Corona Virus:Dunia lazima ijiandae kwa janga, WHO yasema

Shirika la afya duniani limesema dunia inapaswa kujiandaa kwa uwezekano wa janga la virusi vya corona.

WHO linasema ni mapema sana kuuita mlipuko wa virusi hivyo janga lakini nchi zinapaswa kuwa katika "awamu ya maandalizi".

Janga ni pale maambukizi ya ugonjwa yanaposambaa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine katika maeneo mengi ya dunia.

Visa zaidi vya virusi ambavyo husababisha ugonjwa kupumua Covid-19, vinaendela kujitokeza, huku milipuko ya ugonjwa huo ikibainika katika mataifa ya Korea Kusini , Italia na Iran ikisababisha.

Hata hivyo , maambukizi mengi yanapatikana nchini Uchina, chanzo cha asili ya virusi, ambako watu zaidi ya 77,000 wamepata maradhi hayo na zaidi ya 2,600 wamekufa.

Zaidi ya visa 1,200 vimethibitishwa katika nchi 30 na kumekuwa na vifo zaidi ya 20. Italia iliripoti vifo vinne zaidi Jumatatu, na kuifanya idadi ya vifo nchini humo kufikia watu saba.

Masoko ya hisa yalishuka kote duniani kwasababu ya hofu ya athari za kiuchumi.

Uchina ilisema itaahirisha mkutano wa mwaka wa taifa uliotarajiwa kufanyika mwezi ujao ili "kuendelea na juhudi" za kupambana dhidi ya virusi vya corona.

Mkutano huo unaochukua maamuzi ya chama tawala cha Kikomunisti, umekua ukikutana kila mwaka tangu 1978.

Uwiano wa watu walioathirika waliokufa kutokana na Covid-19 vinaonekana kuwa kati ya 1% na 2%, ingawa WHO inaonya kwamba kiwango cha vifo hakijafahamika bado.

Jumatatu Iraq, Afghanistan, Kuwait, Oman na Bahrain ziliripoti visa vyake vya kwanza , vyote vikiwahusisha watu waliokua wamewasili kutoka Iran. Maafisa wa Bahrain walisema mgonjwa aliyeathiriwa na virusi hivyo alikua ni dereva wa basi la shule, na shule kadhaa zimefungwa kutokana na kisa hicho.

Je WHO inasema nini?

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu kwamba idadi ya visa vya Corona katika siku za hivi karibuni katika mataifa ya Iran, Italia na Korea Kusini vina "tisha sana''.

Hata hivyo aliongeza kuwa : "Kwa sasa hatushuhudii kiwango kibaya cha ugonjwa au vifo.

" Je ugonjwa huu una uwezekano wa kuwa janga? Kabisa, unaweza. Je bado haujawa kutokana na tathmini yetu? Kutokana na tathmini yetu, bado haujawa."

Ujumbe muhimu ambao unaweza kutoa matumaini kwa nchi, kutia moyo na kuzipa guvu ni kwamba virusi hivi vinaweza kudhibitiwa, kusema ukweli kuna nchi nyingi ambazo zimefanya hilo ," alisema Bw.

"Kutumia neno 'janga' kwa sasa haifai kwasababu ukweli ni kwamba inaweza kusababisha hofu."

Lakini Mike Ryan mkuu wa mpango wa dharura wa afya wa WHO ,amesema sasa ni muda wa "kufanya kila liwezekanalo kujiandaa kwa janga ".



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?