Coronavirus: China yakerwa Trump kuita corona 'virusi vya China'

China imeghadhibishwa baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuelezea virusi vya corona kuwa ni ''virusi vya China''.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China ameionya Marekani kuwa ''ifuatilie masuala yayoihusu nchi yao'' kabla ya kuinyanyapaa China.
Wagonjwa wa kwanza wa virusi vya corona waliripotiwa katika mji wa Wuhan nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.
Hatahivyo, wiki iliyopita msemaji wa wizara ya mambo ya nje alishutumu jeshi la Marekani kupeleka kirusi katika mji wa Wuhan.
Shutuma zisizo na msingi zilizotolewa na Waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo kuitaka China kuacha kusambaza ''taarifa za kupotosha'' kama ilivyojaribu '' kulaumu'' kuhusu mlipuko wa virusi.
Mpaka sasa zaidi ya watu 170,000 wameambukizwa duniani, huku China ikiwa na watu 80,000 waliopata maambukizi
Hatahivyo, siku ya Jumanne, Beijing ilisema ina mgonjwa mmoja tu mpya nchini China.
Donald Trump amesema nini?
Rais wa Marekani aliandika kwenye ukurasa wa twitter kuhusu virusi vya corona- vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 kuwa ''virusi vya China''.
Shirika la afya duniani (WHO) limeonya kuhusisha virusi na eneo au kundi fulani, kutokana na hatari ya unyanyapaa.
Hatahivyo maafisa wa serikali ya Marekani wameviita virusi hivyo kuwa virusi vya corona. Huku Pompeo akirejea kuita ''virusi vya Wuhan''.

Kauli ya Trump imepokewaje?

Geng Shuang, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, amesema kauli hiyo ni ''unyanyapaa dhidi ya China''.
''Tunaitaka Marekani kusahihisha makosa yao na kuacha kabisa kutoa shutuma zisizo na msingi dhidi ya China,'' aliongeza.
Shirika la habari la Xinhua limenukuu maafisa wa China wakisema kuwa kauli ya Trump ni ya '' kibaguzi'' na kubainisha kuwa ''kutokuwajibika kwa wanasiasa'', kunakoleta athari ya hofu kuhusu virusi vya corona.
Pia Trump amekosolewa ndani ya Marekani, huku Meya wa New York Bill de Blasio akisema kauli yake ''ni ya kichochezi isiyovumilika'' dhidi ya raia wa Marekani wenye asili ya Asia.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?