Vita vya Syria: Serikali ya Syria itajuta kwa kuwashambulia wanajeshi wa Uturuki

Rais wa Uturuki ameionya serikali ya Syria kwamba italipa gharama kubwa kwa mashambulio dhidi ya wanajeshi wake katika eneo la kaskazini mashariki mwa Syria.

Wanajeshi watano wa Uturuki waliuawa katika mji wa Idlib unaodhibitiwa na upinzani siku ya Jumatatu huku jeshi la Syria likiendelea kusonga mbele katika eneo la vita.

Wanajeshi wa Uturuki walifyatua makombora kadhaa ili kujibu shambulio hilo , lakini rais Recep Tayyip Erdogan alisema: Tutaendelea na mashambulizi.

Wakati huohuo wanajeshi wa Syria walikaribia kuikomboa barabara ya eneo la kaskazini la taifa hilo.

Shirika la haki za kibinadamu lenye makao yake huko Uingereza SOHR liliripoti siku ya Jumanne kwamba wanajeshi wa Syria waliwafurusha waasi na wapiganaji wa kijihad kutoka eneo la mwisho ambalo walikuwa wakidhibiti magharibi mwa mji wa Aleppo.

Hatahivyo hakuna thibitisho kutoka kwa jeshi ama vyombo vya habari vya serikali na kwamba kulikuwa na ghasia katika maeneo kadhaa ya barabara hiyo kuu siku ya Jumanne jioni.

Serikali haijafanikiwa kudhibiti eneo lote la barabara hiyo , ambayo inaunganisha mji wa Aleppo na mji mkuu wa Damscus mbali na mpaka na taifa la Jordan tangu 2012.

Pia siku ya Jumanne , helikopta ya serikali iliripotiwa kudunguliwa karibu na kijiji cha Nayrab kusini mashariki mwa mji unaodhibitiwa na upinzani wa Idlib , na kuwauwa wafanyakazi wake.

Kanda za video zilionekana zikionyesha helikopta hiyo ikichomeka moto kabla ya kuanguka ardhini.

Wakati huohuo raia 12 , sita wakiwa watoto waliuawa na wengine 30 kujeruhiwa katika shambulio lililofanyika katika eneo la sanaa na jalaa la mji wa Idlib, kulingana na SOHR

Uturuki inayowasaidia wapinzani wa serikali ya Syria imetuma wanajeshi katika eneo la Idlib chini ya makubaliano na washirika wa serikali ya Syria Urusi na Iran katika makubaliano ya Astana na Sochi.

Hatua hiyo inalenga kupunguza uhasama. Kufikia sasa mwezi huu , mashambulio ya Syria yamewauwa wanajeshi 12 wa Uturuki na mwanakandarasi mmoja.

Wizara ya ulinzi nchini Uturuki imesema kwamba wanajeshi wa Uturuki walijibu shambulio la Jumatatu kuyalenga maeneo 115 ya serikali ya Syria na kuwapokonya bunduki wanajeshi 101.

Hatrahivyo jeshi la Syria halikuripoti majeruhi yoyote. Katika hotuba yake mjini Ankara siku ya Jumanne , rais wa Uturuki Erdogan alisema: Tulitoa jibu mwafaka kwa serikali ya Syria kwa kiwango cha juu. Hususan mjini Idlib, walipata kile walichohitaji. Lakini hii haitoshi. Mashambulio yataendelea.

''Kila wanapozidi kushambulia wanajeshi wetu, ndio gharama ya juu watakayozidi kupata. Tutaambia umma wetu kuhusu hatua tulizochukua kesho'', aliongezea.

Jeshi la Syria linasema wanajeshi wake ambo wmeungwa mkono na wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran pamoja na Urusi wamekomboa zaidi ya kilomita 600 mraba na kutoa uhuru kwa makumi ya miji na vijiji katika siku za hivi karibuni.

Takriban rais 373 wameuawa huku wengine 689,000 wakitoroka makwao tangu vita hivyo vianze mnamo mwezi Disemba kulingana na Umoja wa mataifa.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?