Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 09.02.2020: Grealish, Messi, Sterling, Pochettino, Coutinho, De Bruyne, Bale
Grealish angependelea kujiunga na Manchester United katika msimu wa usajili ujao iwapo ataondoka Aston Villa licha ya tetesi kwamba Barcelona na Real Madrid wameashiria kuwa na nia ya kumsajili. (Sun)
Manchester City wako tayari kukubali kushindwa katika harakati zao za kumpata Lionel Messi katika msimu ujao wa ligi ya Premier baada ya kuarifiwa kwamba mshambuliaji huyo wa Argentina, 32, hana mpango wa kuondoka Barcelona. (Express)
Mchezaji wa Manchester City Raheem Sterling anaamini kwamba atakuwa sawa katika Champions League kwenye mechi dhidi ya Real Madrid, ambao wanataka kumsajili mshambuliaji huyo, 25. (Telegraph)
Aliyekuwa meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino bado hajafikia makubaliano ya kuwa meneja wa Manchester United ajaye msimu ujao.
Kiungo wa kati wa Barcelona raia wa Brazil midfielder Philippe Coutinho, 27 ambaye kwasasa yuko Bayern Munich kwa mkopo, ataruhusiwa kuondoka kwa £77m ikiwa ni kiasi kidogo cha pesa huku Manchester United na iliyokuwa klabu yake Liverpool zikisemekana kuwa na nia ya kumsajili. (Express)
Kiungo wa kati wa Manchester City raia wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 28, anayehusishwa na Real Madrid na Barcelona, amesema kwamba anaridhishwa na mabingwa wa sasa wa Ligi ya Premier. (Goal.com)
Mshambuliaji Gareth Bale, 30, alitaka kuboresha soka ya Uchina aliposemekana kuhamia Asia kipindi cha usajili cha 2019, lakini kwasasa anapanga kusalia at Real Madrid wala hatarejea katika Ligi ya Premier na klabu aliyokuwa akichezea Tottenham. (Goal.com)
Aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey, 29, anasemekana kwamba huenda akaondoka Juventus, akiwa amesaini mkataba wa miaka minne pekee na Italia mwaka jana. (Calciomercato - in Italian).

Maoni
Chapisha Maoni