Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 30.11.2019: Rodgers, Arteta, Vieira, Sancho, Willian, Richarlison

Arsenal wako tayari kuona kama wataweza kumshawishi Brendan Rodgers wa Leicester miongoni mwa watu waliowaorodhesha kuchukua nafasi ya Unai Emery.(Mirror)

Leicester itahitaji fidia ya pauni milioni 14 kama klabu yoyote ya ligi kuu itajaribu kumchukua Rodgers. (Telegraph)

Washika bunduki hao waliwasiliana na kocha wa zamani wa Valencia Marecelino ili awe meneja wao mpya ( Sun)

Mauricio Pochettino, Nuno Espirito Santo, Massimiliano Allegri na Carlo Ancelotti wote ni miongoni wa wanaotamaniwa kujaza nafasi hiyo katika uwanja wa Emirate. (Telegraph)

Wamiliki wa Wolves wanajiandaa kupambana kumbakisha Nuno, ambaye mkataba wake utakwisha mwishoni mwa msimu ujao. (Mail)

Arsenal tena itapendekeza mchezaji wa zamani Mikel Arteta kujaza nafasi iliyoachwa na Emery. (Independent)

Uamuzi wa kumtimua Emary ulifikiwa katika mkutano uluifanyika nchini Marekani siku ya Jumatatu.(Mirror)

Aliyekuwa kipenzi cha Arsenal Patrick Vieira amefuilia mbali mpango wa kuondoka Nice- ingawa amekuwa akihusishwa na taarifa za kuchukua nafasi ya Emery. (Mirror)

Masuala ya winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho yameshapatiwa ufumbuzi na mchezaji huyo hatarajiwi kuondoka mwezi Januari, asisitiza Mkurugenzi wa michezo Michael Zorc. (Goal.com)

Juventus wanapenda kumsajili beki wa kushoto wa Chelsea Emerson Palmieri, 25. (Calciomercato - in Italian)

Real Madrid inafikiria kutoa ya ofa ya kiungo James Rodriguez, 28, kwa Arsenal kubadilishana na mshambuliaji raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30. (El Desmarque via Calciomercato)

Inter Milan ina mpango wa kumsajili mshambuliaji Olivier Giroud,33, mwezi Januari. (Tuttosport, via Calciomercato - in Italian)

Manchester City wako kwenye mazungumzo na wakala wa kiungo wa River Plate Nicolas De La Cruz, 22. (Ole, via Sport Witness)

Mshambuliaji wa kibrazili Richarlison, 22, yu karibuni kusaini mkataba mpya na Everton ili aendelee na klabu hiyo mpaka 2024. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, 32, amemsifu mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, akisema kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 22 anaweza kuwa mwafaka kuwa mbadala wake Nou Camp. (One Football - in Spanish)

Kocha wa Tottenham, Jose Mourinho amesema Ryan Sessegnon anaweza kuwa kama beki wa kushoto wa zamani Ashley Cole, lakini anasema mchezaji huyo mwenye miaka 19, hawezi kucheza kama beki. (London Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Tottenham Jamie Bowden ,18, yuko mbioni kukubali mkataba mpya na klabu hiyo. (Football Insider)

Kocha wa Newcastle Steve Bruce amemuambia mshambuliaji wa Uingereza Dwight Gayle kuwa atapata nafasi msimu huu- lakini mchezaji huyo,29 ameambiwa kusubiri zamu yake. (Newcastle Chronicle)

Brighton haina ''shauku ya kupitiliza'' ya kuimarisha kikosi mwezi Januaru, amesema kocha wa timu hiyo, Graham Potter. (Argus)

Makamu mwenyekiti wa West Ham Karren Brady anamuunga mkono kucha wa Hammers, Manuel Pellegrini. (Sun)

Kiugo wa Aston Villa Callum O'Hare, 21, anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Coventry amesema anayaka kuwa na Sky Blues kwa msimu wote uliobaki. (Birmingham Mail)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?