajiandaa kumpatia mshambuliaji wa Norway Erling Haaland mshahara wa £200,000 kwa wiki ili kujiunga nao kutoka Red Bull Salzburg. (Sun)

Beki wa Chelsea na Uhispania Marcos Alonso, 28, analengwa na klabu ya Inter Milan. (Calciomercato)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32, anakaribia kukamilisha uhamisho wa mwezi Januari kuelekea Atletico Madrid. (Marca)

Arsenal inatarajiwa kumuuza mmoja ya washambuliaji wake na kumnunua mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele. (Le10Sport - in French)

Everton na Atletico Madrid wanapigania kumsaini mshambuliaji wa River Plate na Colombia Rafael Santos Borre, 24. (AS)

Beki wa Manchester United Chris Smalling, 30, anataka kusalia Roma wakati makubaliano yake ya mkopo yatakapokamilika mwisho wa msimu huu. (Roma Press)

AC Milan ina matumaini ya kuafikia makubaliano ya kumsaini mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, katika klabu hiyo mwezi Januari. (Mail)

West Ham inafikiria kumsaini beki wakati wa Uhispania Unai Nunez, 22, kutoka Athletic Bilbao. (AS in Spanish)

Uhispania Unai Nunez, 22, kutoka Athletic Bilbao. (AS in Spanish)
Real Madrid wamemwambia ajenti wa Paul Pogba Mino Raiola kwamba hawatomsaini kiungo huyo wa kati mwezi Januari.. (Mail)

Chelsea wamepewa fursa ya kumsaini Isco mwenye umri wa miaka 27 kwa dau la £44m na Real Madrid, hatua itakayotoa fursa kwa mabingwa hao wa Uhispania kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham Christian. (Mirror)

Beki wa Arsenal na Bosnia-Herzegovina Sead Kolasinac, 26, analengwa na Napoli pamoja na Roma. (Sky Sports)

Mkufunzi mkuu wa RB Leipzig Oliver Mintzlaff amefichua kwamba wanapata shida kushindana na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumsaini mshambuliaji wa Norway Erling Haaland kutoka Salzburg. (Mail)

Tottenham watahitaji kulipa dau la £50m kumsaini beki wa Ufaransa Issa Diop mwenye umi wa miaka ,22, kutoka West Ham. (Express)

Spurs inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Lille Boubakary Soumare . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 pia analengwa na Manchester United. (L'Equipe - via Football 365)

Borussia Dortmund haitazuia uuzaji wa winga wa England Jadon Sancho, 19, mwezi Januari. (Bild)

AC Milan wameweka dau la £26m kwa kiungo wake wa kati Franck Kessie, huku Wolves ikifikiria kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 mwezi Januari.. (Calciomercato - in Italian)

Lyon inamnyatia kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Ufaransa Thomas Lemar, 24,. (L'Equipe - in French)

Atletico wameafikia makubaliano ya kumsaini mshambuliaji wa PSG na Uruguay Edinson Cavani, 32. (Star)

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameungwa mkono kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Croatia Mario Mandzukic, 33, kwa makubaliano ya muda mfupi. (Express)

Everton wameshauriwa kumsaini mshambuliaji wa Wolves na Mexico Raul Jimenez, 28, pamoja na mshambuliaji wa Southampton Danny Ings, 27. (Talksport - via Star)

Mkufunzi wa Leicester City Brendan Rodgers anasema beki wa Croatia Filip Benkovic, 23, huenda akaondoka kwa mkopo mwezi Januari huku klabu ya Derby County. (Leicester Mercury)











Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?