Ubalozi wa Marekani waonya dhidi ya shambulio la kigaidi katika hoteli moja Nairobi Kenya

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umetoa onyo kwamba magaidi huenda wakashambulioa hoteli moja kubwa nchini Nairobi.

Kulingana na ubalozi huo, hoteli iliolengwa ni maarufu kwa kuwa hutemebelewa sana watalii na wanabiashara.

''Makundi ya kigaidi huenda yanapanga njama dhidi ya hoteli moja kubwa mjini Nairobi. Hoteli inayolengwa haijatambulishwa lakini inaaminika kuwa hoteli ilio maarufu sana na watalii na wafanyabiashara wa kigeni'', lilisema onyo hilo.

Wakenya wameshauriwa kuwa waangalifu wakati wanapotembelea ama kuishi katika hoteli mjini Nairobi.

''Unapokuwa unaishi katika hoteli jifahamisheni kuhusu njia za kutorokea . Panga mapema jinsi utakavyoweza kutoroka katika hoteli iwapo kutakuwa na dharura yoyote'', liliongezea onyo hilo.

Wakati huohuo Inspekta jenerali wa polisi nchini Kenya Hilary Mutyambai amewaomba Wakenya kuwa watulivu , akisema idara ya polisi imeimarisha usalama nchini kote mbali na kulinda mipaka yote.

Hatahivyo amewataka Wakenya kuwa makini na kushirikiana na polisi pamoja na vitengo vingine vya usalama dhidi vitendo vyovyote vinavyozua shauku.

''Kufuatia kuimarishwa kwa usalama kote nchini Wakenya wametakiwa kuendelea na shughuli zao za kila siku bila ya hofu''.

''Vilevile amewataka kuripoti chochote wanachokishuku kupitia nambari ya 999,911 na 112'', alisema mkuu huyo wa polisi katika taarifa yake.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?