Je vikwazo vya Marekani ndio sababu ya maandamano haya?

Maandamano yamezuka katika maeneo tofauti nchini Iran bada ya serikali kutangaza ghafla mpango wa kuuza mafuta kwa mgao na kuongeza bei ya bidhaa hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la kitaifa bei ya mafuta ilipanda kwa 50% siku ya Ijumaa.

Mamlaka imepunguza ruzuku kubwa kwa bei ya petroli kukabiliana na athari ya vikwazo vya Marekani ambavyo vimeathiri vibaya uchumui wa Iran.

Iran iliwekewa vikwazo vya kuuza mafuta yake nje ya nchi baada ya Marekani kujiondoa katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia mwaka 2018.

Shirika la habari la Iran IRNA limeripoti maandamano "makali" katika eneo la Sirjan, kati kati ya Iran, usiku wa Ijumaa huku watu "wakisjhambulia bohari ya kuhifadhi mafuta katika mji huo na kujaribu kuliteketeza moto".

Mtu mmoja aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, chombo kingine cha habari kisichokuwa rasmi ISNA kilimnukuu gavana wa jimbo la Sirjan.

Maandamano pia yalizuka katika miji mingine kama vile Mashhad, Birjand, Ahvaz, Gachsaran, Abadan, Khoramshahr, Mahshahr, Shiraz na Bandar Abbas, iliongeza.

Katika mji wa Mashhad,ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Iran, waandamanaji waliojawa na hasira walifunga bara bara kwa kukutumia magari yao, shirika la habari la AP liliripoti likinukuu IRNA.

Kanda za video zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zinawaonesha madereva wa magari waliojipata katika msongamano mkubwa wa magari katika mji mkuu wa Tehran, wakiomba polisi iwasaidie.

Kanda nyingine ambayo inaashiria kufungwa kwa baa bara ya Tehran-Karaj pia imekuwa ikisambazwa mitandaoni.

Chini ya utaratibu huo mpya kila dereva anaruhusiwa kununua lita 60 ya mafuta ya petroli kwa mwezi ambayo ni riali 5,000 sawa na($0.13; £0.10) kwa lita.

Atakayeongeza mafuta zaidi ya kiwango kilichowekwa kwa mwezi atatozwa rial 30,000 za Iran.

Awali madereva waliruhusiwa kununua petroli hadi lita 250 kwa riali 10,000 kili alita, shirika la habari la AP liliripoti.

Fedha zitakazotokana na mauzo ya mafuta ya ziada zitatumiwa kuwalipa watu wa mapato ya chini , serikali imesema.

Mkuu wa idara ya mipango ya bajeti, Mohammad Baqer Nobakht, amesema kuanzia mwezi huu, familia milioni 18 zitapokea fedha zaidi kutokana na hatua ya kuongeza bei mafuta.

Hatua hiyo mpya inatarajiwa kuisaidia serikali kukusanya jumla ya riali 300tn kwa mwaka, alisema katika televisheni ya kitaifa.

Rais Hassan Rouhani alisema siku ya Jumamosi kuwa 75% ya raia wa of Iran wanakabiliwa na "hali ngumu" na kwamba mapato zaidi kutokana na nyongeza ya bei ya petroli itawasaidia moja kwa moja wala sio hazina kuu ya nchi, ripoti ya shirika la habari la AFP zinasema.

Mafuta bei nafuu

Iran imetajwa kuwa na bei ya chini ya mafuta duniani kutokana na ruzuku ya serikali na kushuka thamani kwa sarafu yake.

Pia ni moja ya nchi inayozalisha mafuta kwa wingi duniani, ambayo thamani yake inaiingizia nchi hiyo mabilioni ya madola kila mwaka.

Rais wa Marekani Donald Trump aliiwekea upya vikwazo Iran mwaka jana baada ya kujiondoa katika mkataba wa kimataifa wa nyukli mwaka 2015 ambao ulihusisha Irana na mataifa mengine sita yalio na uchumi mkubwa duniani.

Chini ya mkataba huo, Iran ilikubali kudhibiti shughuli zake za nyuklia na kukubali wakaguzi wa kimataifa kufuatilia hatua hiyo ili kulegezewa vikwazo hivyo, ambavyo vimeathiri pakubwa uchumi wa nchi hiyo.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?