Maktaba kubwa ya propaganda za kundi la IS yabainika

Moja ya eneo kubwa lenye mkusanyiko wa nyenzo nyingi za matandaoni za kundi la Islamic Stale limebainika na watafiti katika Taasisi ya majadiliano ya Kimkakati.
Maktaba hiyo ya mtandaoni ina nyenzo zaidi ya 90,000 na inasemekana wageni wanaoitembelea kwa mwezi idadi yao inakadiriwa kuwa 10,000.
Wataalamu wanasema maktaba hiyo imewezesha kundi hilo lenye msimamo mkali kubadilisha na kuongeza maudhui yake mtandaoni.
Lakini kuondoa maktaba hiyo ni changamoto kwasababu data hiyo haihifadhiwi sehemu moja.
Licha ya hatua za kukabiliana na ugaidi, Uingereza na Marekani zimetahadharishwa kuhusu maktaba hiyo inavyozidi kupanuka.
'Gaidi mzuri'
Ugunduzi wa maktaba hiyo umewadia baada ya kufariki dunia kwa kiongozi maarufu Abu Bakr al-Baghdadi, Oktoba 2019.
Wakati huo, ujumbe mwingi wa mitandao ya kijamii unaounga mkono shirika ukiwa na viunganishi vifupi
Viunganishi hivyo vimesaidia watafiti kufikia nyaraka na video zilizohifadhiwa kwa lugha tisa tofauti.
Walijumuisha taarifa za mashambulizi ikiwemo yaliyotekelezwa katika maeneo ya Manchester Mei 22, 2017, na Uingereza Julai 2005 na Marekani September 2001.
"Kuna kila kitu unachohitajika kujua ili kupanga shambulio," amesema naibu mkurugenzi wa Taasisi ya Majadiliano ya Kimkakati Moustafa Ayad, aliyefumbua hifadhi hiyo.
"Mambo yanayokufunza kuwa gaidi mzuri."
Kwa miezi kadhaa sasa, watafiti wamekuwa wakitafiti chimbuko la kundi hilo na jinsi linavyoendeshwa na nani anayewatembelea.
Data inasambazwa katika sehemu mbalimbali badala ya kuhifadhiwa kwenye kompyuta moja.
Na yeyote yule anaweza kusambaza taarifa hiyo kwenye tovuti, kupitia mfumo katika maeneo mbalimbali.
Na hilo linazuia juhudi zozote za kutaka kuondoa data hiyo.
Mradi utawala wa khalifa inaendelee kuwepo, utasaidia kundi la IS kuwapa njia ya kuendelea kuongeza na kuhifadhi data yao.
Mwanamuziki wa Pop
Nyenzo hizo zimejumuishwa kwenye kurasa za maoni ya mitandao ya kijamii na kusambaa kupitia akaunti zinazojieleza kwa uwazi.
Mbinu nyingine imekuwa kulenga kaunti za Twitter zenye kuhusishwa na watu ambao ni nyota na wanariadha.
Kwa mfano, IS ili teka nyara akaunti ya shabiki wa muziki wa kufokafoka, Justin Bieber na kuitumia kueneza nyenzo yao kutoka kwenye hifadhi yao.
Katika tukio jingine, kundi hilo lilifanikiwa kupumbaza akaunti ya timu ya raga ya Uingereza na ikaanza kulifuatilia kwa kujionesha kama mashabiki wao.
"Wanaelewa sio tu kupumbaza majukwaa ya mitandaoni, wanajua nguvu ya maudhui yao katika hifadhi hiyo," Bwana Ayad amesema
Sio kwamba maudhui yao yote ni ya kufanya vurugu.
Wageni wanaotembelea tovuti yao wanakabiliana na falsafa za IS, ujumbe wa masuala ya dini na taarifa za propaganda kuhusu jinsi maisha ya IS yalivyo.
Watafiti wanasema hilo linajumuisha wake wa kundi hilo waliotoroka kama vile Shamima Begum
Wengi wanaojiunga ni wanaume wenye umri wa kati ya miaka 18 na 24 ambao mara nyingi ni kutoka nchi za kiarabu, huku asilimia 40 ya wanaojiunga wakitoka kwenye mitandao ya kijamii, na kiasi kikubwa kutoka mtandao wa You Tube.
Makundi yenye msimamo mkali.
Taasisi ya Majadiliano ya Kimkakati pia imebaini kwamba hifadhi hiyo ya data zao sio kitu cha kipekee.
Kuna hifadhi nyingine ndogo ndogo za makundi mengine madogo madogo, mengi yao yakiwa pia yanatumia majukwaa ya mitandao ya kijamii yaliyotawanyika.
Mvuto wa majukwaa haya ni kwamba wavumbuzi wa majukwaa hawana namna ya kwenda kinyume na maudhui hayo yanayohifadhiwa kwenye kwenye hifadhi za watumiaji au maudhui ambayo yanashirikishwa katika mtandao ulitawanyika wa watumiaji, " Mtaalamu wa Newsday Swahili ambaye wa masuala ya maudhui ya Mina Al-Lami.
"Inahusu zaidi faragha, uhuru na ufichaji wa data''
"Hilo ndilo linalovutia wapiganaji wa jihadi."
Watafiti hao wametahadharisha ofisi ya Mwendesha mashtaka mkuu mashariki mwa mji wa New York, ambayo imefungua kesi nyingi za kukabiliana na ugaidi pamoja na polisi wa mji.
Mamlaka ya mji wa New York haijasema lolote kuhusiana na hilo
Lakini ofisi ya mji imekiri kupokea ujumbe na kusema kwamba inatathmini na maafisa wataalamu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?