Coronavirus: Hadi 70% ya raia wa Ujerumani huenda wakaambukizwa virusi vya corona - Merkel

Kansela wa Ujerumani, Bi.
Angela Merkel ameonya kuwa hadi 70% ya watu nchini humo - karibu watu milioni 58 - huenda wakaambukizwa virusi vya corona .

Bi. Merkel ametoa tamko hilo katika taarifa kwa wanahabari siku ya Jumatano akiwa na waziri wa afya, Jens Spahn.

Amesema kwa sababu hakuna tiba iliyopatikana kufikia sasa,mikakati zaidi inatakiwa kuelekezwa katika udhibiti wa kusambaaa kwa virusi hivyo "Cha msingi ni juhudi za kukabiliana nao haraka iwezekanavyo,"alifafanua.

Tamko lake linajiri wakati ambapo Italia imeingia siku ya pili ya kuweka karantini ya kitaifa.

Mgonjwa wa tatu afariki Ujerumani

Ujerumani ilithibitisha kisa cha tatu cha maambukizi ya virusi vya corona pamoja na kifo kinachohusiana na kirusi hicho siku ya Jumatano katika wilaya ya Heinsberg magharibi iliyopo katika jimbo la Rhine-Westphalia .

Kifo cha kwanza kilikuwa cha mwanamke wa miaka 89 ambaye alifariki katika mji wa Essen, na cha pili kilikuwa cha mwanaume wa miaka 78 aliyekuwa na changamoto za kiafya ambaye alifariki katika mji wa Heinsberg.

Ujerumani imeripoti visa 1,296 vya maambukizi ya virusi vya corona, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa siku ya Jumanne naTaasisi ya Robert Koch (RKI) ambayo inasimamia masuala ya kudhibiti.

Rais wa RKI, Lothar Wieler amesema taasisi hiyo haiamini kuna visa vingi vya maambukizi ambavyo havijagunduliwa nchini humo.

Katika taarifa yao ya kwanza kwa vyombo vya habari kuhusu mlipuko wa virusi hivyo Bi Wieler - na Chancellor Merkel wameonya hatua ya kufunga mpaka pekee hakutasaidia kudhibiti maaambukizi ya virusi hivyo, na kupuuzilia mbali madai kwamba wameiga hatua ya Austria ya kuwapiga marufuku wageni kutoka Italia.

"Huu ni mtihani unaopima umoja wetu, na ipo haja ya kila mmoja wetu kutilia maanani maslahi na kuona umuhimu wa kujali afya ya kila mmoja wetu. Na kuwa na matumaini kwamba tutapita mtihani," alisema.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?