Ugumu wanoupata wanaume wafupi kupata wapenzi.

Allan Mott anasimulia ugumu wa kuwa kwenye mahusiano kwa sababu ya ufupi wake.

"Ukiwa mwanaume mfupi utegemee katika wanawake 10 ,basi nane kati yao watakukataa kuwa nawe kimapenzi mara tu wanapokuona", Allan ameeleza.

Baadhi ya wasomaji akiwemo mwanamke mmoja mrefu - baadhi walijibu kulingana na mambo ambayo wamepitia katika maisha yao kuwa mazuri au mabaya.

'Wanaume wengi wafupi mara nyingi wanalalamikia kupata wakati mgumu kupata wanawake-Sijawahi kuhisi hivyo'

Robert ambaye ana urefu wa futi 5(anaonekana kwenye picha hapo juu na mpenzi wake wa zamani)

Sweden ni nchi ambayo inajulikana kuwa taifa lenye wanaume warefu.

Licha ya kwamba sikuona kama wananizidi sana. Nimekuwa na marafiki wengi ambao ni warefu- marafiki zangu wanaume wana urefu wa kati ya sentimita 180 na sentimita 190 (kati ya futi 5na futi 6) - na imenifanya kujisikia vizuri nikiwa karibu na watu warefu.

Ni kweli watu huwa wanaongelea ufupi wangu mara kwa mara , lakini sikujiona kama nnanyanyaswa kutokana na kimo changu. Mimi nilikuwa mvulana mfupi darasani.

Kuna mambo ambayo yalikuwa yanatokea miaka ya nyuma- kama vile watu kutaka kunibeba kwa sababu ni rahisi kunyanyuliwa.

Labda mambo ambayo yalikuwa yananikwaza sana ni pale mtu anapoanza kuniuliza kuhusu kimo changu wakati ananiona ni mfupi na wanaanza kusema kuwa Mungu wangu!, wewe mfupi sana?

Wanahoji kama vile kuwa ghafla tu niliamua kuwa mfupi mwenyewe?

Mara nyingine nilihisi kuwa labda maisha yangeweza kuwa magumu sana kama ningekuwa mwanaume mrefu, lakini wakati huohuo nilikuwa najiuliza kama ningekuwa mrefu ningekuwa mtu wa aina hii?

Wakati nilipokuwa mdogo, kuna watu walishauri nichomwe sindano ya homoni itakayoweza kunifanya niwe mrefu.

Nilifanyiwa vipimo vya X-ray katika mkono wangu kuona kama mifupa yangu kama inaweza kukua.

Ninafahamu kuwa wanaume wafupi huwa wanalalamika kuwa wanapata wakati mgumu kupata wanawake, lakini mimi sijawahi kuhisi hivyo.

Mara zote imekuwa rahisi kwangu kuwa rafiki wa wanawake.Yani ni kitu ambacho kitatokea tu kwa asili kupendwa na wanawake lakina sina mbinu yoyote ngumu ambayo natumia kupatana nao.

Nikiwa katika mahusiano huwa sifikirii kuwa ufupi wangu ndio kikwazo. Wanawake niliowahi kuwa nao huwa wana urefu wa kuanzia sentimita 155 ambao ni sawa na kimo changu mpaka sentimita 175.

'Wanawake wengi hawapendi kuwa na wanaume wenye chini ya futi 6'

Chris, ana urefu wa sentimita 170

Nilijaribu kutumia programu ya mtandao kutafuta wapenzi, niliandika urefu wangu wa kweli na sikupata wanawake wengi walionipenda kwa kipindi cha wiki moja.

Nilituma ujumbe kwa wote ambao walikubali urafiki lakini kati yao ni asilimia 20 tu ndio walionijibu. Hivyo nikaamua kubadilisha maelezo yangu ya urefu kuwa nina futi 6 na nikapata idadi kubwa ya watu waliovutiwa na mimi ,yani mara tatu zaidi na asilimia 50 ya watu hao walijibu ujumbe niliowaandikia.

Hii ni kutokana wanawake wengi mjini London hawataki kuwa na wanaume ambao wana urefu wa chini ya futi 6.

'Mpenzi wangu wa zamani alikuwa anapenda wanaume wafupi'

Adrian, ana futi 5 (163sm)

Nilianza chuo kikuu niliambiwa kuwa kuwa kimo changu ni kizuri kushiriki katika michezo wa boti majini.

Nilipoingia kwenye klabu ya mchezo huo, nilikuwa na bahati sana ya ushindi.

Sijawahi kunyanyaswa kutokana na ufupi wangu na hata kwenye mahusiano sijawahi kunyanyaswa yani taofauti kabisa na jinsi ya watu wanavyodai kuhusu watu wafupi.

Mpenzi wangu wa zamani alikuwa ana futi 6, yeye alikuwa anapenda wanaume wafupi, sijui alikuwa anajiona yuko salama akiwa na wanaume wafupi na kuwa na mahusiano na wanaume warefu ilikuwa inampa wakati mgumu na alikuwa anachukia watu wanaposhangaa maamuzi yake.

Ilinichukua muda kuzoea kuwa na mwanamke mrefu mrefu kiasi hicho ingawa ilikuwa sifa kwangu na inawezekana kulikuwa na kitu cha kipekee kwangu.

Mke wangu wa kwanza alikuwa na urefu sawa na mimi. Mke wa pili ambaye nilikaa naye muda mrefu alikuwa na futi 6 na mke wa tatu alikuwa na futi 5,8

Nilikataliwa na wengi kutokana na urefu wangu haswa kwenye utandawazi wa kutafuta wapenzi mtandaoni.

Lakini kwa maoni yangu naona ufupi wangu sio tatizo bali ni tatizo lao.

Nina furaha sasa na kimo changu, nimeweza kuvuka changamoto nyingi pia miaka yote 40 lakini hayo yote yamepita.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?