Marekani yazingirwa na virusi wakati ikisherehekea uhuru
Rekodi mpya ya idadi ya virusi vya corona imeweka kiwingu mwanzoni mwa herehe za uhuru nchini Marekani wakati ongezeko la maambukizi lailazimisha Uingereza kuwaweka wasafiri kutoka Marekani kwenye orodha mbaya.
Wakati fukwe zimefungwa kutoka eneo moja la pwani hadi jingine na maafisa wakiwataka Wamarekani kubakia majumbani mwao, hali isiyokuwa ya furaha kuelekea katika kile ambacho kwa kawaida ni mwishoni mwa juma kunakochomwa nyama na hali ya hewa ya jua imelemea mapambano ya kudhibiti ugonjwa wa COVID-19 katika kitovu cha janga hilo duniani.
Ni idadi usiyoweza kuamini," amesema Faisal Masud , mkurugenzi wa matibabu katika hospitali ya Methodist mjini Texas, ambayo maafisa wamesema inakaribia kabisa kuzidiwa na wagonjwa.
Ukigusa karibu kila nchi duniani tangu kujitokeza nchini China mwishoni mwa mwaka jana, virusi vya corona vimewaambukiza kiasi ya watu milioni 10.9 na kuwauwa watu 522,000 duniani, na kuzima uchumi uliokuwa hapo kabla ukikua kwa kasi na kusababisha maisha ya watu kuzimika.
Lakini wakati Ulaya na sehemu nyingi za Asia kwa kiasi kikubwa zimeweza kudhibiti virusi hivyo vya corona , kwa kiasi kikubwa Uingereza inajitayarisha kufungua biashara zake, mikahawa na cinema, lakini nchini Marekani ugonjwa huo umewauwa karibu watu 130,000 huku kukiwa na ongezeko kubwa la kesi mpya za maambukizi ambapo mtaalamu wa ngazi ya juu wa magonjwa ya kuambukiza Anthony Fauci amesema "unaiweka nchi nzima katika hatari."
Maoni
Chapisha Maoni