Mazungumzo ya amani: Mjumbe wa Marekani hafurahii mpango wa kuwaachia wafungwa wa Taliban

Mjumbe wa Marekani katika mkutano wa kutafuta amani nchini Afghanstan ameiambia Newsday Swahili kuwa "hafurahii" makubalino yenye utata ya kuwaachia huru wafungwa 5,000 wa Talban ili kufanikisha mazungumzo ya amani ya kihistoria.
Hatahivyo mwakilishi huyo Lyse Doucet, Zalmay Khalilzad aliongeza kuwa "Inabidi kufanya maamuzi magumu".
Alipoulizwa kuhusu waliokuwa wafungwa kurejea katika mapigano, bwana Khalilzad alisema "hawana ushahidi wowote".
Mazungumzo ya Amani kati ya viongozi wa Afghan na Talban yalianza mjini Qatar siku ya Jumamosi.
Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya Afghanistan kuwa na mazungumzo ya amani na kundi la wanamgambo wa kiislamu.
Lengo likiwa ni kusitisha mapigano ya miaka 19.
Kuachiwa huru kwa wafungwa 5,000 lilikuwa sharti walilokubaliana Marekani na Taliban baada ya mazungumzo ya amani ya mwaka jana na kuanza mazungumzo haya.
Serikali ya Afghanistan haikuhusishwa katika kuweka makubaliano hayo na wana wasiwasi kuhusu kuachiwa huru kwa maelfu ya wanamgambo. Mwezi uliopita rais wa Afghanistan Ashraf Ghani alitoa angalizo kuwa kuachiwa huru kwa wafungwa ni jambo 'hatari' duniani, Shirika la habari la Ufaransa, AFP liliripoti wakati huo.
"Mpaka suala hili kufika, walikuwa wanatamani kuufikia mpango wa amani lakini si kwa gharama hiyo," Bwana Ghani alisema.
Lakini bwana Khalilzad alikataa kuwa kukubali kuachia huru wafungwa wengi - baadhi yao walikuwa hatari sana hivyo "lilikuwa ni kosa".
"Ninathamini jitihada walizozifanya serikali," aliiambia BBC. "Ninawapongeza kwa kufanya maamuzi magumu. Maamuzi hayo yameweza kusababisha mazungumzo hayo ya amani kufanyika kwa mara ya kwanza."
Taliban imeondolewa madarakani nchini Afghanistan baada ya uvamizi wa Marekani mwaka 2001.
Kundi hilo limepata nguvu ya kudhibiti maeneo mengine zaidi tangu wakati huo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?