Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 24.07.2020: Cavani, Torres, Gimenez, Havertz, Alcantara, Zaniolo, Balotelli


Benfica imesitisha azma yake ya kumsaka mshambuliaji Edinson Cavani, 33, huku mchezaji huyo aliyekuwa Paris St-Germain akidai karibu pauni milioni 18 kwa kila msimu. (A Bola - in Portuguese)
Chelsea imekuwa ikimfuatilia mlinzi wa Atletico Madrid na Uruguay Jose Gimenez, 25, huku kocha Frank Lampard akiwa anafuatilia kutatua mapungufu ya upande wa ulinzi wa kikosi chake. (Telegraph - subscription required)
Leroy Sane, 24, alionekana kuthibitisha wakati anatambulishwa Bayern Munich kwamba mchezaji mwenzake wa Ujerumani Kai Havertz, 21, ianaelekea Chelsea kutoka Bayer Leverkusen msimu huu.

Chelsea na ajenti wa Havertz wamefikia makubaliano ya kibinafsi kwa ajili ya kiungo huyo wa kati wa Leverkusen. (Nicolo Schira, via Star)
Brighton haina mpango wowote wa kumuuza mlinzi wa Uingereza Ben White, 22, kwa Leeds United, ambapo amekuwa kwa mkopo msimu huu. (Mail)
Jesse Lingard, 27, amemtaka kiungo wa kati raia mwenzake wa Uingereza Jadon Sancho, 20, kuondoka Borussia Dortmund na kujiunga naye Manchester United msimu huu. (Evening Standard)

Bayern Munich imesema kuwa kiungo wa kati wa Uhispania Thiago Alcantara, 29, hataruhusiwa kuondoka klabu hiyo kiurahisi baada ya kuhusishwa kuhamia Liverpool. (Metro)
Valencia imesimama kidete kwa malipo inayotaka kwa winga Ferran Torres, 21, huku Manchester City ikiwa makini kumsajili mchezaji huyo wa kiamataifa wa Uhispani wa Under-21. (Telegraph - subscription required)
Ligi ya Serie A nchini Italia imethibitisha kwamba inafanya mazungumza ya kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester City na Liverpool Mario Balotelli. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia, 29 anaondoka kalbu yake ya sasa Brescia. (La Provincia di Como, via Football Italia)

Naibu mwenyekiti wa Manchester United Ed Woodward anafikiria kumteua mkurugenzi wa soka katika klabu hiyo msimu huu. (Telegraph - subscription required)
Sancho ni mmoja kati ya wachezaji watano ambao kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anataka wajiunge na kikosi chake. Hata hivyo huenda akalazimika kuuza baadhi ya wachezaji ili kupata pesa. (Telegraph - subscription required)
Mshindi wa kombe la dunia Marekani Sam Mewis, 27, anaelekea Manchester City kutoka North Carolina Courage, huku mwenzake Rose Lavelle, 25, pia akifikiria kuhamia City kutoka Washington Spirit. (Athletic)

Tottenham inamfuatilia kiungo wa kati wa Roma na Italia Nicolo Zaniolo, 21, ambaye wapania kumsajili.
West Ham imempanga kiungo wa kati wa Queens Park Rangers Eberechi Eze, 22, kama mchezaji wa kwanza wanae mlenga wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa huku Crystal Palace pia nayo ikiwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 20. (Evening Standard)
Aliyekuwa mshambuliaji wa Uholanzi na Arsenal Dennis Bergkamp amesema atakuwa tayari kurejea klabu hiyo kama kocha siku za usoni. (FourFourTwo)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?