Kukatikakatika kwa umeme Zimbabwe kumefanya raia nchini humo kutumia nishati ya jua

Zimbabwe imepiga marufuku kuweka mashine za kupasha moto (heater) ikiwa ni jitihada ya kutunza umeme, Shirika la habari la uingereza Reuters limenukuu shirika la udhibiti wa nishati ya umeme nchini humo.

Wasambazaji wa umeme hawataruhusiwa kuunga umeme kwenye maeneo mbalimbali bila kuunga mfumo wa solar kwa ajili ya mashine ya kupashia maji.

Zimbabwe imekuwa gizani kwa muda mrefu umeme ukikatika mara kwa mara huku biashara nyingi zikifanyika nyakati za usiku, wakati umeme unapokuwa umewaka.

Sababu nyingi zimetolewa kuhusu kukosekana kwa umeme.Kampuni ya serikali ya kusambaza umeme ,Zesa imesema wateja wakubwa hawajalipia huduma za umeme. Wakati huo huo ukame umepunguza kiasi cha maji kwenye bwawa la maji linalozalisha umeme.

Kwanini Zimbabwe imefikia hali hii?

Zimbabwe inategemea bwawa moja tu la Kariba la kuzalisha umeme lakini limeshindwa kusambaza umeme kama kawaida kwa sababu ya kushuka kwa kina cha maji kulikosababishwa na ukame.

Zimbabwe inahitaji umeme wa Megawati 1,700 kila siku kukidhi mahitaji ya watumiaji wake.

Kituo cha umeme cha Hwange nacho kina matatizo, kwani miundombinu yake ni kuukuu.

Shirika la Umeme Zesa nalo linashindwa kununua umeme kwenye nchi jirani kwa kuwa limeshindwa kulipa madeni ya umeme kwa Afrika Kusini na Msumbiji.

Zimbabwe inafanya jitihada za kumudu hali ya kukatika kwa umeme wakati hali ya kiuchumi ikiendelea kuwa mbaya na hofu ya mfumuko mkubwa wa bei.

Kwa serikali na familia wakipambana kulipa gharama za bili, watoto wengi wanafanya kazi za shule kwa mwanga wa mshumaa.

Kwa kipindi cha mwezi Juni, mishumaa ilikuwa ikiwashwa baada ya jua kuzama ili waweze kumaliza kazi zao za shule.

Umeme ulikuwa ukirejea wakiwa wamelala majira ya saa nne za usiku, saa za Zimbabwe.

Nyumba nyingi zimekumbwa na changamoto hiyo isipokuwa tu kwa wale wanaoweka majenereta na solar- lakini ni vigumu kwa wanaotumia majenereta wakati wote kwa sababu ya upungufu wa mafuta ya dizeli na mistari mirefu kwenye gereji.

Umeme wa solar ni njia pekee inayokua kwa sasa- vifaa vya umeme wa solar vimekuwa vikiongezeka kwa kasi katika nyumba za raia wa Zimbabwe.

Huenda Zimbabwe itaendelea kuwa gizani kwa siku nyingi zijazo.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?