Virusi vya corona: China yatumia dawa ya asili huku virusi vikichacha

Wakati wanasayansi wakipambana kutengeneza chanjo ya virusi vya corona, China ambayo imekuwa kinara katika utengenezaji wa dawa za asili imetengeneza dawa ya asili inayojulikana kama 'Traditional Chinese medicine (TCM)' ili kutibu ugonjwa wa corona.
Gazeti moja lilizinduliwa na serikali ya China lilidai kuwa 92% ya wagonjwa wa corona wa nchi hiyo walitibiwa na dawa hiyo.
TCM ni dawa ya kale zaidi duniani ambayo imetengenezwa kwa mitishamba.
Dawa hiyo ni maarufu sana nchini China licha ya kwamba ilizua mjadala kuhusu matumizi yake mtandaoni.
Wataalamu wanasema China inajaribu kuisambaza dawa hiyo ya TCM ndani ya nchi na nje ya nchi lakini wataalamu wa afya bado hawaamini uwezo wake wa kutibu.

Ufanisi wake kwa ujumla

Wizara ya afya ya China imeweka kitengo maalum cha TCM pamoja na muongozo wa kukabiliana na virusi vya corona, wakati televisheni ya taifa ilidai kuw adawa hiyo ilifanya kazi katika mlipuko wa miaka ya nyuma kama Sars mwaka 2003.
Kuna dawa sita ambazo zimekuwa zikitanga kutibu virusi vya corona, dawa mbili ambazo ni maarufu moja ni 'Lianhua Qingwen' - ambayo ni mchanganyiko wa dawa za mitishamba 13 kama vile forsythia na rhodiola rose - na Jinhua Qinggan - ambazo zilizinduliwa mwaka 2009 katika mplipuko wa H1N1 na ilitengenezwa na mchanganyiko wa vitu 12 vikiwemo asali, majani ya 'mint' na mizizi yam mea wa 'liquorice'.
Wanaounga mkono dawa ya TCM wanadai kuwa hakuna madhara yeyote ukitumia dawa hizo lakini wanasayansi wanasema ni muhimu kwa vipimo vya kisayansi kufanyika ili kuhakikisha usalama wa dawa hiyo.
Taasisi ya afya Marekani ilisema labda dawa hiyo itasaidia kuondoa dalili lakini suala la kutibu corona bado kuna mashaka.
"Kwa upande wake hakuna ushaidi wowote mzuri ambao unaweza kudhibitisha matumizi yake hivyo kuna hatari ambayo bado haijaweza kuelezewa," Edzard Ernst, ni mtafiti wa zamani wa Uingereza wa dawa ambazo zimeunganishwa , alinukuliwa akisema hivi karibuni kuwa ni safari ya asili.
Aidha dawa ya TCM inazidi kupata umaarufu nchini China na inaonekana kuwa kuna hitajiko kubwa la kimataifa.
Baraza la taifa la China, mwaka jana lilikadiria kuwa kiwanda cha TCM kitakuwa na thamani ya dola bilioni 420 (£337bn) ifikapo mwishoni mwa mwaka 2020.
Rais Xi alisema kuna watu wengi ambao wanapenda dawa hiyo tangu enzi za mababu China na kuiita kuwa hazina ya watu wa China.
Lakini Yanzhong Huang, mtaalamu wa afya wa wizara ya mambo ya kigeni, amebainisha kuwa usalama na ufanyaji kazi kiufasaha ndio jambo linaloangaliwa katika dawa ya TCM na watu wengi wa China bado wanaona sawa za kisasa ni bora zaidi ya dawa za miti shamba kama TCM".
Taasisi ya kitaifa ya chakula na dawa nchini China ilibaini sumu katika sampuli ya TCM.

China kuonyesha uwezo wake wa mamlaka

Licha ya kwamba China kuwa na juhudi ya kuisambaza TCM kimataifa , watu wengi nje ya China wamekuwa hawaifahamu.
Wakosoaji wanasema China kwa sasa inatumia mlipuko kuitangaza dawa hiyo nje ya nchi na kudai kuwa dawa hiyo imekataliwa katika vyombo vya habari vya taifa.
Hata hivyo China imekuwa ikisambaza dawa yake ya TCM pamoja na vifaa vyake katika mataifa ya Afrika, Asia na ulaya.
"Tuko radhi kushirikiana na wenzetu uzoefu wa China na suluhisho la China katika kutibu Covid-19,na kuwaruhusu mataifa mengine kufahamu na kuielewa dawa ya Kichina pamoja na kuitumia dawa hiyo ," Yu Yanhong, Naibu mkuu wa mamlaka ya dawa za asili nchini China alisema mwezi Machi.
Bwana Huang anaamini kuwa matangazo ya China katika dawa ya TCM kutoka nje ya nchi inawezekana inashinikizwa kwa nguvu kidogo sana.
"Jinsi serikali inavyoichukulia dawa ya TCM kuwa inatibu vizuri ugonjwa wa corona na vilevile inataka kuonyesha kuwa China inatumia mbinu thabiti katika kukabiliana na virusi vya corona, wakati ambao mataifa ya magharibi yakionekana kutumia njia ambazo hazifanyi kazi kiufasaha," alisema.
TCM ilianza kufahamika kimataifa mwaka jana baada ya shirika la afya duniani WHO, kuitambua rasmi baada ya China kuishawishi kwa miaka kadhaa - hatua ambayo ilipingwa na baraza la afya la kimataifa .
Hivyo WHO ikaingia katika utata wa kuondoa tahadhari kuhusu matumizi ya dawa za asili ili kutibu ugonjwa wa corona na kuanzia kwenye lugha ya kiingereza mpaka kichina.
Lakini ubora wa dawa hizo hakuna jaribio lolote la kisayansi ambalo limefanyika ili kuhakiki ufanisi wa dawa ya TCM.Mwezi Mei, mamlaka ya Sweden ilijaribu kutumia sampuli za Lianhua Qingwen na kubaini kuwa zina dawa ya 'menthol' pekee.
Uhusiano wa biashara ya wanyama pori
TCM pia inahusishwa na mambo kadhaa ambayo yana na ugonjwa wa corona umeongeza utata huo kwa kuhusisha na biashara ya mwanyama pori.
Tume ya afya ya China imekosoa vikali matumizi ya sindano ambayo ina unga unaotumika kutibu virusi vya corona.
Hivi karibuni China imesitisha matumizi ya kakakuona', kwa sababu ya kuhatarisha maisha ya viumbe hai ambapo magamba yake yanatumika kama dawa.
Lakini hifadhi ya wanyama pori inahofia kuongezeka kwa matumizi ya dawa ya TCM inayoweza kupelekea biashara haramu ya usafirishaji wa wanyama pori.
"Hata kama hawa wanyama ambao wako katika hatari wanaweza kutibu , kwa kutumia bidhaa nyingine ambazo zinaweza kuwa mbadala wa magamba ya kakakuona ili ziweze kutumika kutengeneza dawa ya TCM," Dkt Lixing Lao, ni profesa wa chuo kikuu cha Hong Kong, shule ya dawa za China
Kwa sasa chombo cha habari cha taifa na mamlaka imekuwa ikihamasisha TCM kuwa inaweza kuwa ndivyo sivyo.
Katika jimbo la Yunnan, iliripotiwa kuwa kuna mwanafunzi alilazimishwa kutumia dawa ya miti shamba kuwa kama kinga akiwa anarejea shuleni.
Hivi karibuni hatua ya serikali ya mji wa Beijing inayowatafuta watu wanaoibeza dawa ya TCM imepingwa vikali mtandaoni.
"Wanasayansi wanaweza kuhoji. Tiba asili ya China haiwezi kuhojiwa kwa sababu dawa ya mitishamba sio sayansi," mtumiaji mmoja alitoa maoni yake katika mtandao wa Weibo.
Dkt Lao anasema namna pekee ya kuifanya dawa ya TCM kukubalika duniani ni kwa ushahidi wa kisayansi pekee badala ya kutumia propaganda".



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?