Illuminati ilianzaje? na ni kwanini kuna mvuto kuhusu wafuasi wake?

Je Jay Z ni mfuasi wa Ilimunati? Donald Tump, Katty Perry na hata Beyonce wameshutumiwa kuwa wafuasi wa Illumanti. Kundi la siri linalo arifiwa kuwajumuisha watu wenye nguvu na udhibiti duniani.
Hata kama hujawahi kusikia kuhusu illuminati , kuna uwezekano kwamba umeshawahi kuona ishara zinazohusishwa nazo.
Mbuzi, jicho linaloona kila kitu - 'the all seeing eye' linaloonekana kwenye noti za Marekani.
Katika kanda za video za muziki, baadhi ya mistari iliyokatwa pia huhusishwa na hilo kama kibao cha Rihana S&M kilichoonyesha kichwa bandia cha habari kinachomtaja yeye kuwa mwanamfalme wa illuminati.
Basi kwanini wanamuziki na wasanii wanapenda kufanya mzaha kuhusisha illuminati?
Mwandishi habari na muandishi vitabu, David Bramwell anasema kwa ufupi ni kujifurahisha.
Wengi wanavutiwa na hadithi hizo kama baadhi yetu tunavyovutiwa.
'Nakumbuka uvumi uliosambazwa mnamo 1966 kwamba Paul McCartney wa kundi la the Beatles alifariki katika ajali ya gari alipokuwa akielekea nyumbani baada ya kurekodi muziki.
Na kwamba alibadilishwa na DJ mmoja wa Canada ambaye alifanana mno na yeye ambaye alijifunza kwa haraka, kuimba na kupiga gita kama yeye'.
Bramwell anaeleza kwamba McCartney mwenyewe hajawahi kukana fikra hiyo. Na kama ilivyo kwa Mccartney na Jay Z na Rihanna, wengineo pia wanafurahishwa na taarifa hiyo.

Iluminati ni nani?

Ni kweli kwamba Illuminati ni vivuli vya watu wanaoidhibiti dunia?
Illuminati kwa ufahamu uliopo, walikuwa ni jamii yenye usiri kutoka Bavaria iliyoundwa katika karne ya 18.
Jamii hiyo ilipinga mazingaombwe, ushawishi wa kidini na uongozi wa taifa.
Waliunda kitabu cha sheria kilichosema kuwa lengo kuu ni kusitisha matumizi ya mashine ya wanaodhulumu watu, na kuwadhibiti bila ya kuwatawala.
Punde si punde jamii hiyo ya Bavaria ikaishia kutokuwa na maana.
Na halihusiki kwa namna yoyote na fikra zilizopo leo kuhusu Illuminati.
Fikra inayofahamika leo inatokana na vuguvugu la Discordian - wanaomini kwamba vurugu ni muhimu kama utulivu.
Inaelezwa kwamba vuguvugu hilo lilianzishwa mnamo 1965 katika ofisi ya wakili mmoja jimboni texas Marekani.
Wanafunzi wawili waliosoma shule moja, Greg Hill na Kerry Thornley walitumia mashine ya kutoa kopi kuchapisha nakala za waraka ulioidhinisha vuguvugu hilo.
Waraka huo uliendekeza fikra kwamba 'vurugu au ghasia ni muhimu kama ilivyo kwa utulivu'.
Na vuguvugu hilo lilishika kasi katika miaka ya 60 na 70 huku wanafunzi hao wawili wakizidi kusambaza utundu na taarifa za uongo.
Lengo lao lilisambazwa zaidi na raia wawili wengine wa Marekani.
Mwandishi Robert Anton Wilson aliyeliandikia jarida la PlayBoy na rafiki yake Robert Shea.
Wawili hao Bramwell anaeleza waliamua kuandika riwaya inayojumuisha fikra zote hizo na kukiita kitabu Illuminatis.
Walihisi kwamba itakuwa ni jambo la kufurahisha kujaribu kusambaza vurugu na taarifa za uongo kwa makusudi kuhusu illuminati na walifanikiwa kwa kuandika barua kwa vyombo vya habari, lakini pia kupitia sehemu ya barua ndani ya jarida hilo la Playboy.
Waliandika barua za urongo kutoka kwa wasomaji wasiokuwepo, waliosema kwamba illuminati sio wa kweli au wengine walioonekana kutokuwa na msimamo kamili kuhusu suala hilo.
Kilichokuwa na uzito ni kwamba watu wote hao waliokuwa wamezusha gumzo kuhusu illuminati na fikra ilikuwa ni kwa lengo kwamba msomaji atauliza maswali, kulihoji suala hilo na kuuliza iwapo 'ni kweli kuna illuminati?'
Dhana hiyo ilisambaa pakubwa, na kitabu hicho kilizusha maswali kama kwa mfano 'ni nani aliyempiga risasi John F. Kennedy?'
Licha ya kwamba ukubwa wa fikra hizo zinazojitokeza katika kitabu hicho ni za uongo, zimechanganyika na ukweli wa kiasi fulani kuzifanya kukubalika.
Kitabu hicho kilipata umaarufu kiasi cha kugeuzwa mchezo wa kuigiza wa muda wa saa nane ulioigizwa katika jukwaa Liverpool.
Jarida hilo la miaka ya 70 la utamaduni kwa sasa halipatikani katika kizazi cha intaneti, lakini uvumi kuhusu illuminati bado unaendelea katika mitandao kadhaa ambapo watu wanaomaini hubadilishana mawazo, fikra na ushahidi wa uwepo wa illuminati.
Mwisho wa siku uamuzi ni wako wewe kuamini iwapo kuna illuminati au la.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?