Inaelezwa kuwa matumizi ya risasi za mpira ni hatari kwa waandamanaji.

Dunia imeshuhudia maandamano makubwa mitaani kwenye kipindi cha miezi michache iliyopita, kwa kiasi kikubwa na kusababisha, majeraha na hata vifo.

Majeraha kama ya macho yaliyosababishwa na silaha za kudhibiti makundi kama vile risasi za mpira.

Kwa mfano nchini Chile, wataalamu wa masuala ya afya na makundi ya haki za binaadamu wanakadiria kuwa takribani watu 220 wamepata majeraha ya macho kwa kipindi cha mwezi mmoja wa maandamano.

Na ripoti mpya ya Shirika la Amnesty International, shirika ambalo lilifanya uchunguzi katika nchi hiyo ya kusini mwa Amerika, imeshutumu serikali ya Chile kuwadhuru waandamanaji makusudi.

Madhara ya makusudi

''Nia ya vikosi vya usalama vya Chile iko wazi: kuwajeruhi wale wanaoandamana ili kuyapiga marufuku maandamano,'' Erika Guevara Rosas, Mkurugenzi wa shirika la Amnesty International Amerika, amesema kwenye taarifa yake aliyoitoa tarehe 21 mwezi Novemba.

''Mamlaka chini ya Rais Sebastian Pinera zimeendelea na sera ya adhabu kwa zaidi ya mwezi mmoja, na kusababisha idadi ya waathiriwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa.''

Enrique Morales Castillo, rais wa idara inayoshughulikia masuala ya haki za binaadamu katika chuo cha kitabibu, ameiambia BBC kuwa ''hakuna taifa jingine ambalo limeripoti kuhusu idadi hii ya matukio ya (majeraha ya macho)''

''Takwimu hizi zimezidi marejeo yoyote ambayo tunayo,'' Castillo aliongeza.

Kufahamu ni namna gani kiwango cha majeraha kinavyoogopesha , katika utafiti wa mwaka 2011 kuhusu madhara ya mzozo wa Israel na palestina ilibainika kuwepo kwa majeraha ya macho 154 wakati wa mapambano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama kwa zaidi ya kipindi cha miaka sita(1987-93).

Mzozo uliosababisha idadi ya majeraha ya jicho, hata hivyo, yalitosha kwa mamlaka za Chile kurudi nyuma: mnamo Novemba 20, mkuu wa jeshi la polisi wa kitaifa, Mario Rozas, alitangaza kusimama kazi kutokana na matumizi ya risasi za mpira.

Rozas, hata hivyo, alisema kuwa maafisa bado wataruhusiwa kutumia silaha zisizo na madhara kama '' kama njia ya kujilinda ikiwa kuna tishio linaloweza kugharimu maisha yao''.

Kiwango cha majeraha nchini Chile kinaweza kufananishwa na hali ilivyokuwa katika mji wa Kashmir, mji uliokuwa ukizozaniwa na India na Pakistan.

BBC iliripoti mwaka 2018 kuwa takribani watu 3,000 walipata majeraha ya macho katika miaka ya hivi karibuni kwa sababu ya matumizi makubwa ya risasi za baridi dhidi ya waandamanaji katika eneo la mji linalodhibitiwa na India.

Hong Kong, madhara ambayo muandamanaji mwanamke baada ya kujeruhiwa jichoni mwezi uliopita wakati wa maandamano ya kuunga mkono demokrasia yalikuwa alama ya kupinga vitendo vya vikosi vya usalama kushambulia waandamanaji.

Waandamanaji ambao walivaa vitambaa kufunika jicho moja walionekana wakitembea mitaani, mtindo ulioigwa na Chile pia.

Maandamano ya kuunga mkono kujitenga kwa mji wa Catalonia nchini Uhispania pia yalisababisha kuwepo kwa matukio mengi ya majeraha ya macho yaliyosababishwa na silaha.

Siku ya Jumatatu , picha iliyomuonesha mpigapicha wa kipalestina Muath Amarneh akivuja damu kwenye jicho lake la kushoto baada ya kufyatuliwa na risasi ya mpira na vikosi vya usalama vya Israeli kwenye ukingo wa magharibi ilisambaa mitandaoni.

Takwimu za dunia kuhusu majeraha yaliyotokana na silaha za kudhibiti makundi ya watu si rahisi kuzipata.

Katika mapitio yake mwaka 2017, timu ya watafiti wa Marekani, ambao walichambua tafiti zaidi ya 26 zilizofanywa duniani kote tangu mwaka 1990 ilibaini kuwa katika nchi nyingi ''hakuna matakwa ya kisheria ya kukusanya data kuhusu majeraha'' yaliyosababishwa na madhara ya matumizi ya risasi za mpira.

Timu hiyo ilibaini jumla ya watu 1,984 katika miji mbalimbali duniani walipata majeraha.

Upofu wa kudumu

Lakini kujeruhiwa jichoni kulikuwa na madhara ya muda mrefu: Upofu wa kudumu ni madhara kwa matukio 261 ya kujeruhiwa macho , ambayo ni zaidi ya 84%.

Watafiti wamesema kuwa silaha hizo haziaminiki vya kutosha kutumika.

''Silaha baridi nyingi zimeundwa kwa kupunguza kasi yake zinapofyatuliwa na hupunguza uwezekano wa kupenya kwenye ngozi, ''wameandika.

''Kutokana na kutoaminika kwake, matumizi mabaya ya silaha hizi husababisha madhara kama vile majeraha mabaya, ulemavu na vifo. Silaha hizi KIP kwa kitaalamu zimebainika kutokuwa silaha mwafaka kutumika kwenye kudhibiti mwakundi ya watu.

Umoja wa Mataifa una miongozo kwa hatua za vikosi vya usalama ambavyo vinakuwa na kazi ya kudhibiti waandamanaji- Miongozo hiyo inaitwa Miongozo kuhusu matumuzi ya nguvu na silaha kwa maafisa wa ulinzi.

Miongozo hiyo inasema polisi wana haki ya kuchukua hatua kwa ajili ya kujitetea au kuwatetea wengine.

Lakini machapisho mengine ya Umoja wa Mataifa, ikiwemo maazimio ya baraza la haki za binaadamu, yameeleza kuwa silaha za KIP zinaweza kusababisha madhara makubwa kuwa zinaweza kurushwa kwa kasi mpaka ya umbali wa mita 100 kwa sekunde.

Mwezi Februari, Baraza la Ulaya, kundi la kutetea haki za binaadamu barani ulaya, liliitaka Ufaransa kuacha matumizi ya risasi za mpira baada ya ripoti ya Taasisi iitwayo Disarm Collective iliyosema kuwa watu 100 walipata majeraha mabaya kutokana na matumizi ya silaha hizo mwezi Novemba mwaka 2018 na Januari mwaka 2019.

Kwa mujibu wa taasisi hiyo, kulikuwa na visa 17 vya kupoteza uoni kutokana na matumizi ya silaha hizo.

Wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa ilikana takwimu hizo ikisema kuwa kulikuwa na visa vinne pekee vya watu ambao walipata madhara makubwa ya macho, ingawa takwimu za wizara zinaonesha kuwa vikozi vya usalama vilivyatua zaidi ya risasi 13,000 kati ya mwezi Novemba mwaka 2018 na mwezi Machi mwaka 2019.

Katika ripoti ya hivi karibuni kuhusu masuala hayo hayo, nchini Afrika Kusini, kati ya mwaka 2002 na mwaka 2011, taasisi hiyo ilinukuu malalamiko 204 dhidi ya polisi kuhusu namna walivyodhibiti watu.

Visa 85 vimekuwa vikichunguzwa na askari mmoja ameshtakiwa.









Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?