Virusi vya corona: Dkt Anthony Fauci atahadharisha kuwa Marekani itakuwa na visa 100,000 kwa siku

Mtafiti mkuu wa magonjwa Dkt Anthony Fauci ameliambia bunge la seneti nchini Marekani kuwa ''hatashangazwa'' ikiwa maambukizi mapya yatafikia 100,000 kwa siku.
''Ni wazi hatujaudhibiti kwa sasa,'' alikiri, akitoa tahadhari kuwa haitoshi kwa Wamarekani kuvaa barakoa na kutochangamana
Katika hotuba yake, alisema kuwa karibu nusu ya watu wote wapya walioambukizwa wanatoka katika majimbo manne.
Awali, Gavana wa New York alisema karibu nusu ya Wamarekani wote lazima wajiweke karantini ikiwa watatembelea jimbo hilo.
Siku ya Jumanne, idadi ya watu walioambukizwa iliongezeka kwa zaidi ya 40,000 kwa siku moja kwa mara ya nne katika kipindi cha siku tano.
Ongezeko- ambalo limekuwa kubwa katika majimbo ya Kusini na Magharibi limelazimu majimbo karibu 16 kusitisha na kutazama upya mipango yao ya kuyafungulia majimbo hayo, kwa mujibu wa shirika la habari la CNN.
Florida, Arizona,Texas na California ni majimbo manne yaliyotolewa mfano na Dkt Fauci kuwa majimbo yaliyoathiriwa zaidi na virusi vya corona kwa sasa.
Kwa baadhi hatua mpya zimekuja katika kipindi cha mwezi mmoja baada ya kufungua tena shughuli za kiuchumi
Pia siku ya Jumanne , Gavana wa New York Andrew Cuomo iliongeza idadi ya Wamarekani ambao wanatakiwa kujiweka karantini kwa siku 14 ikiwa watatembelea jimbo hilo. Kwa sasa kuna majimbo 16 kwenye orodha.
Majimbo mapya yaliyo kwenye orodha ni pamoja na California, Georgia, Iowa,Idaho, Lousiana, Mississippi, Nevada na Tennessee.
Yanaungana na Alabama, Arkansas, Arizona, Florida, North Carolina, South Carolina, Texas na Utah.
Yote kwa pamoja, yanagusa 48% ya wakazi wote wa Marekani kwa mujibu wa wataalamu.
Fauci amesema nini?
Akizungumza mbele ya kamati ya bunge la seneti katika jitihada za kufungua tena shule na biashara, Mkurugenzi wa taasisi ya kitaifa ya uzio na magonjwa ya kuambukiza alikosoa majimbo hayo kwa ''kupuuza'' taratibu zinazohitajika kufuatwa wakati wa mchakato wa kufungua tena shughuli, na matokeo yake maambukizi yataongezeka.
''Siwezi kukisia , lakini hali itakuwa ya kutamausha, ninaweza kuwahakikishia hilo,'' alimwambia seneta Elizabeth Warren.
''Kwasababu ikiwa una mlipuko wa ugonjwa katika sehemu moja ya nchi hata kama maeneo mengine ya nchi yanafanya vyema, pia wanakuwa hatarini.''''Hatuwezi kuzingatia tu maeneo ambayo yana maambukizi ya hali ya juu. Inaweka nchi nzima katika hatari,'' aliongeza.
Dkt Fauci ameitaka serkali ya Marekani kuzalisha barakoa na kuzisambaza bure kwa Wamarekani wote, na kukemea baadhi ya watu ambao hawazingatii kanuni za kutochangamana.
Robert Redfield, Mkurugenzi wa Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) ambaye pia alitoa maelezo yake siku ya Jumanne, aliwaambia wabunge kuwa majimbo 12 yameshuhudia idadi ya wagonjwa wanaolazwa hospitali ikiongezeka na jimbo la Arizona limerekodi ongezeko la idadi ya watu wanaofariki.
Kabla ya kumsikiliza Dkt Fauci, Seneta wa chama cha Republican Lamar Alexander, anayeongoza kamati hiyo, alitoa wito kwa Rais Donald Trump kuvaa barakoa- kitendo ambacho hakifanyi anapokuwa kwenye shughuli zinazokusanya Umma.
''Inasikitisha hatua rahisi ya kuokoa maisha imekuwa sehemu ya mjadala wa kisiasa,'' alisema mshirika wa Trump.
''Kama unamuunga mkono Trump huvai barakoa, kama haumuungi mkono unavaa,'' aliendelea, akisema kuwa ''rais huvaa barakoa mara chache''.
''Rais ana watu wengi wanaompenda ambao wanafuata mfano wake,'' alisema.
'Tuna maambukizi makubwa sana ya virusi'
Siku ya Jumatatu, Dkt Anne Schuchat, Naibu Mkurugeni wa CDC alitahadharisha kuwa Marekani haichukui hatua kama nchi nyingine ambazo zimeonesha kupiga hatua kudhibiti virusi vya corona, na imeruhusu kusambaa sana kwa virusi na kwa kasi kubwa.
''Si kama hali ilivyo New Zealand au Singapore au Korea ambako mtu mmoja anapoambukizwa hutambulika na kufanya ufuatiliaji wa watu aliochangamana nao na watu wanatengwa na watu walioambukizwa huwekwa karantini na wanaweza kudhibiti hali hii,'' alisema Dkt Schuchat katika mahojiano na jarida la shirika la kitabibu la Marekani.
''Tuna maambukizi mengi sana ya virusi nchini na kwa hili sasa , linavunja moyo sana.''
New Zealand ilitangaza kuwa haina maambukizi tarehe 8 mwezi Juni, na tangu wakati huo ilikuwa ikishughulika na watu wachache walioambukizwa ambao ni wasafiri waliokuwa wameingia nchini humo kutoka nje.
Korea Kusini imeajiri wataalamu wa kufuatilia watu waliochangamana na watu waliopata maambukizi , na tangu tarehe 1 mwezi Aprili nchi hiyo imerekodi maambukizi ya watu chini ya 100 kwa siku. Mlipuko nchi Singapore uliongezeka katikati ya Aprili baada ya watu wapya 1,400 kuripotiwa kupata maambukizi kwa siku moja.
Marekani imerekodi maambukizi ya watu 2,682,897 mpaka siku ya Jumanne, kwa mujibu wa Chuo cha John Hop



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?