Makubaliano ya kusitisha vita Sudan yadumishwa licha ya ukiukaji wa mkataba


Makubaliano ya hivi punde ya kusitisha vita nchini Sudan sasa unaonekana kudumishwa licha ya ukiukaji wa mapema wa makubaliano hayo.

Ni mapatano ya kwanza kuafikiwa rasmi na kutiwa saini na pande zote mbili, lakini kulikuwa na ripoti za mashambulizi ya anga na mapigano katika mji mkuu Khartoum yalipoanza kutekelezwa Jumatatu jioni.

Katika miji ya Omdurman na Bahri inayopakana na mji mkuu, watu walisema wamesikia milio ya risasi.

Usitishaji huo wa mapigano utawezesha utoaji wa misaada ya kibinadamu inayohitajika sana.

Saa chache kabla ya mapatano ya hivi punde kuanza, mkuu wa wanamgambo wa RSF, Jenerali Hamdan Dagalo, alitoa taarifa ya kivita akiwataka wanajeshi wake kulishinda jeshi la taifa na kushinda vita hivyo.

Unaweza pia kusoma:

  • f

    Afisa wa wa ujasusi alisema hakuna mtu aliyejeruhiwa - baadaye akaongeza kuwa lori hilo lilichukuliwa kuwa salama, na kwamba uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa ajali hiyo inaweza kuwa ya makusudi.

    Baadhi ya barabara za mitaa na maeneo ya watembea kwa miguu yalifungwa, alisema mapema.

    Dereva wa lori la kuondoa U-Haul hakutambuliwa mara moja.

    WUSA - kituo cha televisheni washirika na CBS kinachoangazia taarifa hiyo mjini Washington DC - kilimnukuu shahidi akisema kuwa dereva aligonga vizuizi kwa mara ya pili kufuatia mgongano wa awali.

    Tukio hilo - lililotokea kabla ya saa nane usiku kwa saa za Marekani - lilisababisha kuhamishwa kwa wateja wa hoteli zilizo karibu ikiwa ni pamoja na Hay Adams.

  • Video content

    Video caption: Siku ya Fistula Duniani: Jitihada maalum zanahitajika kuwapa tiba waliothirika

    Leo ulimwengu inaadhimisha siku ya fistula huku tatizo hilo likionekana bado kuwepo katika nchi mbali mbali ikiwemo Tanzania.

    Kila mwaka takriban wagonjwa 3,000 wanaripotiwa kuwa na tatizo hilo katika maeneo mbalimbali hasa vijijini.

    Mwandishi wetu Aboubakar Famau ametembelea katika moja ya hospitali maalumu inayotoa matibabu kwa wagonjwa wa fistula.

  • Makampuni ya maduka ya dawa ya India yamekuwa chini ya uangalizi mkubwa juu ya ubora
    Image caption: Makampuni ya maduka ya dawa ya India yamekuwa chini ya uangalizi mkubwa kuhusiana an suala la ubora

    Serikali ya India imewaamuru watengenezaji wa dawa za kikohozi kupima sampuli kabla ya kuuza bidhaa zao nje ya nchi.

    Kuanzia tarehe 1 Juni, kampuni hizo zitalazimika kupata cheti cha uchambuzi kutoka kwa maabara iliyoidhinishwa na serikali.

    Mabadiliko haya ya sheria yanakuja baada ya baadhi ya dawa za kikohozi zilizotengenezwa India kuhusishwa na vifo nchini Gambia na Uzbekistan.

  • Maoni

    Machapisho maarufu kutoka blogu hii

    Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

    Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?