Je Afrika inaweza kufanya nini kuwaepusha vijana na uhamiaji?

Mwanamuziki wa Kinyarwanda Mani Martin anawaasa vijana wa Afrika kuacha kufikiria kwamba matumaini yao yako ulaya au Marekani.

Katika albumu yake mpya aliyoipa jina la ''Africa ndota'' yaani -Africa ninayoiota katika lugha ya Kiswahili, msanii huyo maarufu sana nchini Rwanda ameelezea namna anavyosikitishwa anasikitishwa na jinsi maelfu ya vijana wa Afrika wanavyofuja pesa wakitaka kwenda kutafuta rizki Ulaya na kupoteza maisha yao katika bahari ya Mediterranean badala ya kuwekeza pesa hizo katika mataifa yao ya Afrika.

Mani Martin katika kibao chake ''Afrika Ndota''anaimba ndoto zake kwa bara la Afrika,namna anavyopendelea bara la Afrika kuwa, huku akipinga Waafrika wanaokimbilia barani Ulaya na Marekani wanakodhani watapata maisha bora.

Kuhusu wanaokimbia vita na usalama mdogo katika nchi zao Bwana Marte alisema:

"Viongozi wa Afrika lazima wafanye juhudi kubwa ili vijana waweze kupata maisha ya ndoto zao pasipo kufikiria kutoroka mataifa yao.

Wanapaswa kubuni mikakati ya kuimarisha usalama na amani kwa sababu wanaokwenda wana sababu mbali mbali. Lakini hayo yote yanaweza kupatiwa suluhu na sisi Waafrika wenyewe.Nchi zetu zitaendelezwa na nani?wazungu wanapokuja hapa wanaitwa wataalamu, lakini sisi tunapofika kwao tunaitwa wahamiaji haramu!"

Msanii huyu ambaye ni miongoni mwa wasanii wanaokonga nyoyo za walio wengi nchini Rwanda na Afrika Mashariki katika nyimbo zake zenye ujumbe wa Amani, hivi karibuni alikuwa na tamasha nchini Japan.

Bwana Marte ambaye alianza muziki wake kwa kuimba nyimbo za injili, anafahamika zaidi kwa mtindo wake wa muziki wa Afrobit kwa lugha nne jambo ambalo limempatia umaaru ndani na nje ya mipaka ya taifa lake taifa lake.

''Mimi kama mwanamuziki kutoka Rwanda natumia lugha ya Kinyarwanda,kiingereza,kifaransa na Kiswahili na hizo lugha hazisikiki hata kidogo huko mfano nchini Japan ambako nilifanya tamasha hivi karibuni. Nimejifunza kwamba muziki ni lugha ya kukutanisha watu bila kujali wako nchi gani na hata pasipo kujali utamaduni wala kabila...yaani muziki hauna mipaka.'' anasema Msanii huyo.

Nchi yake Rwanda ilitangaza kutoa hifadhi kwa wahamiaji mwezi Novemba mwaka 2017 baada ya chombo cha habari cha CNN kuonesha video ikiwaonesha wanaume wakipigwa mnada kuuzwa kama wafanyakazi wa mashamba nchini Libya.

Mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu Kundi la wahamiaji 66 linalojumuisha watu watu walio hatarini zaidi pamoja na watoto walio peke yao lilipokelewa chini Rwanda kutoka Libya, baada ya Rwanda kukubali kuwapokea wahamiaji hao

Miongoni mwa watu hao ambao baadhi yao wanatoka mataifa ya upembe wa Afrika, walikuwa ni mtoto wa miezi miwili mwenye asili ya kisomali aliyezaliwa katika kituo cha kuwazuilia wahamiaji nchini Libya.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?