SUGU: Niliamua Kukubali kwamba nimefungwa bila haki, kwa hivyo sikuwa na majuto

Aliposimama kuwa mbunge nchini Tanzania, Joseph Mbilinyi aka Sugu hakudhani kwamba angefika gerezani. 

Katika mahojiano mapya na kipindi cha redio cha Newsday Swahili Outlook amesimulia hadithi yake, kutoka miezi ya kwanza mjini Mbeya, mpaka Maisha yake bungeni Dodoma. 

Sugu alijipatia umaarufu na hip hop ya Kiswahili miaka ya 1990, alihamia kwenda Dar es Salaam kufuata ndoto yake kuwa mwanamuziki. Alijitahidi kupata wakati studioni na kukabili ushawishi wa mitaani. 

“Harakati ilikuwa halisi, unajaribu sana usifungwa katika jinai. Mara nyingine jinai inaonekana kuwa njia rahisi. Lakini mimi niliamua kwenda njia ndefu,” alisema.

Sugu anazungumzia alipofanya kazi na producer Master J na DJ Mike Mhagama, kuelezea kwa nini albamu yake ya kwaza alirekodiwa ndani ya studio ya kanisa, na alipotangazwa redioni kwa mara ya kwanza.

Anajulikana kwa maneno makali sana katika muziki wake, mara nyingine huwa na vina na maneno ya kisiasa. Mwaka wa 2010 aliingia kwenye siasa baada ya kuingia bungeni alipochaguliwa kuwa mbunge wa upinzani. Lakini mwaka wa 2018 alifungwa jela baada ya kumkosoa Rais John Pombe Magufuli. 

“Nilichagua kukubali uhalisi kwamba nimefungwa bila haki, kwa hivyo nilikuwa sina majuto. Ni gharama ya kulipa kama ukishindania demokrasia,” alisema.

Alikuwa gerezani kwa zaidi ya miezi miwili baada ya kuonekana na hatia ya uchochezi dhidi yar rais, lakini baadae aliachiliwa huru.

Rais wa sasa wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amebadilisha baadhi ya sera za mtangulizi wake, na Sugu ana uhasiano bora naye. Rais huyo alijumuika katika sherehe ya Sugu kusherekea miaka thelathini katika biashara ya muziki.

“Ilikuwa kitu kizuri sana, licha ya mimi, lakini kwa heshima ya muziki wa hip hop. Ilikuwa bomba kabisa,” anasema Sugu. 

Sikiliza mahojiano kwa urefu, akuzungumzia alivyoendelea kama mwanamuziki, na uzoefu wake wa kuwa mwanasiasa:

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?