Mzee aiba pesa na kuzitoa kama zawadi akisema 'Merry Christmas'

Bwana mmoja mwenye ndevu nyeupe alifanya u
vamizi wa benki siku mbili kabla ya Krismasi na kuzirusha juu kwa furaha na kuwatakia kheri ya siku kuu wapita njia, mashuhuda wameeleza.
Polisi wamethibitisha "mwanaume mzee wa kizungu" alivamia benki ya Academy mjini Colorado Springs, Marekani siku ya Jumatatu.
"Aliiba pesa benki, akatoka nje na kuzitawanya kwa watu," shuhuda Dion Pascale alikiambia kituo cha Colorado's 11 News.
"Alianza kurusha fedha kutoka kwenye begi na kisha akaanza kusema, 'Merry Christmas!'"
Kwa mujibu wa mashuhuda, mtuhumiwa huyo akapiga hatua chache kutoka benki na kuketi mbele ya mkahawa wa Starbucks akisubiri kukamatwa.
Katika hali ambayo inaweza kuwa ya kustaajabisha kwa wakazi wa Afrika Mashariki, wapita njia wanaripotiwa kuwa walichota fedha zote zilizozagaa na kuzirudisha benki.
Polisi hawadhani kuwa alikuwa na usaidizi wowote.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?