Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 25.05.2023

Victor Osimhen alijiunga na Napoli kutoka klabu ya Ufaransa ya Lille mnamo Julai 2020

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

Victor Osimhen alijiunga na Napoli kutoka klabu ya Ufaransa ya Lille mnamo Julai 2020

Manchester United hawana budi kulipa pauni milioni 140 kama wanataka kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, msimu huu baada ya kuafikiana dili la mchezaji-mwenza na mlinzi wa Korea Kusini Kim Min-jae, 26. (Il Mattino) via Mirror)

Napoli wanajaribu sana kumshawishi Kim kusaini mkataba mpya kabla ya kifungu cha kuachiliwa kuanza kutumika msimu huu wa joto. (90 Min)

Mikel Arteta yuko tayari kumruhusu kiungo wa kati wa Uingereza Emile Smith Rowe, 22, kuondoka Emirates ili kutoa nafasi kwa kiungo wa Leicester na England James Maddison, 26. (Mirror)

Rowe

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

The Gunners pia wana nia ya kumuongeza mshambuliaji wa Torino na Paraguay Antonio Sanabria, 26, kwa mkataba wa thamani ya £21.6m. (La Repubblica via Mail)

Mshambulzi wa Tottenham na England Harry Kane, 29, bado anasalia kuwa chaguo la kwanza la Manchester United na klabu hiyo inapania kuanza mapema kufanya mazungumzo na Spurs. (Guardian)

Real Betis huenda ikafufua nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa Leeds United Mhispania Marc Roca, 26, ikiwa klabu hiyo ya Yorkshire itashushwa daraja kutoka Ligi ya Premia. (Estadio Deportivo)

Harry Kane

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

Harry Kane

Arsenal wamempa kiungo wa Uingereza Reiss Nelson mkataba mpya hadi 2027, inayojumuisha chaguo la nyongeza ya mwaka, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 pia amepokea ofa kutoka kwa timu zingine za Ligi ya Premia, Italia na Uhispania. (Fabrizio Romano)

Kocha wa Swansea, Russell Martin amekubali kuwa meneja mpya wa Southampton. (Sky Sports)

Martin, 37, amekubali mkataba wa miaka mitatu kuwa meneja mpya wa Southampton, huku klabu hiyo iliyoshuka daraja ya Premier League ikitarajiwa kutangaza kuteuliwa kwake siku zijazo. (Sun)

Russel

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

Kocha wa Swansea, Russell Martin amekubali kuwa meneja mpya wa Southampton.

Barcelona wameshangazwa na tetesi kwamba mlinzi wa Ufaransa Jules Kounde, 24, anataka kuondoka katika klabu hiyo, mwaka mmoja tu baada ya kujiunga nayo kutoka Sevilla. (90 Min)

Manchester United wako tayari kulipa pauni milioni 55 kumnunua kiungo wa Chelsea na England Mason Mount na nia yao kuzishinda Liverpool na Arsenal katika mbio za kuinasa saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mail)

Mount atajadili mustakabali wake wa Chelsea katika mkutano na uongozi wa klabu hiyo wiki ijayo. (90 Min)

Mount ataelekea Manchester United ikiwa Chelsea itaamua kumuuza. (The Atheletic- Usajili unahitajika)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?