Yanga yaichapa Malumo 2-0, yajihakikishia kuvuka hatua ya nusu Fainali.


Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga imeichapa Marumo Gallants ya Afrika Kusini mabao 2-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, uliofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mechi hiyo ilianza kwa kasi, huku pande zote mbili zikijaribu kupata mabao ya haraka, ingawa ulikuwa wa kupoa na kupata kasi tena.

Ulikuwa mchezo wa wazi, kila timu ikitengeneza nafasi za wazi kadhaa lakini ni Yanga ndiyo iliyoweza kunufaika zaidi kwa nafasi mbili. 

Mzunguko wa pili utahitimisha kujua kama Yanga itafuzu kwa mara ya kwanza fainali ya michuano hiyo mwaka huu.

Mechi ya marejeano itapigwa Royal Bafokeng Stadium Rustenburg Mei 17 nchini Afrika Kusini.

  • DRC

    Watoto wawili wameokolewa wakielea karibu na ufukwe wa ziwa Kivu siku chache baada ya mafuriko kuua zaidi ya watu 400 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    "Ni muujiza, sote tulishangaa," kiongozi wa jumuiya ya eneo hilo Delphin Birimbi aliambia BBC. Wazazi wao wamefariki lakini jamii inawasiliana na watu wanaoweza kuwalea, Bw Birimbi anaongeza.

    Haijabainika jinsi watoto hao wachanga walinusurika kwa karibu siku tatu katika ziwa hilo, lakini mashuhuda wanasema waliwaona wakielea kwenye vifusi.

    Watoto hao waliokolewa Jumatatu - mmoja huko Bushushu na mwingine Nyamukubi, vijiji viwili vilivyoathiriwa zaidi na mafuriko yaliyotokea wiki jana, Bw Birimbi anasema. 

    Mkasa huo umesababisha hisia za kuhuzunisha katika vijiji hivyo vyenye mrundikano wa maiti zilizofunikwa kwa blanketi.

  • Bunge

    Wabunge wa Tanzania wameonywa kutovua nguo zozote wanapokuwa bungeni.

    Spika Tulia Ackson alitoa onyo hilo baada ya Mbunge Mwita Waitara kuvua koti na tai wakati wa mjadala.

    Alikuwa akionyesha kutoridhishwa na na majibu ya serikali - kuhusu fidia kwa wapiga kura wake walioko kwenye maeneo ya uchimbaji madini.

    Alivua mavazi hayo huku akitoka nje ya ukumbi.

    Kwa mujibu wa Spika, hakukerwa na namna ya kuondoka kwake, bali alikiuka kanuni za mavazi ya ubunge, ambayo yanahitaji uvaaji rasmi ndani ya ukumbi wa Bunge.

    Alielezea kitendo chake ni kilikuwa ni "utovu wa nidhamu".

    "Tabia hii hairuhusiwi ndani ya bunge na isijirudie tena," alisema Bi Ackson.

  • .

    Mvulana wa miaka minane aliyepotea katika misitu ya mbali ya Michigan alinusurika kwa siku mbili kwa kula theluji na kujificha chini ya magogo.

    Nante Niemi alitoweka siku ya Jumamosi alipokuwa akipiga kambi na familia yake katika mbuga ya serikali ya Milima ya Porcupine.

    Alipotea wakati akitembea kutafuta kuni, na hivyo kuzua jitihada za watu 150 kumtafuta ili kumwokoa.

    Siku ya Jumatatu alipatikana chini ya gogo moja "akiwa na afya njema", kama maili mbili kutoka kambi yake.

    "Alikuwa amevumilia hali ngumu kwa kujikinga chini ya gogo ambapo hatimaye alipatikana," Polisi wa Jimbo la Michigan walisema katika taarifa.

    Mvulana huyo aliwaambia polisi kwamba "alikula theluji safi kwa ajili ya maji".

    Mara tu baada ya habari kuenea kuhusu kutoweka kwake Jumamosi, mama yake aliwashukuru watu kwa usaidizi wao lakini akawasihi kila mtu "tafadhali kaa mbali itafanya iwe vigumu kumpata".

    Polisi wa serikali walisema eneo hilo "liko mbali sana na lenye vilima na maji mengi ya kusimama kutokana na wakati wa mwaka". Barabara nyingi hazipitiki kutokana na wingi wa theluji.

    Timu hiyo ililenga eneo la takriban maili 40 za mraba (km 100 za mraba) katika bustani hiyo, na hatimaye kumpata mvulana huyo.

    Amekutanishwa tena na familia yake, polisi walisema.

  • .
    Image caption: Alfie Halaanda ni babake mshambuliaji wa Manchester City Erling Braut Halaand

    Alfie Haaland anasema alisindikizwa kutoka kiti chake Bernabeu kwa sababu mashabiki wa Real Madrid "hawakufurahishwa" na sherehe zake baada ya Kevin de Bruyne kuisawazishia Manchester City katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa.

    Video kwenye mitandao ya kijamii inaonekana kumuonyesha babake Erling Haaland akiwakejeli mashabiki wa nyumbani kabla ya kuondolewa katika eneo lake.

    Haaland alitweet: "Sawa. RM hakufurahi tulikuwa tukisherehekea bao la KDB.

    "Zaidi ya hayo tulilazimika kuhama kwa sababu mashabiki wa RM hawakufurahishwa na 1-1."

    De Bruyne alifunga dakika ya 67 na kusawazisha bao la kuongoza la Vinicius Junior.

    Haaland alipunga mkono kwa mikono miwili huku akitabasamu kwa umati wa watu waliokuwa chini yake, akitega masikio yake kwa mashabiki wa Real Madrid na kufanya ishara, huku ripoti nchini Uhispania zikipendekeza kuwa aliwarushia chakula wafuasi hao.

    Kiungo huyo wa zamani wa Manchester City na Leeds ni mtu wa kawaida kwenye mechi za City, ambapo mwanawe amefunga mabao 51 hadi sasa msimu huu.

    Miamba wa Uhispania Madrid wametwaa taji la Ligi ya Mabingwa - mashindano ambayo City bado hawajashinda - mara tano tangu 2014 na kuwaondoa mabingwa hao wa Ligi ya Premia katika hatua ya nusu fainali mwaka jana.

    Mnamo Oktoba ripoti zilipendekeza kwamba kandarasi ya Haaland ina kipengele maalum cha kuachiliwa kwake ili ajiunge na Real Madrid mnamo 2024, ambayo bosi wa City Pep Guardiola alisema baadaye "sio kweli".

  • .Kiongozi wa kanisa la kufunga hadi kufa paul Mackenzie
    Image caption: .Kiongozi wa kanisa la kufunga hadi kufa paul Mackenzie

    Kiongozi wa madhehebu ya Shakahola Paul Mackenzie atasalia rumande kwa siku 30 zaidi, mahakama ya Mombasa iliamua Jumatano.

    Hakimu Mkuu wa Shanzu Yusuf Shikanda alichukua uamuzi wa kuwazuilia Mackenzie, mkewe Rhoda Maweu na washukiwa wengine 16 akitaja uchunguzi unaoendelea.

    Bw Shikanda zaidi alisema usalama na usalama wa washukiwa huenda ukawa hatarini iwapo wataachiliwa kwa dhamana katika hatua hii.

    Kiongozi huyo wa madhehebu ya Kilifi anaaminika kuwahadaa makumi ya wafuasi wake hadi kufa kwa njaa.

  • .
    Image caption: Mfumo wa kulinda anga wa patriot

    Katika mkutano na Jeshi la Wanahewa Brigedia Jenerali Pat Ryder, msemaji wa Idara ya Ulinzi ya Marekani, alithibitisha kwamba kombora la Kirusi la Kinzhal la hypersonic lilidunguliwa juu ya anga yam ji wa Kiev mnamo Mei 4 kwa kutumia mfumo wa Patriot uliopatikana hivi karibuni na jeshi la Ukraine.

    Kombora la Kinzahl lililodaiwa kutowezekana na Urusi lilizinduliwa wiki iliyopita katika shambulio kubwa la kombora la Urusi.

    Hapo awali, mifumo ya Patriot ilitumiwa dhidi ya makombora ya kawaida ya balestiki, na uwezo wa kurusha makombora ya hypersonic ulikuwa wa kinadharia tu.

    Ijapokuwa wanajeshi wa Ukraine walipata mabaki ya kombora hilo, mamlaka zilichelewa kutoa maelezo hadi iliporipotiwa mahali pengine, kwani inaaminika kuwa kombora hilo haliwezi kuharibika.

    Baada ya hapo, habari hiyo ilithibitishwa na kamanda wa Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine, Luteni Jenerali Nikolai Oleshchuk.

    "Ndio, tulipiga risasi" isiyo na kifani "Kinzhal"! Hii ilitokea wakati wa shambulio la usiku Mei 4 katika anga ya mkoa wa Kiev. Kombora la X-47 lilirushwa na MiG-31K kutoka eneo la Urusi," aliandika.

    Taarifa hii ya Jumanne iliungwa mkono na uthibitisho rasmi kutoka Pentagon.

  • Rais Felix Tshisekedi alisema wanajeshi hao wanaweza kuondoka mwishoni mwa Juni
    Image caption: Rais Felix Tshisekedi alisema wanajeshi hao wanaweza kuondoka mwishoni mwa Juni

    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amesema Jeshi la Kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF) litaondolewa mashariki mwa nchi hiyo iwapo litashindwa kutekeleza majukumu yake ya kuleta amani ifikapo Juni.

    "Tutaamua kutoa kikosi hiki ... na kuwashukuru," alisema Jumanne nchini Botswana, ambako yuko katika ziara ya serikali.

    EACRF ilipelekwa katika eneo hilo mwezi Machi ili kusaidia kukabiliana uasi wa Waasi M23 lakini tangu wakati huo imekosolewa kwa kushindwa kuwaondoa waasi katika eneo hilo.

    Rais Tshisekedi pia alionyesha kuchoshwa na jeshi la kikanda, ambalo alisema halifanyi kazi kama ilivyotarajiwa DR Congo na inadaiwa kuwa lilikuwa likishirikiana na waasi.

    "Katika baadhi ya mikoa, jeshi la kikanda linaishi pamoja na magaidi wa M23.

    Hii haikuwa sehemu ya mpango huo. "Makubaliano yalikuwa kuondoa vikosi vya M23 na kusitisha mapigano" aliongeza.

    Kauli yake ilikuja siku moja baada ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) kukubali kupeleka wanajeshi mashariki mwa DR Congo.

    Kiongozi huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pia alikosoa mamlaka ya Kenya kwa kujiuzulu na kuchukua nafasi ya kamanda wa kikosi cha kwanza, Jenerali Jeff Nyagah, kutokana na "vitisho" ambavyo havijabainishwa.

    Ramani
  • Wanataka kuendelea kumzuilia Paul Nthenge Mackenzie
    Image caption: Polisi wanataka kuendelea kumzuilia Paul Nthenge Mackenzie.

    Kiongozi wa dhehebu tata la kidini linalohusishwa na tuhuma ya mauaji ya waumini wake nchini Kenya leo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa mara nyingine tena.

    Huku hayo yakijiri polisi wanandelea kuchunguza vifo vya zaidi ya wafuasi 130 wa dhehebu hilo la kidini lenye utata.

    Wanataka kuendelea kumzuilia Paul Nthenge Mackenzie, anayedaiwa kuamuru wafuasi wake kufunga hadi kufa ili wafike mbinguni haraka zaidi.

    Uchimbaji wa makaburi ya pamoja katika msitu wa Shakahola huko Kilifi pwani ya Kenya unaendelea - miili mingine 21 ilifukuliwa Jumanne. 

    Mamia watu hawajulikani walipo.

    Pia unaweza kusoma:

  • Buhari

    Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameongeza muda wa kukaa London kwa wiki moja kwa matibabu ya meno, msaidizi wake amesema.

    Awali rais huyo alikuwa amesafiri kwenda Uingereza wiki iliyopita kuhudhuria kutawazwa kwa Mfalme Charles III.

    Alipangiwa kurejea Nigeria wiki hii lakini sasa atasalia "kwa amri ya daktari wake wa meno, ambaye ameanza kumhudumia".

    "Mtaalamu anahitaji kuonana na rais katika siku nyingine tano kwa ajili ya utaratibu ambao tayari umeanza," msemaji wa rais Femi Adesina alisema katika taarifa iliyotolewa Jumanne usiku.

    Kukaa kwa muda mrefu kwa rais huyo mjini London kumezua shutuma kutoka kwa baadhi ya Wanigeria, wanaosema kwamba anapaswa kuyapa kipaumbele masuala ya ndani na kushughulikia changamoto za usalama zinazoikabili nchi hiyo.

    Bw Buhari amesafiri hadi Uingereza mara kadhaa katika kipindi chake cha urais kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi huku kukiwa na uvumi kuhusu afya yake. Ameratibiwa kumkabidhi Rais Mteule Bola Tinubu tarehe 29 Mei.

  • Erdogan

    Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameangaza nyongeza ya asilimia 45 ya mshahara kwa wafanyikazi wa umma 700,000 siku tano kabla ya uchaguzi mkuu.

    Haya yanajiri wakati uchumi wa nchi hiyo ukiyumba kutokana na athari za matetemeko makubwa ya ardhi mwezi Februari.

    Erdogan, ambaye alichaguliwa kuwa rais wa Uturuki mwaka 2014, atawania muhula mwingine katika uchaguzi wa rais na wabunge mnamo Mei 14.

    Kura za maoni zinaonyesha Erdogan anakabiliwa na kinyang'anyiro kikali kutoka mgombea urais wa upinzani, Kemal Kilicdaroglu.

    Uchumi wa Uturuki ni suala muhimu kuelekea uchaguzi wa Jumapili. 

    Hatua ya Erdogan ya kupunguza kwa viwango vya riba kusiko kwa kawaida kulisababisha kushuka kwa thamani ya lira ya Uturuki mwishoni mwa 2021 na kufanya mfumuko wa bei kufikia asilimia 85.5 mwaka jana, kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa ndani ya miaka 24.

  • Eliud Wekesa amewaongoza waumini wa kanisa lake kuamini kuwa yeye ni Yesu

    Mhubiri mwenye utata nchini Kenya ametakiwa kufika polisi kwa mahojiano huku serikali ikikabiliana na kile inachokiita makanisa yenye utata na viongozi wa kidini wenye msimamo mkali.

    Eliud Wekesa, almaarufu "Yesu wa Tongaren", kiongozi wa dhehebu la New Jerusalem, aliitwa siku ya Jumanne ili kuhojiwa kuhusu mafundisho yake ya kidini yanayotiliwa shaka.

    Amewaongoza waumini wa kanisa lake kuamini kuwa yeye ni Yesu.

    Anatarajiwa kufika mbele ya polisi katika kaunti ya magharibi ya Bungoma siku ya Jumatano.

    Mhubiri huyo, hata hivyo, anasema hajafanya chochote kibaya kutakachomfanya akamatwe, akiongeza kuwa anaeneza injili pekee, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

    Haya yanajiri huku wachunguzi wakifukua miili 21 zaidi katika kaunti ya Kilifi pwani, ya Kenya na kufanya jumla ya waliofariki katika mauaji ya Shakahola kufikia 133. 

    Mchungaji Paul Mackenzie, kiongozi wa Kanisa la Good News International lenye makao yake makuu mjini Kilifi, anasubiri kufikishwa mahakamani, kwa tuhuma za kuwasihi wafuasi wake kufunga hadi kufa ili ''waende mbinguni''.

    Mamia ya wengine wameripotiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.

    Rais William Ruto ameunda tume ya uchunguzi kuchunguza vifo vya Shakahola katika kaunti ya Kilifi.

    Polisi katika jimbo jirani la Kwale siku ya Jumatatu waliwaokoa watu 200 wakiwemo watoto 50 kutoka msituni katika kisa kinachoshukiwa cha utekaji nyara wa kidini.

    Maelezo zaidi:

    Yesu wa Tongareni ni nani?

  • Cheng

    "Siku elfu moja ni muda mrefu sana kizuizini," anasema Nick Coyle.

    Anazungumzia kilichokuta mpenzi wake, mwandishi wa habari wa Australia Cheng Lei, ambaye bado anazuiliwa katika gereza la China.

    Maelezo kuhusu mashtaka dhidi yake bado yamewekwa siri na hajahukumiwa.

    Kama marafiki na familia nyingine za Bi Cheng, Bw Coyle anasema hailewi kwa nini Cheng anapitia madhila kama haya.

    "Nitoa wito kwa mamlaka husika nchini China kutatua hali hii mbaya haraka iwezekanavyo," anaiambia BBC.

    Cheng Lei alikuwa akifanya kazi kama mwandishi wa taarifa za biashara katika kituo cha televisheni cha taifa cha China cha CGTN alipokamatwa ghafla na maafisa wa usalama wa serikali tarehe 13 Agosti 2020, na baadaye kushutumiwa kwa "kutoa siri za serikali nje ya nchi kinyume cha sheria".

    Miezi yake sita ya kwanza alizuiliwa katika kifungo cha upweke, akidhibitiwa vikali ingawa alihojiwa bila kuwa na wakili.

    Tangu wakati huo, amekuwa akizuiliwa pamoja na wafungwa wengine.

    Kesi yake ilifanyika faraghani mwezi Machi mwaka jana.

    Balozi wa Australia nchini China Graham Fletcher alinyimwa kuingia mahakamani.

    Lakini hukumu yake imeahirishwa mara kwa mara.

    Juhudi za BBC kuwasiliana na maafisa wa kwa Mahakama ya Beijing, ambako kesi yake ilifanyika, hazikufaulu.

    Bw Coyle - mtendaji mkuu wa zamani wa Chama cha Wafanyabiashara wa China-Australia - sasa ameondoka Beijing lakini anaendelea kufuatilia suala hilo kutoka ng'ambo wa ajili ya kuachiwa kwake.

    Wizara ya mambo ya nje ya China imejaribu kupunguza wasiwasi wa kimataifa kuhusu kesi hiyo.

  • Mwandishi wa habari wa Ufaransa aliyeuawa akitabasamu na paka begani
    Image caption: Mwandishi wa habari wa Ufaransa aliyeuawa akitabasamu na paka begani

    Mwandishi wa habari wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 32 ameuawa alipokuwa akiripoti kutoka eneo la vita mashariki mwa Ukraine.

    Arman Soldin, ambaye alifanya kazi katika shirika la habari la AFP, alifariki Jumanne baada ya kupigwa na roketi karibu na Chasiv Yar, magharibi mwa Bakhmut.

    Timu ya waandishi wa habari ilishambuliwa mwendo wa saa 16:30 (13:30 GMT) wakiwa na kundi la wanajeshi wa Ukraine.

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitoa pongezi kwa kazi ya Soldin kwenye mstari wa mbele wa vita.

    "Tunaungana na wapendwa wake na wenzake," aliandika kwenye ujumbe wa Twitter.

    Mwenyekiti wa AFP, Fabrice Fries, alisema shirika la habari "limehuzunishwa" na kifo cha Soldin, ambacho alisema "ni ukumbusho mbaya wa hali hatari wanazokabiliana nazo waandishi wa habari kila siku wanapoangazia mzozo wa Ukraine".

    Mkurugenzi wa shirika hilo la Ulaya, Christine Buhagiar, alimkumbuka Soldin kama "mwenye shauku, mwenye nguvu na jasiri", na kuongeza kuwa "amejitolea kabisa kwa uwelediwake".

    Wabunge walisimama katika Bunge la Kitaifa la Ufaransa na kutoa heshima kwa Soldin.

    Unaweza pia kusoma

    Ukraine yatangaza kuliangusha kombora la Urusi 'lisilowezekana'

    Vita vya Ukraine: Urusi yazindua shambulio 'kubwa zaidi' la ndege isiyo na rubani ya Kamikaze

  • Carroll

    Jopo la majaji katika kesi ya madai limempata Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump n ahatia ya kumnyanyasa kingono mwandishi wa jarida katika duka moja kuu la New York miaka ya 1990.

    Ni mara ya kwanza kwa Bw Trump kupatikana na hatia ya kuhusika na unyanyasaji wa kingono.

    Lakini Bw Trump hakupatikana na hatia ya kumbaka E Jean Carroll katika chumba cha kubadilishia nguo cha Bergdorf Goodman.

    Mahakama pia ilimpata Bw Trump na hatia ya kuharibia jina kwa kuyaita madai ya mwandishi huyo "Uvumi na uwongo".

    Mahakama ya Manhattan iliamuru Bw Trump amlipe takriban dola milioni milioni tano kama fidia.

    Jopo hilo la majaji tisa ilifikia uamuzi wao baada mashaurinao ya chini ya saa tatu siku ya Jumanne.

    "Leo, ulimwengu hatimaye unajua ukweli," Bi Carroll alisema katika taarifa iliyoandikwa kufuatia uamuzi huo.

    "Ushindi huu sio kwangu tu bali kwa kila mwanamke ambaye ameteseka kwa sababu hakuaminiwa."

    Wakili wa Bw Trump alisema rais huyo wa zamani anapanga kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

    Maelezo zaidi:

  • Maoni

    Machapisho maarufu kutoka blogu hii

    Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

    Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?