Tiba ya corona: Mgonjwa wa 91' aliyezua hofu katika taifa zima la Vietnam

Iwapo angekuwa katika eneo lolote jingine , angekuwa amefariki. Wangezima mashine ya kumsaidia kuishi baada ya siku 30'', anasema Stephen Cameron akiwa katika kitanda chake cha hospitali.
Raia huyo wa Uskochi mwenye umri wa miaka 43 aliishi siku 68 akiwa anasaidiwa na mashine ya kupumua .
Huu ndio muda mrefu zaidi ambao haujawahi kutumiwa na mgonjwa mwingine yeyote nchini Uingereza katika hali hiyo.
Lakini hakuwa amelazwa katika wodi ya hospitali ya Motherwell , nyumbani kwao bali katika chumba cha wagonjwa mahututi cha Ho Chi Minh, nchini Vietnam bila marafiki ama watu wake wa familia yake.
Cameron ambaye alikuwa ndie mgonjwa wa mwisho katika chumba cha wagonjwa mahututi nchini Vietnam ni mgonjwa ambaye ameugua sana nchini humo wakati wa mlipuko wa virusi vya corona.
Taifa la Vietnam lenye wageni milioni 95, lilikuwa na wagonjwa wachache waliothibitishwa kuwa na corona , huku chini ya 10 wakilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na hakuna kifo chochote kilichotangazwa.
Ugonjwa wa Cameron haukuwa wa kawaida nchini Vietnam hatua ambayo ilisababisha hali yake kuripotiwa kila dakika katika magazeti ya kitaifa pamoja na televisheni.
Alisalia na asilimia 10 pekee ya kuweza kupona.
Makumi ya wataalam wa vyumba vya wagonjwa mahututi nchini Vietnam walifanya mikutano ya video ya mara kwa mara ili kujadiliana kuhusu hali ya Cameron.
"Kutokana na idadi ndogo ya wagonjwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi, ilimaanisha kwamba kila mgonjwa aliye katika hali mahututi aliwavutia madaktari wa hali ya juu nchini '', anaelezea Dkt. Kidong Park, mwakilishi wa Shirika la afya duniani WHO nchini Vietnam.
Kwa muda wa miezi miwili na nusu Bwana Cameron alikuwa amelazwa akiwa hana fahamu, na alitegemea mashine ya oksijeni inayotumika kusaidia mtu aliye katika hali mahututi kuwa hai.
Mashine hiyo ilikuwa ikichukua damu kutoka kwa mwili wake kuichanganya na oksijeni kabla ya kuirudisha mwilini mwake.
"Nina bahati kwa kuwa tatizo langu sasa ni kushindwa kusukuma miguu yangu , lakini ninafanyiwa tiba ya viungo katika miguu yangu mara mbili kwa siku'', alisema Cameron.
"Wakati mmoja, wizara ya masuala ya kigeni ilimwambia rafiki yangu Craig kwamba nilikuwa na asilimia 10 kupona , hivyobasi akajianda kwa lolote lile.
Aliifahamisha idara niliokuwa nikifanyia kazi na kuanza kufanya kile ambacho mtu angefanya iwapo mtu angerudi nyumbani akiwa ndani ya jeneza.
Tangu alipopata fahamu , alianza mawasiliano ya simu na marafiki nyumbani kwake huko nchini Uskochi ambao hawakufikiria kwamba angerudi akiwa hai ."
Madaktari walilazimika kukabiliana na magonjwa kadhaa tofauti wakati Cameron alipokuwa amepoteza fahamu: Alikuwa na mgando wa damu, figo zake zilikuwa zimeathirika - ikimaanisha kwamba zilihitaji kusafishwa.
Ilipotangazwa katika vyombo vya habari kwamba alihitaji upandikizaji wa pafu moja , wengi walijitolea akiwemo ajuza mmoja mwenye umri wa miaka 70 ambaye alipigana katika vita vya Vietnam'', anatabasamu.
''Lakini iwapo ingekuwa upandikizaji wa mapafu mawili hilo lisingekuwa na mwisho mwema kwake."
Lakini licha ya kupata usaidi mkubwa kutoka kwa raia wa Vietnam huku mamia ya maelfu ya madola yakitumika kumtibu Stephen Cameron, habari za yeye kupatikana na virusi vya corona hazikupokelewa vyema.

Kundi la Baa ya Buddha

Cameron alianza kuugua wiki chache baada ya kuwasili nchini Vietnam mapema mwezi Februari.
Kama marubani wengine wengi kutoka mataifa ya magharibi, alielekea bara Asia kusomea kazi yake ili kujiongezea mshahara.
Lakini siku mbili kabla ya kupeleka ndege yake ya kwanza katika kampuni ya ndege ya Vietnam, na siku ya mkesha wa safari hiyo baa nyingi na mikahawa ya burudani vilifungwa katika eneo la Ho Chi Minh, ili kuzuia maambukizi ya corona, hivyobasi alikwenda kukutana na rafikiye katika baa moja iliyopo mtaa jirani wa mji huo.
Wakati huo, Vietnam ilikuwa na chini ya wagonjwa 50 wa corona, lakini kulingana na Guy Thwaites, mkurugenzi wa kitengo cha utafiti katika chuo kikuu cha Oxford kilichopo katika mji wa Ho Chi Minh na mshauri wa serikali kuhusu magonjwa ya maambukizi, anasema kwamba raia tayari walikuwa na hofu kuhusu virusi hivyo.
Ilikuwa wikendi kabla ya kuadhimisha siku ya St Patrick , hivyobasi baa ya Buddha ilikuwa imejaa, huku wateja wakiwa wamevalia nguo za Ireland wakati Cameron alipowasili muda mfupi baada ya saa nne usiku.
"Sinywi pombe, mara nyingi nilikuwa peke yangu katika kona moja ya baa hiyo, nikacheza michezo michache ya Billiards na kwenda nyumbani muda wa saa tisa na robo alfajiri'' , anakumbuka.
Hatahivyo alivyoanza kuhisi joto mwilini siku iliofuatia baada ya safari yake ya ndege, watu 12 walipatikana na maambukizi baada ya kufanyiwa vipimo.
Baa ya Buddha Group kama ilivyotangazwa katika vyombo vya habari ilisababisha mlipuko mkubwa wa corona kusini mwa taifa hilo, huku watu 20 wakidaiwa kuambukizwa.
Na wengine katika mitandao ya kijamii walisema kwamba ni makosa ya Cameron ambaye amekuwa akizuru mji huo.
Ijapokuwa hakuna ushahidi kwamba yeye ndio chanzo cha maambukizi hayo, mfanyabishara maarufu , Luong Hoai Nam alimtaja Cameron ''kama bomu lililokuwa likisubiri muda wake kulipuka''.
Aliwataka raia wa kigeni wanaovunja sheria kurudishwa makwao, hatua ilioungwa mkono na wafuasi wake katika mitandao ya kijamii.
"Kulikuwa na sababu ya kuniwekea lawama ya mlipuko huo, kwasababu nilikuwa nimetoka Bangkok wiki moja kabla kutatua suala la visa yangu'', alisema Cameron ambaye anadai aliambukizwa katika baa hiyo ya Buddha na kwamba hakuwa chanzo cha mlipuko huo.
''Nilikua mtu wa kwanza kutoa sauti yangu na kusema, tazama, sihisi vyema . Ilikuwa wazi kwamba watanilaumu''.

Hali yake ilidhoofika

Mnamo tarehe 18 mwezi Machi , Cameron alilazwa hospitalini baada ya kugunduliwa na virusi vya corona , na mamlaka zikaamua kuifunga baa na kumtenga kila mtu aliyeishi katika jengo hilo. Kwa jumla takriban watu 4000 waliohusishwa na baa hiyo walipimwa corona.
"Hatahivyo hali ya mgonjwa wa 91 ilidhoofika kwa haraka'' , anakumbuka Luong Ngoc Khue, ambaye ni miongoni mwa jopo la maafisa wa afya katika wizara ya afya nchini Vietnam na mshauri wa tiba ya Cameron.
Utendakzi wa viungo vya vya mwili kama vile mapafu , figo , ini na damu yake ulipungua.
Huku hali yake ikizidi kudhoofika , Cameron anakumbuka kuomba kuwekewa mashine ya kumsaidia kupumua .
''Nilikuwa nimechoka kwasababu sikuweza kulala'', .Na baadaye alikuwa katika koma kwa wiki kadhaa , huku madaktari wakichoshwa na matibabu yake .
Wakati huohuo wagonjwa wachache waliokuwa wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi nchini Vietnam walipona na kwenda nyumbani.
Kisa chake kilipata umaarufu. Viongozi wa kisiasa walimuahidi kufanya chochote katika uwezo wao kumuwezesha kuishi huku hospitali aliokuwa amelazwa ikichukua gharama za matibabu yake.
"Kuna pongezi nyingi ambazo Vietnam inaweza kupata kutokana na kupona kwangu ," anasema Cameron , "na anasisitiza kuhusu vita vyake vya Covid -19 ambapo kuna wagonjwa wachache tu nchini humo.
Khue anasisitiza kwamba kila mtu, wageni na raia wa Vietnam walipata matibabu ya kiwango cha juu. ''Tunatilia mkazo kuwatibu wagonjwa kwa kiwango cha juu, kupitia vifaa bora na nguvu kazi, bila kujali uraia'', anasema.
Alijigamba akisema kwamba takriban wagonjwa 49 kati ya 50 wa kigeni walipona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

''Hazikuwa siku za kawaida''

Wakati Stephen Cameron alipowekewa mashine ya kumsaidia kupumua mapema mwezi Aprili, kulikuwa na wagonjwa zaidi ya milioni moja duniani.
Wakati madaktari walipomuamsha tarehe 12 mwezi Juni , kulikuwa na zaidi ya wagonjwa milioni 7. Lakini Vietnam ilifanikiwa kuzuia mlipuko huo mbaya zaidi . Hakujakuwa na kisa chochote cha maambukizi ya wenyewe kwa wenyewe tangu tarehe 6 Aprili.
"Sikufikiria itachukua takriban wiki 10 kwa mimi kuamka''.
Katika kitanda chake kilichokuwa katika chumba cha kibinafsi katika hospitali ya Cho Ray katika eneo jingine la mji wa Ho Chi, ambako nilihamishwa baada ya kugunduliwa sina corona , Cameron anahisi changamoto za kushindwa kutembea na kuugua kwa miezi kadhaa.
Amepoteza takriban kilo 20 na misuli yake imedhoofika hali ya kwamba analazimika kulazimisha mguu wake kutembea kwa nchi chache.Pia amechoka sana.
Nimeathirika vibaya kiakili. Kwa sasa , kile ninachokitaka kufanya ni kwenda nyumbani. Kile ninachokikosa ni mazingira yasio na kelele na joto. Kuna kelele hapa zinazosababishwa na bodaboda na bila kusahau msimu wa joto''.
Katika kipindi cha wiki chache zilizopita , sio tu madaktari wachache na manesi waliokaa kandokando ya kitanda chake , lakini pia wanadiplomasia wakuu, maafisa wa serikali wanasiasa akiwemo balozi wa Uingereza na mwenyekiti wa hospitali ya Ho Chi .
Anataka kurudi nyumbani kwao Uskochi. Matibabu yake yamekuwa ya gharama ya juu . Mashine ya kumsaidia kuishi hugharimu kati $ 5,000 na $ 10,000 kwa siku, na aliitegemea kwa wiki nane na nusu.
Mara ya kwanza hospitali hiyo ya kukabiliana na magonjwa ya kitropiki ililipa gharama ya matibabu yake. Hivyobasi wakadhania kwamba ubalozi wa Uingereza utaingilia. Bima ya kazi yake baadaye ikasimamia gharama hiyo. Lakini gharama ya matibabu yake katika hospitali ya Cho Ray bado haijalipwa.
''Ni kitu ambacho kinakera sana. Mara ya kwanza nilituma barua pepe kwa bima yangu ya afya na wakasema, ndio tutalipa. Sasa jibu ni kutatua tatizo hili hivi karibuni na hakuna kinachofanyika''.
Kwa sasa amehifadhiwa kiti katika kampuni ya ndege ya Vietnam kuelekea Uingereza arehe 12 mwezi Julai.
Wakati ambapo ndege zinaendelea kuwasafirisha raia wa Vietnam kutoka Ulaya, Cameron haelewi kwanini hawezi kurudi nyumbani mapema kwa kuwa aliambiwa amepona na anaweza kusafiri kwa ndege wiki moja iliopita.
Kwa kuwa yeye ni mtu maarufu nchini Vietnam kila kitu kinadhibitiwa na serikali, anasema.
Tatizo la yeye kurudi kwao ni kwamba kupona kimiujiza kwa mgonjwa huyo wa 91 sio tu hadithi ya rubani wa Uskochi ambaye alipona virusi vya corona.
Ni hadhithi ya jinsi taifa linaloendelea la kusini mwa bara Asia lilizongwa na misukosuko katika historia yake lilivyofanikiwa kudhibiti corona.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?