Virusi vya corona: Madhara ya Covid-19 kwa wagonjwa wasioonesha dalili za virusi

Baadhi ya watu wenye maambukizi ya virusi vya corona, huwa hawana dalili zozote za ugonjwa, lakini je hii inamaanisha kuwa hawaumwi?
Matibabu ya kisasa yanasisitiza ukweli juu ya umuhimu wa sayansi.
Mtazamo wetu hatahivyo mara nyingi hutofauti na lengo halisi la huduma za matibabu ya wagonjwa.
Suala hilo lilizungumziwa na William Osler katika onyo lake alilotoa kati ya 1849-1919 ambapo aliwaasa wanasayansi kumjali zaidi mgonjwa kuliko ugonjwa.
Ukweli juu ya ushauri huu ulibainika wakati wagonjwa wawili walipothihirisha hayo walipopata maambukizi ya covid-19 na kuwafanya wahudumu wa afya kujiuliza maswali mengi juu ya uzoefu wao wa kutibu homa ya mapafu.
Mgonjwa wa kwanza wa covid-19 katika hospitali yangu alikua ni mgonjwa wa kama mgonjwa mwingine anayeweza kufika kwa mara ya kwanza katika hospitali nyingine yoyote, anasema John Kinnear Mkurugenzi wa Chuo kikuu cha udaktari cha Anglia, kilichopo nchini Uingereza.
Alikua ni mwanaume mkongwe ambaye alikua na homa ya mapafu, ambaye alikua hajafanyiwa vipimo kwa virusi vipya vya corona, lakini alikua navyo.
Timu ya wataalamu walimchunguza kwa makini , wakamuandikia dozi ya juu ya hea ya oksijeni, na wakamfuatilia kwa karibu. Usiku ule, alikufa bilakutarajia.
Mgonjwa wa pili alikua ni mwanamke mwenye umri wa miaka zaidi ya thelathini, ambaye alilazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi ili awekwe kwenye mashine ya kumuongezea hewa ya kupumua.
Kifo cha hivi karibuni kimenifanya nihisi kuwa mwenye wasiwasi, kwa hiyo nikaenda kukitathmini. Nilipokua kua nikienda kumtazama, mawazoni nilifikiria kile ambacho ninakitarajia: mgonjwa mwenye tatizo kubwa la kupumua, asiyeweza kuongeza vizuri, ambaye kifua chake kinatoa mlio wa sauti, akihangaika kujitahidi kuingiza oksijeni katika damu yake.
Lakini nilipoingia huku nimevalia mavazi ya kujikinga na maambukizi PPE, na nikiwa tayari kumchoma sindano ya nusu kaputi ili nimwekee mirija ya kumsaidia kupumua mara moja, nilifikiriniko katika kitanda chama mgonjwa ambacho sikua nimekukusudia.
Mgonjwa alikua ameketi kwa starehe kwenye kitanda chake, akiongea kwa simu yake na mtoto wake wa kike, akionekana kunishangaa. Lakini nikapima oksijeni kaytika damu yake kama kuthibitisha tu kuwa ana maambukizi na wala si kwa hofu, maana alikua anaonekana mzima wa afya.
Kwa muonekana wa damu yake, nilitarajia matokeo yawe ya kawaida kabisa kwa (100%). Matokeo yalikuwa 75%, kiwango ambacho humfanya daktari awe na wasi wasi.

Kuharibika mapafu

Nilitambua haraka kwamba wagonjwa wengi waliougua sana covid-19 hawakuwahi kuwa na dalili kali za ugonjwa wa pumu hadi wanapoanguka ghafla na kufa.
Sayansi iliyonyuma ya somo hili lililotolewa awali sasa linajitokeza, huku utafiti kutoka Wuhan, China ukielezea mabadiliko makubwa katika mapafu yanayoweza kuonekana kupitia kipimo cha CT scans kwa wagonjwa ambao hawaonyeshi kabisa dalili za ugonjwa.
Ukosefu wa dalili za corona zio jambo lisilo la kawaida kwa virusi vya aina nyingine viya maambukizi kama vile methicillin- Staphylococcus aureus au MRSA na C diff ( Clostridioides difficile ), lakini kile kinachoshangaza kwa virusi vya SARS-CoV-2 (vinavyosababisha covid -19) ni Kwamba vinaweza kusababisha kuharibika kwa viungo vya ndani ya mwili hasa vinapompata mtu mwenye magonjwa mengine ya kudumu, kama vile maradhi ya kisukari, moyo na Ukimwi.
Watafiti walibaini kuwa virusi husababisha kuumia kwa sehemu ya ndani ya mapafu, lakini hilo si kwa maambukizi ya virusi vya SARS-CoV-2 pekee, kwani hali hii inaweza kushuhudiwa kwa mgonjwa mwenye magonjwa mengine ya mapafu.
Kile ambacho kimesalia kuwa jambo la kushangaza ni kwamba , licha ya mabadiliko haya, ni kwanini baadhi ya wagonjwa hawaonyeshi dalili za homa ya mapafu, kama vile matatizo makubwa ya kushindwa kupumua?
Takriban robo ya wagonjwa katika utafiti walionyesha kuwa na homa, kikohozi na kushindwa kupumua, lakini wengi hawakuonyesha dalili hizi
Kujificha kwa dalili za maambukizi ni mojawapo ya mambo a,mbayo hayajafahamika juu ya covid-19, kiasi kwamba virusi hivi hushambulia baadhi ya watu lakini sio wengine : Watu wawili wanaoishi katika mazingira ya aina moja na hali ya afya iliyo sawa wanaweza kupatwa na kuathiriwa na maambukizi hayo kwa namna tofauti.
Utafiti unasisitiza kuwa ukosefu wa dalili za corona haimaanishi ukosefu wa athari zake mwilini.






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?