Coronavirus: Nchi za Muungano wa Ulaya zarekodi idadi ya juu ya vifo vinavyotokana na virusi vya corona

Nchi tatu zilizo na kiwango kikubwa cha watu walioambukizwa virusi vya Corona barani Ulaya zimerekodi idadi kubwa ya vifo kwa siku.

Italia ilikuwa na idadi ya vifo 368 na kufanya idadi yao kufikia 1,809, Uhispania ikarekodi vifo 97 zaidi na kufikia 288, huku Ufaransa ikiripoti vifo 29, na kufikisha idadi ya waliokufa hadi 120.

Uingereza pia imeshuhudia ongezeko la idadi ya vifo vipya 14 na kufikisha jumla ya 35.

Serikali za nchi nyingi zanchi wanachama wa Muungano wa Ulaya zimechukua hatua kwa kuweka masharti ya uhuru wa kusafiri kwa wanaoingia kuimarisha mipaka yao.

Mfano Ujerumani imedhibiti mipaka yake na Ufaransa, Uswizi, Austria, Denmark na Luxembourg kuanzia Jumatatu asubuhi huku Ureno ikifunga mpaka wake na Uhispania.

Serikali ya Czech imeanzisha hatua kali: Watu wataruhusiwa tu kwenda na kutoka kazini na kununua chakula na dawa na kutembelea familia kwa dharura lakini uhuru wa kusafiri utadhibitiwa kwa kiasi kikubwa kuanzia Jumapili usiku hadi Machi 24.

Austria inaanza kupiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya watano kuanzia Jumatatu na Jamuhuri ya Ireland imeagiza baa zote kufungwa kuanzia Machi 29.

Shule zitafungwa katika nchi nyingi za Ulaya.

Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa sasa limetangaza Ulaya kama kitovu cha janga hili la Corona ambao chimbuko lake ni China.

Virusi hivi vimesambaa kiasi gani?

Kwa kuangazia ukubwa kwa janga hili, Uswizi ilitangaza kwamba maambukizi yaliongezeka kutoka 800 hadi 2,200 kwa saa 24 peke yake. Nchi hii imerekodi visa 14 vya vifo.

Italia imeathirika kwa kiasi kikubwa na janga hili ikiwa na maambukizi 24,747 huku 1,218 wakiaga dunia katika eneo moja la Lombardy, ambalo ni kama kaya kwa eneo ambalo ni kitovu cha biashara la Milan.

Serikali imesitisha shughuli zote nchini humo kuanzia Jumatatu iliopita, watu hawaruhusiwi kutembea na pia imeagiza maduka yote yafungwe isipokuwa ya chakula tu na maduka ya kuuza dawa. Shule, vituo vya kufanyia mazoezi, makumbusho, maeneo ya burudani na maeneo yalikuwa yamefungwa.

Jumamosi, Uhispania ambayo imerekodi maambukizi 7,753, na Ufaransa ambayo imeripoti visa 5,400 zilichukua hatua za dharura.

Serikali ya Uhispania imepiga marufuku watu kundoka majumbani isipokuwa tu kama wanaenda kununua vifaa muhimu kama vile dawa au kwenda kazini pekee.

Ufaansa, migahawa, majumba ya sinema na maduka mengi yamefungwa.

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen ametoa wito kwa nchi wanachama kukabiliana na janga la Corona kwa kuchukua hatua za dharura na kushirikiana.

Rais huyo amesema kuwa Muungano huo utaimarisha uzalishaji wa vifaa kama vile mashine za kuingiza hewa safi, barakoa, vifaa vya kufanyia majaribio virusi hivyo, na kugawanywa kwa nchi mbalimbali za Muungano wa Ulaya badala ya kila nchi kutengeneza vifaa vyake peke yake.

Uagizaji wa bidhaa hizo kwa nchi ambazo sio wanachama wa Muungano wa Ulaya utadhibitiwa kwa kiasi kikubwa.

Je nchi zingine duniani zinakabialiana vipi na virusi vya Corona?

Hadi kufikia sasa inakadiriwa kuwa watu 162,687 wameambukizwa virusi vya corona kote duniani huku chini tu ya idadi hiyo ikiwa ni kutoka China ambayo imerekodi visa 81,003. Inakisiwa kuwa watu 6,065 wamekufa, huku 3,085 wakiwa ni kutoka China.

Afrika Kusini inafunga mipaka yake kuanzia Jumatano kwa raia wa nje wanaotoka nchi ambazo zimeathirika vibaya na coronavirus.

Afrika Kusini ikiwa imerekodi visa 61, Rais Cyril Ramaphosa alisema kwamba nchi yake kwasasa inakabiliana na namna ya kusitisha virusi hivyo kusambaa na kuutangaza ugonjwa huo kama janga la taifa.

Marekani imepunguza ushuru wake hadi karibia sufuri kwa maslahi ya uchumi wake ambao unaendelea kudorora vibaya tangu janga la corona lililopotokea.

Ramani ya Coronavirus: Kasi ya kusambaa kwa virusi 16 Machi 2020

Maelezo haya yanatokana na data za mara kwa mara kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins na huenda yasiangazie hali halisi ya mambo yalivyo katika kila nchi.

Jumla ya visa vilivyothibitishwaJumla ya vifo168,1346,480

VisaVifoUchina81,0793,218Italia24,7471,809Iran13,938724Korea Kusini8,23275Uhispania7,844292Ujerumani5,79511France4,50091Marekani3,57068Uswizi2,20014Uingereza1,39135Norway1,2563Netherlands1,13620Sweden1,0323Belgium8864Denmark8642Austria8601Japan83922Mili ya Diamond Princess6967Malaysia428Qatar401Ugiriki3314Australia2973Jamuhuri ya Czech253Israel251Canada2501Ureno245Finland244Singapore226Slovenia2191Bahrain214Iceland1715Estonia171Brazil162Ufilipino14012Romania139Ireland1292Poland1253Saudi Arabia118Indonesia1175Iraq11610Thailand1141India1132Kuwait112Misri1102San Marino1097Lebanon993Milki za Kiarabu98Luxembourg771Chile74Peru71Urusi63Afrika Kusini61Slovakia61Taipei ya China591Vietnam56Kashmir inayotawaliwa na Pakistan53Bulgeria512Brunei Darussalam50Croatia49Serbia48Algeria484Argentina452Panama431Mexico43lbania421Colombia34Georgia33Hungary321Latvia30Morocco281Ecuador282Costa Rica27Belarus27Cyprus26Armenia26Senegal24Bosnia na Herzegovina24Moldova23Azerbaijan231Oman22Malta21Tunisia20Uturuki18Sri Lanka18Venezuela17Afghanistan16Macedonia Kaskazini14Maldivers13Lithuania12Jordan12Visiwa vya Faroe11Jamuhuri ya Dominica11Martinique10Jamaica10Bolivia10Kazakhstan9New Zealand8Kisiwa cha Reunion7Paraguay7Cambodia7Guiana ya Ufaransa7Ghana6Rwanda5Puerto Rico5Jersey5Bangaldesha5Uruguay4Liechtenstein4Guyana41Cuba4Ukrain31Ushelisheli3Polynesia ya Ufaransa3Kenya3Honduras3Guadeloupe3Burkina Faso3Trinidad and Tobago22Nigeria2Namibia2Monaco2Saint Martin (Eneo la Ufaransa)2Saint Lucia2Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo2Cameroon2Aruba2St St Vincent na Gradines1Vatican1Uzbekistan1Togo1Swaziland1Suriname1Sudan11Nepal1Mauritania1Mongolia1Guatemala1Equitorial Guinea1Guinea1Gibraltar1Guernsey1Gabon1Ethiopia1Visiwa vya Cayman1Congo1Cote d'voire1Jamuhuri ya Afrika ya Kati1Bhutan1Saint Barthélemy1Antigua na Barbuda1Andorra1



Chanzo: Chuo kikuu cha Johns Hopkins (Baltimore, Marekani), maafisa wa eneo

Mara ya mwisho kufanyiwa mabadiliko 16 Machi 2020, 04:00 GMT +1.

Uamuzi wa Marekani a kukagua raia wake wanaorejea nchini humo kutoka Uaya umesababisha ghasia katika viwanja vya ndege.

Utawala wa Trump umepiga marufuku raia wasio wa Marekani kutembelea nchi 26 za Muungano wa Ulaya na marufuku hiyo inatarajiwa kujumuisha Uingereza na Jamuhuri ya Ireland kuanzia Jumanne.

Marekani imerekodi vifo 62 vyenye kuhusishwa na coronavirus na maambukizi and 3,244.
Gt

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?