Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2026

Wanasiasa 7 barani Afrika wanaokabiliwa na mashtaka ya uhaini.

Picha
Usomaji maandishi tu kupunguza gharama za data Iliyochapishwa 22 Septemba 2026 Muda wa kusoma: Dakika 5 Kesi za hivi karibuni zinazohusisha mashtaka ya uhaini au vitendo vinavyotishia usalama wa taifa, ambapo wanasiasa mashuhuri barani Afrika wamekuwa wakishtakiwa, zimeibua maswali kuhusu iwapo walio madarakani wanalinda kweli usalama wa taifa, au wanatumia mfumo wa haki kudhoofisha wapinzani wao wa kisiasa au watu wengine wanaoonekana kuwa tishio. Katika kesi hizi, washtakiwa au wafuasi wao mara nyingi hudai kuwa mashtaka hayo yana misukumo ya kisiasa, huku wakikanusha tuhuma zinazowakabili. Kwa upande mwingine, viongozi wa serikali wanasema kuwa mahakama ni huru na mamlaka za sheria zina uhuru wa kumchukulia hatua mtu yeyote wanayeona anapaswa kushtakiwa. Hizi ni kesi saba za hivi karibuni zinazohusisha watu wanaotuhumiwa kwa uhaini. 1. Burundi: Alain-Guillaume Bunyoni Alain-Guillaume Bunyoni, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Burundi, alihukumiwa kifungo cha maisha mwezi Disemba mwaka wa 202...

Mafuriko na maporomoko ya ardhi yaua 15 India, 4 Nepal

Picha
CHANZO CHA PICHA, REUTERS Mvua kubwa na dhoruba zimesababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini India na nchi jirani ya Nepal, na kusababisha vifo vya angalau watu 19, huku wafanyakazi 10 wakiripotiwa kutoweka baada ya mito kufurika na kuvunja kingo zake. Katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India, watu 15 wamefariki na watano kujeruhiwa katika kipindi cha saa 48 zilizopita, huku nyumba 117 zikiharibiwa, mamlaka za jimbo hilo zimesema kupitia taarifa kwa umma. Nchini Nepal, watu wanne, wakiwemo watoto watatu na mwanamke mmoja, wamefariki baada ya maporomoko ya ardhi kuifunika nyumba yao walipokuwa wamelala katika kijiji cha Nishi Khola, wilayani Baglung. Wafanyakazi 10 wa Nepal pia hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya theluji kuifunika kambi ya chini ya mlima Himlung Himal yenye urefu wa mita 7,126, katika wilaya ya Manang kaskazini mwa Nepal. Wafanyakazi hao walikuwa wakijenga mahema kwa ajili ya wapanda milima kutoka mataifa ya kigeni, ambao hawakuwepo wakati maporomoko ha...