Mkanyagano wasababisha vifo vya wanafunzi 13 Kenya

Wanafunzi 13 wa shule ya msingi Kakamega nchini Kenya wamefariki baada ya kupata taharuki na kukanyagana shuleni.

Mkuu wa kituo cha polisi cha Kakamega ,bwana David Kabena amesema kuwa wanafunzi wengine 39 walijeruhiwa na 20 wamepata huduma ya afya tayari.

Inadaiwa kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

Zaidi ya wanafunzi 100 wanatibiwa na wengine wako kwenye hali mbaya.

Mkanyagano huo ulitokea baada ya kengele ya kumaliza masomo kupigwa na wanafunzi walikuwa wakitoka kuelekea nyumbani.

Ripoti zinasema kuwa wanafunzi hao walikuwa wakitoka katika madarasa yao mwendo wa saa kumi na moja jioni wakati mkasa huo ulipotokea.

Imedaiwa kwamba baadhi yao walianguka kutoka ghorofa ya tatu ya jengo hilo walipokuwa wakitoka darasani.

Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa wanafunzi wawili wamepelekwa katika chumba cha dharura katika hospitali iliyopo kaunti ya Kakamega.

Wazazi wamekusanyika hospitalini wakiwa na hofu kuwa inawezekana kuna wanafunzi wengi zaidi wamejeruhiwa.

Wengi waliumia wakati wakijaribu kutoka kwenye jengo la shule.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?