Mafuriko na maporomoko ya ardhi yaua 15 India, 4 Nepal


.

Mvua kubwa na dhoruba zimesababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini India na nchi jirani ya Nepal, na kusababisha vifo vya angalau watu 19, huku wafanyakazi 10 wakiripotiwa kutoweka baada ya mito kufurika na kuvunja kingo zake.

Katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India, watu 15 wamefariki na watano kujeruhiwa katika kipindi cha saa 48 zilizopita, huku nyumba 117 zikiharibiwa, mamlaka za jimbo hilo zimesema kupitia taarifa kwa umma.

Nchini Nepal, watu wanne, wakiwemo watoto watatu na mwanamke mmoja, wamefariki baada ya maporomoko ya ardhi kuifunika nyumba yao walipokuwa wamelala katika kijiji cha Nishi Khola, wilayani Baglung.

Wafanyakazi 10 wa Nepal pia hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya theluji kuifunika kambi ya chini ya mlima Himlung Himal yenye urefu wa mita 7,126, katika wilaya ya Manang kaskazini mwa Nepal.

Wafanyakazi hao walikuwa wakijenga mahema kwa ajili ya wapanda milima kutoka mataifa ya kigeni, ambao hawakuwepo wakati maporomoko hayo yalipotokea.

Mamlaka nchini Nepal zimeonya kuhusu uwezekano wa mafuriko ya ghafla katika wilaya 49 kati ya 77.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Kwanini Somaliland ina matumaini na ujio wa Trump?

Maandamano Kenya: 'Msiwaue, wapigeni risasi mguuni' Ruto awaambia polisi

Urusi yatetea uzinduzi wa satelaiti wa Iran