Coronavirus: Tofauti kati ya virusi vya corona, homa ya kawaida na mzio

Kuwasili kwa virusi vya corona kumezua mkanganyiko kuhusu tofauti ya dalili za ugonjwa huo na zile za homa ya kawaida.
Katika programu ya Google, maneno kama vile 'kupiga chafya' yameongeza dalili za virusi vya corona katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, suala ambalo linaleta shaka kutofautisha kati ya dalili za virusi hivyo vipya na dalili nyingine za magonjwa ya mapafu kama vile homa ya kawaida.
''Watu wanapaswa kujua kwamba virusi vya corona au Covid 19 ni mojawapo ya homa, hivyobasi vina dalili nyingi zinazofanana na homa ya kawaida'', alisema Paulo Ramos mtaalam wa magonjwa ya kuambukizwa katika taasisi ya Fiocruz Recife, nchini Brazil.
"Lazima uwe makini iwapo unahisi tatizo la kupumua. Hatua hiyo ina maana kwamba ugonjwa huo unatatiza, ni muhimu kutafuta msaada wa kimatibabu kwa haraka," anafafanua zaidi mtaalam huyo.
''Ukiwa na shaka, shauriana na fuata mwongozo uliotolewa na nchi yako''.

Tofauti kati ya coronavirus na homa na kawaida

Ugonjwa unoasababisha SARS-Cov-2 virus, kwa jina covid-19, ni ugonjwa wa mapafu ambao huanza kupitia dalili kama vile joto mwilini na kikohozi kikavu na baada ya wiki moja kinaweza kusababisha tatizo la kushindwa kupumua.
Kulingana na uchanganuzi uliofanywa na shirika la afya duniani WHO, utafiti uliofanyiwa wagonjwa 56,000, asilimia 80 ya wale walioambukizwa hupata dalili zisizo kali kama vile kukohoa, joto mwilini na mara nyingine homa ya mapafu, asilimia 14 hupatwa na dalili kali , kama vile tatizo la kupumua huku asilimia sita wakikumbwa na tatizo la mapafu kushindwa kufanya kazi na viungo vingine mwilini na hata kusababisha kifo.
Miongoni mwa dalili nyingi zinazoripotiwa na wagonjwa , asilimia 88 wamedai kuwa na joto mwilini, asilimia 68 wameripoti kikohozi kikavu huku asilimia 38 wakiripoti uchovu.
Tatizo la kupumua liliwapata asilimia 19 ya wagonjwa huku wagonjwa wengine asilimia 13 wakiripoti visa vya kuumwa na kichwa.
Asilimia 4 ya wagonjwa walioambukizwa virusi hivyo waliripoti kuharisha.
Hatahivyo virusi vingine vingi vinaweza kusababisha kikohozi , joto mwilini, kuwashwa na koo , kuumwa na kichwa na kuhisi uchovu mwilini.
"Kuna takriban virusi 200 tofauti vinavyoweza kusababisha dalili za homa , hivyo ni pamoja na virusi vya homa ya kawaida , hatua inayomaanisha kwamba mara kwa mara unaweza kuwa na homa ya kawaida lakini kuhisi dalili kidogo ambazo unaweza kudhania kuwa homa ya kawaida badala ya ile ya virusi vya corona'', alisema mtaalam wa magonjwa ya Jonathan Ball akizungumza na Newsday Swahili.
Wataalam wanasema kwamba dalili hizo zinafaa kuchunguzwa na iwapo hazitakuwa na nguvu zinaweza kutibiwa nyumbani.
Uangalifu maalum unapaswa kupewa wazee na watu wenye kinga ya chini na unatakiwa kuwasiliana na mtaalamu wa matibabu iwapo kuna shaka yoyote.
''Homa ya kawaida ndio inayotufanya kuhisi maumivu ya misuli. Na hiyo hukaa katika mwili wa bindamu kati ya siku tatu hadi tano. Hii ni ishara kwamba ni homa ya kawaida'', alisema rais wa taasisi ya magonjwa ya maambukizi nchini Brazil.

Je homa ya kawaida na mzio?

Kuhusu homa ya kawaida , dalili zake huwa hafifu na mgonjwa hupata tatizo la kupumua, kamasi katikia pua , kikohozi , kuwashwa na koo lakini sio dalili zote hujitokeza wakati mmoja.
''Iwapo mtu anakohoa na kuwa na dalli nyengine , wasisahau kuvaa barakoa wakati wanapokaribiana na watu wengine mbali na kwamba wanatakiwa kusafisha maeneo waliokaribiana nayo.
Huenda hawana virusi vya Covid 19 , lakini wakati mwingine kama huu ni muhimu kuwa makini'', kwa mujibu wa mtaalamu huyo.
Mzio unaweza kumfanya mwathirika kutokwa na kamasi puani sawa na homa ya kawaiada na virusi vya covid 19.
Lakini kwa jumla dalili hizo husababishwa na kupiga chafya na wakati mwingi hasababisha kikohozi ama hata joto mwilini, kulingana na Paulo Sergio Ramos.
Kitu muhimu ni kwamba watu , hata wanapoathirika kutokana na mzio, mafua ama homa ya kawaida . Ni vyema kukaa umbali wa mita moja wakati wanapokohoa ama kupiga chafya.
Ni muhimu pia kufanya hivyo katika mkono wao au katika kitambaa ambacho baadaye wanakitupa.
Wakati wanapokohoa ama kupiga chafya wanapaswa kuosha mikono yao ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.
Kufuata maagizo hayo ni muhimu kwa sababu kulingana na utafiti mkubwa uliofanywa na kituo cha kudhibiti magonjwa na kinga nchini China, kufikia sasa , asilimia 80 ya wagonjwa wana dalili hafifu.
Hatahivyo kuna ushahidi wa kisayansi kwamba hata mtu ambaye hana dalili anaweza kusambaza virusi hivyo.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?