Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 30.11.2019: Rodgers, Arteta, Vieira, Sancho, Willian, Richarlison
Arsenal wako tayari kuona kama wataweza kumshawishi Brendan Rodgers wa Leicester miongoni mwa watu waliowaorodhesha kuchukua nafasi ya Unai Emery.(Mirror) Leicester itahitaji fidia ya pauni milioni 14 kama klabu yoyote ya ligi kuu itajaribu kumchukua Rodgers. (Telegraph) Washika bunduki hao waliwasiliana na kocha wa zamani wa Valencia Marecelino ili awe meneja wao mpya ( Sun) Mauricio Pochettino, Nuno Espirito Santo, Massimiliano Allegri na Carlo Ancelotti wote ni miongoni wa wanaotamaniwa kujaza nafasi hiyo katika uwanja wa Emirate. (Telegraph) Wamiliki wa Wolves wanajiandaa kupambana kumbakisha Nuno, ambaye mkataba wake utakwisha mwishoni mwa msimu ujao. (Mail) Arsenal tena itapendekeza mchezaji wa zamani Mikel Arteta kujaza nafasi iliyoachwa na Emery. (Independent) Uamuzi wa kumtimua Emary ulifikiwa katika mkutano uluifanyika nchini Marekani siku ya Jumatatu.(Mirror) Aliyekuwa kipenzi cha Arsenal Patrick Vieira amefuilia mbali mpango wa kuondoka Nice- ingawa amekuwa akihusishwa na t...