Tetesi za soka Ulaya Jumanne 10.12.2019: McTominay, Solskjaer, Eriksen, Emery

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameambiwa kwamba kazi yake ipo salama na mmiliki wa klabu hiyo na kwamba hawatamuajiri aliyekuwa mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino.. (Mail) Manchester United wana mpango wa kumpatia kiungo wa kati wa Uskochi mwenye umri wa miaka 23 Scott McTominay mkataba mpya wa £60,000 kwa wiki . (Sun) Everton iliwasiliiana na mkufunzi wa zamani wa Arsenal Unai Emery kuhusu pengo la mkufunzi katika klabu hiyo ya Goodison Park. (Sky Sports) Rasi wa Barcelona Josep Maria Bartomeu anasema kwamba mlango upo wazi kila mara iwapo mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola atahitaji kurudi katika klabu hiyo.. (La Repubblica, via Goal) Arsenal inakabiliwa na upinzani kutoka kwa Inter Milan na Juventus kwa saini ya beki wa Manchester United Chris Smalling, 30, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Roma. (Mirror) Newcastle na Bournemouth zinamchunguza mshambuliaji wa Hull City mwenye umri wa miaka 22 Jarrod Bowen. (90min) Bologna wamewasiliana na klabu mbili za ligi ya Premia kuhusu mshambulaiji wa Wolves raia wa Itali Patrick Cutrone, 21, na mshambuliaji wa Everton mwenye umri wa miaka 19 Moise Kean. (Le Repubblica - in Italian) Mkurugenzi wa Bologna Walter Sabatini amesema hakuna uwezekano wowote wa kumsaini Zlatan Ibrahimovic baada ya kufichua kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 raia wa Sweden ameamua kule atakakohamia . (Mail) Mkufunzi wa klabu ya Dalian Yifang Rafael Benitez amesema haoni sababu ya kurudi katika kuifunza klabu ya Ligi ya Premia kwa sasa .{Sky Sports) Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard ana wasiwasi kuhusu kuanzisha matumizi mwezi Januari baada ya marufuku ya timu hiyo kuondolewa. (Evening Standard) Rais wa Besiktas Ahmet Nur Cebi amesema kwamba hakuna uwezekano kwa mshambuliaji wa Evertonna Uturuki Cenk Tosun, 28 kuhamia klabu hiyo. (Hayatta Besiktas Radio station, via Liverpool Echo)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?