Tetesi za soka Ulaya Jumanne 30.05.2023

Harry Kane

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Tottenham wamedhamiria kuzima majaribio ya Manchester United ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa England Harry Kane, 29, msimu huu wa joto, huku mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy akigoma kumuuza Kane kwa timu pinzani ya Ligi kuu England. (Mirror)

Erik ten Hag ana imani kuwa anaweza kumshawishi kiungo wa kati wa Chelsea Mason Mount mwenye umri wa miaka 24 ajiunge na Manchester United kama sehemu ya maboresho ya kikosi chake kwenye usajili wa majira ya joto. (Telegraph)

Bayern Munich wako tayari kulipa pauni milioni 95 kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, huku timu hiyo ya Ujerumani ikiwa na nia ya kuipiku Arsenal katika kuinasa saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mirror)

Paris St-Germain wana nia ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal na Norway Martin Odegaard mwenye umri wa miaka 24. (Mail)

Martin Odegaard

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

Martin Odegaard

Tottenham, Newcastle na Arsenal ni miongoni mwa vilabu vya Ligi kuu ya England vinavyomtaka James Maddison wa Leicester. Kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 26 anaweza kununuliwa kwa takriban £40m. (Mirror)

Crystal Palace wamemtafuta mkufunzi wa zamani wa Chelsea na Brighton Graham Potter kuziba nafasi ya kocha iliyo wazi, huku Nice pia ikimtaka Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 48. (Footmercato)

Liverpool wamekataa ofa ya kudumu ya uhamisho kutoka nje ya nchi kwa kiungo mshambuliaji wa Ureno chini ya umri wa miaka 21 Fabio Carvalho huku klabu hiyo ya Merseyside ikifikiria kumtoa kwa mkopo tu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Athletic)

West Ham wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumnunua James Ward-Prowse, huku Southampton wakisema thamani ya kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 28 ni pauni milioni 40. (Sun)

James Ward-Prowse

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

James Ward-Prowse

Newcastle wana imani kuwa kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes, 25, atasaini kandarasi mpya huko St James' Park licha ya kutakiwa na Barcelona. (90Min)

Mshambulizi wa Brazil Roberto Firmino, 31, ambaye ataondoka Liverpool msimu huu wa joto, anasubiri kuona kama atafaa kwenye mipango ya Real Madrid kabla ya kuchukua uamuzi wa kuhamia Hispania. (Mail)

Kocha wa Barcelona Xavi amekiri kuwa yuko kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Argentina na Paris St-Germain Lionel Messi mwenye umri wa miaka 35 kuhusu kurejea Camp Nou msimu wa joto. (Standard)

Lionel Messi

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

Lionel Messi 

Everton inamtaka mshambuliaji wa Mali El Bilal Toure mwenye umri wa miaka 21 baada ya kurejea kwenye kikosi cha kwanza cha Almeria siku ya Jumapili. (Mail)

Chelsea wameanzisha mazungumzo kuhusu mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Uruguay na Sporting CP Manuel Ugarte, 22. (90Min)

Crystal Palace wanafikiria kumchukua kwa mkopo kiungo wa kati wa Chelsea na England wa chini ya umri wa miaka 19 Lewis Hall, 18. (Mail)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?