Vita vya Syria. Wanajeshi wa Uturuki 33 wauawa katika mashambulio Idlib

Takriban askari 33 wa Uturuki wameuawa katika mashambulio ya anga ya "vikosi vya Syria" Kaskazini-Magharibi mwa Syria, amesema afisa wa ngazi ya juu wa Uturuki .

Wengi waliumizwa katika jimbo la Idlib, amesema Rahmi Dogan, Gavana wa jimbo la Uturuki la Hatay. Taarifa nyingine zinasema idadi ya vifo ni ya juu zaidi.

Uturuki kwa sasa inajibu kwa kuyalenga kushambulia dhidi ya maeneo ya vikosi vya Uturuki.

Vikosi vya Syria vinavyoungwa mkono na Urusi vinajaribu kurejesha jimbo la Idlib ambalo kwa sasa linadhibitiwa na waasi wanaosaidiwa na wanajeshi wa Uturuki

Maafisa nchini Syria bado hawajatoa kauli yao wazi kuhusu mapigano ya sasa ya Idlib, ambalo ni jimbo la mwisho lililosalia mikononi mwa upinzani.

Jeshi la Uturuki lilianza kupiga maeneo ya Syria baada ya Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan kufanya mkutano na maafisa wa ngazi ya juu wa usalama mjini Ankara.

Jimbo la Idlib

Kiongozi wa Uturuki anataka vikosi vya Syria virudi nyuma kutoka kwenye maeneo ambayo Uturuki imeweka vituo vya uchunguzi na awali ilitishia kuvishambulia kama haitaacha mashambulio yake.

Lakini serikali ya Syria na Urusi zimekataa madai yake ya kurudi nyuma kwenye mistari ya usitishaji mapigano iliyokubaliwa mwaka 2018. Urusi pia imeishutumu Uturuki kwa kukiuka makubaliano ya mwaka 2018 ya usitishaji mapigano kwa kuwaunga mkono waasi kwa kufyatua makombora.

Waangalizi wa haki za binadamu nchini Syria wenye makao yao makuu nchini Uingereza,The UK-based monitor, the Syrian Observatory for Human Rights, wamesema kuwa wanajeshi 34 wa Uturuki waliuawa Alhamisi katika mashambulio ya anga jana jioni.

Waliojeruhiwa wamerudishwa nchini Uturuki kwa ajili ya matibabu, amesema Bw. Dogan.

"Yote yanajulikana"maeneo ya serikali ya Syria yalishambuliwa na ndege za Uturuki na vikosi vya ardhini, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Uturuki Fahrettin alinukuliwa na Shirika la habari la taifa Anadolu akisema. Uturuki ilikua imeamua ku "jibu kwa ukarimu" mashambulio, alisema Bw, Altun.

Wakati huo huo ,Uturuki ambaye ni mjumbe wa Muungano wa kujihami wa nchi za Magharibi Nato imesema waziri wake wa mambo ya nje Mevlut Cavusoglu amezungumza na katibu mkuu wa muungano wa Nato -Generali Jens Stoltenberg.

Uwanja sasa umewekwa tayari kwa ajili ya makabiliano kamili baina ya Uturuki na Syria.

Hii inaacha maswali mengi ya kila aina.

Je utawala wa Ankara au Damascus utasitisha mapigano? Utawala wsa Moscow- ambao umeegemea upande mmoja katika mzozo huu unaweza kushawishi pande husika kusitisha mapigano?

Na je kuna njia ya kuushawishi utawala wa Syria kuacha mashambulio yake makubwa katika jimbo la Idlib.?

Hili linaonekana kutiliwa shaka kwani rais Bashar al-Assad anaonekana ameazimia kuchukua tena udhibiti wa eneo hilo, na Urusi tayari imekua ikimuunga mkono hadi sasa.

Na vipi juu ya janga la kibinadamu linaloendelea ?

Uturuki tayari imekwisha wapokea wakimbizi milioni 3.7

Hili sasa limegeuka kuwa suala lenye utata katika siasa za ndani ya Uturuki, na hasira ya Uturuki inaweza kuifanya itume wimbi la wakimbizi Ulaya

Makabiliano ya hivi karibuni yanakuja baada ya waasi wanaoungwa mkono na Uturuki kusema kuwa walichukua tena mji muhimu wa Saraqebkutoka kutoka kwa vikosi vya serikali Alhamisi.

Mapigano katika Idlib yamewafurusha raia wa Syria karibu milioni moja kutoka kwenye makazi yao tangu mwezi Disemba mwaka jana. Umoja wa Mataifa unasema kuwa mapigano kamili kuhusu udhibiti wa Idlib yanaweza kusababisha'' umwagaji damu wa hali ya juu.''

Shirika la habari la Reuters lilimnukuu afisa wa Uturuki Alhamisi akisema kuwa Uturuki ilikua imeamua kuwaondoa walinzi wake wa mpaka na kutowazuia wakimbizi wa Syria kujaribu kuingia Ulaya. Hata hivyo hilo bado halijathibitishwa rasmi.

Mapama Jumatatu, Bw. Eldogan alisema kuwa wanajeshi wa Uturuki wameuawa katika mashambulio ya anga yaliyopigwa Idlib.

Wizara ya ulinzi ya Uturuki imesema kuwa ililazimika kujibu tukio kwa kupiga ''maeneo ya utawala'' wa Syria.

Urusi imekataa wa Baraza la Usalama la Umoja wa Matifa likiitaka kusitisha mapigano Kaskazini mwa Syria kwa ajili ya kutolewa kwa huduma za kibinadamu Kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa ya Ubelgiji na Ujerumani juu ya mashambulio imesema kuwa mauaji ya raia lazima yakome, Balozi wa Urusi wamesema kuwa suluhu pekee ni kufukuza kile alichokiita magaidi kutoka nchini Syria.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?