Tanzania yapigwa marufuku bahati nasibu ya viza Marekani

Serikali ya Marekani imepiga marufuku raia wa Tanzania kushiriki katika bahati nasibu wa kupata viza ya kuingia Marekani.

Hatua hiyo inakuja saa chache baada ya serikali ya Trump kumpiga marufuku

Bahati nasibu hiyo hutoa viza kwa watu takribani 50,000 kutoka nchi zenye kasi ndogo ya maendeleo kila mwaka kuingia na kufanya kazi Marekani.

Nchi ya Sudani pia raia wake wamepigwa marufuku kuingia katika bahati nasibu hiyo.

Wakati huo huo raia wa nchi nne ikiwemo mbili za Afrika Nigeria na Eritrea wamepigwa marufuku kabisa kuomba viza za kuhamia Marekani.

Marufuku hiyo pia itazihusisha nchi za Myanmar na Kyryzstan.

Hata hivyo raia wa nchi hizo ambao watataka kuingia Marekani kwa kutalii ama biashara wataruhusiwa.

Afisa wa ngazi ya juu nchini Marekani amesema kuwa nchi hizo sita zimeshindwa kufikia "kiwango stahiki cha ulinzi na kupashana taarifa".

"Nchi hizi, kwa sehemu kubwa, zinataka kutoa msaada lakini kwa sababu mbali mwali zimefeli kufikia viwango vya chini tulivyoviweka," Naibu Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Chad Wolf amewaambia wanahabari siku ya Ijumaa.

Bwana Wolf amesema maafisa wa Marekani watakuwa tayari kushirikiana na nchi hizo sita ili kuimarisha matakwa ya ulinzi kwa nchi hizo ili iwasaidie kutoka kwenye listi hiyo.

Nchi hizo mpya zinaungana na nchi nyengine saba ambazo raia wake wamepigwa marufuku kuingia Marekani toka mwaka 2017.

Nchi hizo, nyingi zikiwa na raia wengi Waislamu ni Libya, Iran, Somalia, Syria, Yemen.

Aidha nchi za Korea Kaskazini na Venezuela pia zimo kwenye marufuku hiyo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?