wachezaji wa Ireland wakataa kusalimiana na timu ya Israel.

  1. Wachezaji wa Ireland wakataa kusalimiana na timu ya Israel

    .
    Maelezo ya picha,Wachezaji wa Ireland waliinamisha vichwa vyao wakati wa wimbo wa taifa wa Israel kabla ya mechi.

    Kocha wa Jamhuri ya Ireland, Heimir Hallgrímsson, amesema wachezaji wake walivutia hisia duniani baada ya kukataa kutekeleza baadhi ya taratibu za kawaida kabla ya mechi yao dhidi ya Israel.

    Kabla ya mchezo huo uliochezwa Hungary na kumalizika kwa ushindi wa mabao 3-0 kwa Ireland, wachezaji wa Jamhuri ya Ireland na Israel hawakusalimiana kwa kupeana mikono. Aidha, wachezaji wa Ireland waliinamisha vichwa vyao wakati wimbo wa taifa wa Israel ukipigwa.

    Nahodha wa Ireland, Dara O'Shea, na mwenzake wa Israel, Manor Solomon, pia hawakusalimiana kabla ya mechi, huku timu hizo mbili zikikosa kubadilishana bendera za kumbukumbu kama ilivyo kawaida.

    Tangu droo ya Kundi B3 ilipofanyika mwezi Februari, mechi kati ya timu hizo zimezua mjadala kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Israel na Gaza.

    Awali, baadhi ya wachezaji wa Ireland walikabiliwa na wito wa kujiondoa kwenye mashindano hayo, huku kampeni ya "Stop the Game", iliyoandaliwa na kundi la Irish Sport for Palestine, ikipata uungwaji mkono mkubwa katika wiki za hivi karibuni.

    Pia unaweza kusoma:

  2. Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Nyota wa Chelsea Estevao kwenye rada za Barcelona

    .

    Winga wa Brazil Estevao Willian anazidi kukerwa na ukosefu wa muda wa kucheza Chelsea, huku Barcelona ikifuatilia kwa karibu hali ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 19. (Sport - in Spanish)

    Mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, anayekipiga kwa sasa Al-Nassr, amesema angependa kurejea kucheza soka barani Ulaya, ingawa hajataja klabu anayotamani kujiunga nayo. (AS - in Spanish)

    Nyota wa Norway Erling Haaland, 26, ameanza kuvutia macho ya Arsenal na Real Madrid kutokana na hali ya sintofahamu inayoikabili Manchester City. (Football Insider)

    Newcastle United inamfuatilia beki wa Morocco Abdelhamid Ait Boudlal, 20, wa Rennes, lakini itakumbana na ushindani kutoka Everton, Brentford na Hull City. (Teamtalk)

    Arsenal na Tottenham Hotspur zinatajwa kufuatilia kiungo wa Algeria Ibrahim Maza, 20, wa Bayer Leverkusen. (Teamtalk)

    Chelsea inamuwania beki wa kushoto wa England Tyrick Mitchell, 27, wa Crystal Palace, lakini pia inakabiliwa na ushindani kutoka Manchester United na Liverpool. (Caught Offside)

    Leeds United haina mpango wa kumuuza beki wa Wales Ethan Ampadu, 26, licha ya taarifa zinazomhusisha na kurejea katika klabu yake ya zamani ya Chelsea. (Football Insider)

    Soma Zaidi:

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Kwanini Somaliland ina matumaini na ujio wa Trump?

Maandamano Kenya: 'Msiwaue, wapigeni risasi mguuni' Ruto awaambia polisi

Urusi yatetea uzinduzi wa satelaiti wa Iran