Teknolojia ya kupunguza kasi ya kuzeeka kwa binadamu

w

CHANZO CHA PICHA, BRAIN JOHNSON

Katika miaka 150 iliyopita, umri wa kuishi wa wanadamu unaweza kuwa umeongezeka maradufu. Hata hivyo, watu wengi wanakatishwa tamaa sana na mabadiliko yanayotokea katika Maisha yao wanapoanza kuzeeka.

Lakni Teknolojia mpya inaibuka ili kupunguza hali hii ya kuwakatisha watu tamaa. Wanasayansi wanasema kwamba teknolijia hii itawasaidia watu kuishi Maisha yenye afya tele na muda mrefu pia.

Wanasayasani wanafanya kila juhudi ili kupunguza hatari na mateso wanayopitia watu kutokana na ugonjwa unaovamia mwili, kupitia matibabu mengi ya kisasa.

Mara nyingi Matibabu hutolewa ili kupunguza kudhoofika kwa seli za mwili, na ili kufanikisha jambo hilo vidogo hutolewa kwa wagonjwa.

g

CHANZO CHA PICHA, BRAIN JOHNSON

Maelezo ya picha, 

Brain Johnson akiwa na mwandishi wa BBC Laura Levinington

Fursa za biashara katika sekta hii kupitia matibabu haya pia zimekuwa zikiongezeka katika siku za hivi karibuni.

"Nilienda California ili kujua kama masomo haya na matibabu ni mradi wa kutengeneza pesa tu au kuchangia maendeleo katika uwanja wa matibabu," mwandishi wa BBC Laura Levinington alisema.

Brain Johnson, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 45, anatumia mamia ya maelfu ya dola kwa matibabu ya vinasaba ili kumfanya aonekane ana muonekano wa mtu mwenye umri wa miaka ishirini au mtu wa makamo.

Tunapozeeka, kuna mabadiliko mengi katika mwili wetu. Mwili umeharibiwa sana. Chanzo cha saratani, kisukari na magonjwa ya moyo ni kutokana na umri.

Wataalamu wanaamini kwamba matukio ya magonjwa haya yanaweza pia kupunguzwa kwa kupunguza hali ya uzee.

w

CHANZO CHA PICHA, BBC LAURA LEVININGTON

Brian , aligeuza nyumba yake iliopo katika ufukwe wa kifahari wa Venice kuwa kliniki ya Johnson. Kiliniki ya kutoa tiba ya kuwa na muonekano wa vijana.

Ratiba yake katika kliniki hiyo huanza mapema asubuhi saa kumi na moja kabla ya jua kuchomoza , kisha watu hupata kiamshwa kinywa zoezi linaloendelea mpaka saa sita mchana kisha baada ya hapo chakula cha mchana ambacho kina aambatana na vidoge 54 vya lishe yenye lengo la kuzuia uzee.

Mwili wa Johnson utafanyiwa uchunguzi kwa mara kwanza na madaktari wataamua kipimo cha dawa hizi na muda wa kuchukuliwa.

Johnson hatumii tu dawa peke yake, ratiba yake ya kupunguza uzee inajumuisha maozezi kila siku na lishe bora.

Kwa matibabu ya laser ya ngozi, umri wa ngozi pia umepunguzwa hadi miaka 22. Johnson anasema ngozi yake inaoneka kama mtu mwenye umri mdogo kuliko hata muonekano wa mwili wake.

"Ngozi yangu ni sehemu muhimu sana ya kuimarisha urembo wangu na kunifanya niwe na nguvu mara kwa mara," Johnson alisema.

Johnson anashikilia umuhimu mkubwa kwa afya. Tembea kilomita 5 kila siku. Jaribu kadiri uwezavyo kuzuia mwili kushambuliwa na ugonjwa wa kisukari .

Jinsi ya kuweza kuishi kwa maisha marefu

"Jeni husaidia tu katika asilimia 7 ya muda wa maisha yako. Asilimia 93 iliyobaki inategemea mtindo wako wa maisha," Eric Verdin, mtendaji mkuu wa Taasisi ya Buck ya Utafiti wa Uzee alisema.

Aliongeza kuwa wale wanaofuata maisha ya afya wataishi kwa miaka 95. Muda wao wa kuishi ni miaka 15 hadi 17 zaidi ya wastani wa umri wa kuishi wa mwanadamu, Eric alisema.

Lakni , watu wengi wanafanya utafiti ili kujua ni maisha gani ya kiafya yanahusika.

Kula chakula chenye afya, kutotumia sukari kwa kiasi kikubwa , na kupata usingizi wa kutosha ni muhimu katika afya.

"Ninafuata kila siku mazoezi mengi, kufunga kwa saa chache, kupata usingizi mzuri, mahusiano ya kijamii, na kunywa pombe kidogo," Eric alisema.

"Jaribu kutokula kwa angalau saa 24 kati ya saa 14. Kwa sababu inasaidia pakubwa kwenye mmengenyeko wa chakula .

w

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

"ni vyema kuatilia mienendo ya hali ya afya mara kwa mara.

Tunapozeeka, tunahitaji kutunza mwili wetu ipasavyo. Afya inapaswa kuchunguzwa mara kwa mara. Ikiwa matatizo yoyote ya afya yanatokea, matibabu yanayotakiwa yanapaswa kuchukuliwa kwa wakati unaofaa.

Eric anasema kwamba njia hii inapaswa kuwa sehemu ya maisha na inaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha.

Wengi wa washiriki katika utafiti wanatumia zaidi ya njia moja mahiri ili kuongeza muda wa kuishi.

Saa ya kunakili mapigo ya moyo na umbali uliotembea hutumika kutambua michakato katika mwili na pete pia hutumika kufuatilia nyakati za kulala. Watafiti wengi wanasema kwamba pete ni nzuri zaidi kuliko saa wakati wa kulala.

w

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Je, kuwa na maisha marefu pia ni tatizo?

Matarajio ya maisha ya watu yanaongezeka taratibu. Umri wa kuishi umeongezeka baada ya ujio wa teknolojia nyingi za kisasa katika uwanja wa dawa. 

Hata hivyo, katika wakati ambapo umri wa kuishi wa watu unaongezeka, je, tunaweza kufikiria kuzeeka kuwa ugonjwa baada ya umri fulani? Maswali yanaibuliwa.

Ikiwa umri umewekwa kuelezea uzee, gharama ya matibabu kwao pia itaongezeka mara kumi.

Mara tu wanapofikia umri fulani, kuna hatari kwamba wataitwa 'wagonjwa'.

Maisha yenye afya inamaanisha kuwa watu wataweza kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi. Hii ina maana kwamba saa za kazi za watu pia zitaongezeka.

"Baada ya kurudi California, ninafuata maisha ya afya. Nimebadilisha maisha yangu ya kila siku. Ninalala vizuri na kufanya mazoezi kila siku. Ninakula chakula kizuri," alisema mwandishi wamakala ya Afya Laura Levinington.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?