Virusi vya corona: Covid-19 ilivyowalazimisha kuendelea na fungate isiyoisha

Ilianza na harusi iliyofanyika katika mji mkuu wa Misri -Cairo tarehe 06 Machi: Miaka minane tangu wakutane, Khaled mwenye umri wa miaka 36 na Peri mwenye umri wa miaka 35 walioana mbele ya marafiki na famiolia zao.
Siku chache baadae, wawili hao wanaoishi kwa kawaida Dubai waliondoka kuelekea CancĂșn, Mexico, wakati hakukua na hofu dunaini: virusi vya corona vilionekana kama hofu iliyokua mbali nao, kwani havikua vimesambaa duniani kote.
Wakati wawili hao walikua makini kuepuka maeneo yenye umati wa watu, wanasema "hawakutarajia kabisa" kuwa vikwazo vya kusafiri vingeathiri mipango yao.
Lakini wakati walipokua wakirejea nyumbani katika Milki za kiarabu (UAE) kupitia Uturuki tarehe 19 Machi, athari kamili zilianza kudhihirika.
"Wakati tulipokua katika ndege tulikuwa tunaweza kupata mawasiliano ya intaneti na tukaanza kupokea jumbe kutoka kwa watu wakituambia ' je mtaweza kufika ? Kuna sheria mpya, wanazuwia wageni kuingia ,'" Peri aliiambia BC.
Kwasababu walikua tayari angani, walidhani wangeruhusiwa kusafiri. Lakini walipojaribu kupanda ndege ya kuwaunganisha na safari yao ya kuelekea mjini Instanbul, waliambiwa hawawezi kuipanda.
Sheria mpya zilikua zimeanza kutekelezwa tayari walipoondoka kutoka Mexico.
Wanandoa hao waliachwa bila kujua la kufanya katika uwanja wa ndege kwa siku mbili. Masharti nchini Uturuki yalimaanisha kwamba hawaruhusiwi kuondoka au kuingia mjini kwa hiyo walibaki katika uwanja wa ndege.
Huku wakiwa hawana kibali cha kupanda ndege kinachokubalika walihangaika kununua vijaa vya usafi wa mwili wao na nguo na hata hawakuwa wanaruhusiowa hata kuchukua mizigo yao.
Kwasababu hawakuweza kuingia UAE, na kwasababu safari za ndege za kwenda Misri ziliahirishwa , walihitaji mpango wa kuwanusuru.
"Tuliamua kwenda kwenye Google na kujtafuta nchi zote ambazo zinawaruhusu Wamisri kuingia bila kinbali cha VISA, halafu kuangalia kama walikua na safari za ndege ," alisema Peri .Ilitokea kwamba walikua na chaguo moja: kwenda the Maldives.
Vikiwa ni visiwa vyenye mchanga mweupe msafi na maji safi vilivyopo katika Bahari ya Hindi Indian , the Maldives vinafahamika kama mojawapo ya maeneo mazuri ya kuvutia duniani . Khaled na Peri walikua hata wamefikiria kwenda huko kwa ajili ya fuingate badala ya Mexico.
Hata hivyo, katika wakati huu haikua matarajio yao kwenda katika fukwe na fursa ya kuogelea huku wakifanya utalii wa baharini hilo liliwafurahisha wapenzi hao sana
"Ninakumbuka wakati ule tuliporuhusiwa kupita katika uhamiaji ," Peri alikumbuka. "Tuliangaliana na tulifurahi sana kwamba angalau tutakua tunalala kitandani na wala si kwenye viti vya uwanja wa ndege!"
Khaled, ambaye ni mhandisi wa mawasiliano ya simu, alisema, akicheka: "Tulifurahi sana kuona mizigo yetu."
Lakini mara moja mkanganyiko wa kupata mahali pa kukaa ulipotatuliwa, changamoto nyingine ikawakumba.
"Tulianza kubaini kuwa tulikuwa na tatizo kubwa la kifedha, kazi zetu- hatungeweza kuzifanya vizuri. Hatukua tumekuja na kompyuta zetu ," alisema Peri, anayefanya kazi katika chombo cha habari . "Unapokua katika fungate hutarajii kufanya kazi sana ."
Walipofika katika hoteli yao katika kisiwa hicho waligundua kuwa walikua miongoni mwa wageni wachache sana, wengi wao walikua wanasubiri ndege za kuwarudisha kwao.
Wakati wengine wakiondoka, hoteli ikafungwa, na wawili hao wakahamishiwa kwenye kisiwa kingine, ambako walipata uzoefu huo huo.
Waliiishi mwezi uliopita katika eneo maalumu la karantini lililotengwa na serikali ya the Maldivian -hoteli iliyopo kwenye kisiwa resort on the island of Olhuveli.
Wanawashukuru maafisa, ambao wanawatoza viwango vya chini vya garama, na wahudumu wa hoteli.
"Wanafanya kila wawezavyo kusema kweli kuhakikisha wanayafanya haya maisha hapa kuwa mazuri kwetu. Kwa hiyo, jioni, wanacheza muziki, wana DJ kila siku, na wakati mwingine hata tunahisi vibaya sana kwasababu hakuna mtu anayedensi ," anasema Khaled.
Kuna hoteli nyingine takriban 70 za ufukweni, nyingi kati yake zikiwa ni za watu walioko katika fungate pia. Tofauti pekee kulingana na Peri, ni kwamba wengine "walichagua the Maldives kama eneo lao la fungate -sisi hatukuichagua ".
Kuna karibu watalii 300 waliobaki katika the Maldives, ambayo kwa sasa imezuwia wageni wapya kuwasili. Lakini huku kukiwa na maeneo mengine mabaya zaidi ya kuishi wakati wa amri ya kutotoka nje, wawili hao wanahamu sana ya kurudi Dubai.
Wanasema wameweza tu kutembelea "mata kadhaa", kwa upande mmoja kwasababu mvua kubwa imekua ikiendelea kunyesha wakati wa kipindi cha msimu wa mvua, na pia kwasababu walikua wamefunga wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Wote sasa wamerejea kazini, lakini wanahangaika kujumuika katika mikutano kwa njia wi-fi ili kushiriki mikujtano ya video.
Lakini kufika nyumbani ni jambo rahisi. Kama wakazi wa UAE, ambao sio raia, wanasema hawakuruhusiwa kuingia katika ndege iliyowarejesha wengine katika Ghuba.
Na wakati wanasafiri kwa ndege kuelekea Misri katika ndege ya kuwarudisha nyumbani lingekua ni chaguo lao, ugumu unakuja kwamba itamaanisha wakae karantini kwa muda wa siku 14 katika makazi ya serikali-na bado wasiweze kurejea nyumbani kwao Dubai.
Wanawatolea wito maafisa wa UAE kuwasaidia na wakazi wengine waliokwama. Wametuma maombi ya kuruhusiwa kusafiri kwa serikali kwa njia ya mtandao, lakini bado hawajapewa ruhusa.
Na kwa vyovyote vile, hakumna safari ya ndege iliyopo kwa sasa.
"Inakanganya zaidi kila mara tunaposoma katika magazeti kwamba ndege zinaahirisha tarehe za kuanza upya shughuli zake … Tutafanya vyovyote tunavyoambiwa inapokuja katika suala la karantini iwe katika hoteli au kujitenga wenyewe katika nyumba zetu ," Peri alisema.
Inapokuja katika suala la kuongezeka kwa gharama za safari , wawili hao wameamua ''kutofanya mahesabu yeyote hadi tutakaporudi nyumbani, kwasababu hatujui itamalizika lini ".
Bado wanajua kwamba watu wengine duniani wamo katika hali ngumu zaidi. Lakini wanasisitiza safari yao imekua zaidi ya fungate.
" Inasikitisha kila mara unapokua katika hoteli na unakua ni mgeni wa mwisho pale, na wahudumu wote wanakupa mkono wa kwa heri . Pia unahisi vijbaya kwa ajili yao … Hilo lilitotokea kwetu mara ," anasema Khaled. "Maeneo kama haya yanapaswa kuwa yamejaa watu na nyakati nzuri, hivyo sivyo ilivyo sasa ."
" Kila mara tunapowaambia watu tumekwama katika visiwa vya Maldives, wanacheka na ni kama sio hali mbaya. Natamani ningekua katika hali yako '," Peri aliongeza. "Sio rahisi au raha, kusema kweli inachosha…kufurahi kuwa nyumbani na familia. Ningechagua hilo zaidi ya kitu kingine chochote kile.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?