Rais ameahirisha kura ya maoni yenye utata huku maandamano yakiendelea

Rais wa Guinea ameahir
isha kura ya maoni yenye utata iliyokuwa ifanyike leo Jumapili kuhusu kubadilishwa kwa katiba na iwapo itapita huenda ikamruhusu kuwania tena Urais kwa awamu ya tatu.

Alpha Condé, 81, amesema ameamua kuahirisha kidogo kura hiyo kwasababu upinzani umedai kuwa maafisa wameingilia sajili ya wapiga kura.

Tangazo hilo linawadia huku wasiwasi ukiendelea kuongezeka kuhusu suala la kura hiyo kufanyika kwa haki.

Maandamanao yenye ghasia yamekuwa yakishuhudiwa katika miezi ya hivi karibuni kupinga kura hiyo.

Karibia watu 30 wameuawa katika maandamano ambayo yamekuwa yakifanyika tangu Oktoba.

Umoja wa afrika na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), wamesema kwamba hawatatuma waangalizi wao kwa uchaguzi huo.

Inakadiriwa kuwa raia milioni 7.7 waliosajiliwa kupiga kura pia watapiga kura kuchagua wabunge.

Mapema wiki hii, Shirika la Kimataifa la Wazungumzaji wa Kifaransa, lilisema kwamba kuna tatizo la kutambua majina karibia milioni 2.5 katika sajili ya wapiga kura.

Je kura hiyo itafanyika kama ilivyopangwa?

Kulingana na rais, ndio itafanyika. Na kulingana na barua iliyotumwa na Bwana Condé kwa Ecowas kuhusu kuahirishwa kwa uchaguzi huo, ambayo ilionekana na shirika la habari la AFP, inasema kwamba uchaguzi huo utafanyika ndani ya wiki mbili.

Huku hakumaanishi kwamba ni kulegeza msimamo au kurudi nyuma. Raia wa Guinea tamchagua wanaempenda kwa uhuru katika kura ya maoni," amesema rais Condé katika runinga inayomilikiwa na serikali Ijumaa jioni.

Muungano wa upinzani uliokuwa unapinga katiba mpya, FNDC, umetoa wito wa kususia kura hiyo ya maoni na kuongeza uwezakano wa wale wanaoiunga mkono kuibuka na ushindi kwa urahisi.

Je katiba inayopendekezwa inaondoa ukomo wa muda wa kuhudumu kwa rais ?

Hapana - bado rais atakuwa madarakani kwa mihula miwili, ingawa miaka ya mihula hiyo imeongezwa kutoka mitano hadi sita.

Hata hivyo, kupitisha katiba mpya kutamaanisha kwamba muda ambao Bwana Condé ameshatawala kama raisi hakutahesabika - na muhula wake wa pili unamalizika Desemba.

Je Bwana Condé amesema anataka kuwania tena Urais?

Hapana lakini chama chake hakijakataa kwamba katiba mpya itamuwezesha kufanya hivyo. Chama kinasisitiza kwamba katiba inahusu kubadilisha yale yaliyoandikwa wakati wa utawala wa kijeshi kati ya mwaka 2008 na 2019
Utayari wake wa kubadilisha katiba hauna uhusiano wowote na mpango wa yeye kuwania uraisi kwa muhula wa tatu" Amadou Damaro Camara, mbunge wa chama tawala amezungumza na Newsday swahili

"Cha msingi ni kuhakikisha kwamba katiba mpya inapatikana kwa nchi ya Guinea kwasababu tuliyo nayo sio nzuri ya haja."

Kipi kingine kimejumuishwa katika katiba mpya inayopendekezwa?

Ina sheria nyingi zinazolenga kuimarisha usawa kijinsia katika taifa hilo ambalo wengi wao ni waislamu: Itapiga marufuku ukeketaji wa wanawake, pamoja na ndoa za mapema au za kulazimishwa.

Pia inaeleza kwamba jinsia moja haiwezi kuwa zaidi ya theluthi mbili katika taasisi za serikali.

Lakini chama cha Upizani cha FNDC, kinasema kwamba mabadiliko yote hayo yanaweza kufanywa kupitia bunge.

"Madhumuni ya Rais Alpha Condé ni kutaka kuendelea kuwepo madarakani kinyume na sheria," Nadia Nahman, msemaji wa chama cha upinzani cha Union of Democratic Forces of Guinea, ameiambia Newsday Swahili

"Mabadiliko yote wanayoyazungumzia yanaweza kufanyika kwa kupitia tena katiba - kwanini tunahitaji katiba mpya?"

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?