Coronavirus: Jinsi ya kulinda afya ya akili kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona

Coronavirus imevamia dunia na taarifa za kila mara kuhusu janga hili ni jambo lisiloweza kuepukika. Haya yote yanaathiri afya ya akili hususan wale ambao tayari huwa na matatizo ya wasiwasi. Sasa je ni vipi unaweza kulinda afya ya akili?

Kuwa na wasiwasi kuhusu taarifa hizi ni jambo linaloeleweka lakini kwa wengi linaweza kusababisha tatizo la afya kuongezeka.

Wakati Shirika la Afya Duniani lilipotoa ushauri kuhusu kulinda afya ya akili wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Corona wazo hilo lilipokelewa vizuri katika mitandao ya kijamii.

Kama mtaalamu wa afya ya akili anayehisika zaidi na tatizo la kuwa na wasiwasi nchini Uingereza, Nicky Lidbetter anavyoelezea, wasiwasi wa kushindwa kudhibiti jambo na kuwa na taharuki ni miongoni mwa dalili nyingi za matatizo ya kuwa na hofu kupita kiasi.

Kwahiyo ni jambo linaloeleweka kwamba wengi ambao tayari wana tatizo la kuwa na hofu kupita kiasi wanakumbana na changamoto si haba kwa wakati huu.

"Tatizo hili husababishwa na kuwa na wasiwasi kuhusu kutojua litakalotokea wakati unasubiri matokeo kama ilivyo wa coronavirus," Rosie Weatherley, msemaji wa afya ya akili wa shirika la charity Mind.

Kwahiyo, tunawezaje kulinda afya yetu ya akili?

Chuja taarifa na kuwa makini unaposoma

Kusoma mambo mengi kuhusu coronavirus kumesababisha watu kuingiwa na hofu na kwa Nick, baba wa watoto wawili kutoka Kent, anayeishi na tatizo la wasiwasi anasema:

"Ninapokuwa na wasiwasi naweza kushindwa kudhibiti fikra zangu na kuanza kufikiria mambo mabaya," anasema. Nick ana wasiwasi kuhusu wazazi wake na watu wazee anaowafahamu.

"Kawaida tatizo linapoanza huwa siko tayari kukabiliana na hali yoyote ninayokumbana nayo,"anasema.

Kutoangalia sana tovuti za taarifa ya habari na mitandao ya kijamii kumemsaidia kukabiliana na tatizo la kuwa na wasiwasi. Pia amepata usaidizi kutoka kwa mashirika ya huduma ya afya ya akili.

Punguza muda unaoutumia kusoma au kutazama vitu ambavyo vinakufanya kukosa furaha. Pengine unaweza kuamua ni muda gani maalum utakuwa unatazama taarifa ya habari.Pia taarifa nyingi za uwongo zinazoendelea - jitahidi kila wakati uwe na taarifa za uhakika kwa kusalia kwenye vyombo vya habari vinavyoaminika kama vile serikali.

Namna ya kutojuhusisha na mitandao ya kijamii na kuachana na mambo yanayochochea hali

Alison, 24, kutoka Manchester, ana tatizo la kuwa na wasiwasi na anahisi kwamba ni lazima kila wakati kujua kinachoendelea na kufanya utafiti kuhusu tatizo lake. Lakini wakati huohuo, anajua kwamba mitandao ya kijamii inaweza kufanya tatizo kuongezeka.

"Mwezi mmoja uliopita nilikuwa naangalia hashtagi na kile nilichokiona ni taarifa zisizokuwa na uhakika ambazo zilinifanya kujawa na hofu kweli na kukosa matumaini kiasi cha kuanza kulia," anasema.

Na kwa sasa yuko makini kuhusu akaunti anazofungua kutafuta taarifa ama kusikiliza na pia anakwepa kutafuta hashtagi za coronavirus. Aidha anajitahidi sana kutoingia kwenye mitandao ya kijamii, na badala yake ameamua kutazama televisheni au kusoma vitabu.

Wacha kutafuta taarifa kwa kutumia maneno ambayo yanaweza kuwa kichocheo cha kupaata taarifa za kuzua hofu kwenye Twitter na pia wacha kufuata watu wanaotuma ujumbe wa kutia wengine wasiwasiJitoe kwenye makundi ya WhatsApp na Facebook iwapo pia nayo utaona yamezidi kukupa taarifa za hofu

Osha mikono yako lakini sio kupita kiasi

Shirika la kutoa usaidizi nchini Uingereza limeshuhudia ongezeko la watu wanatfuta usaidizi kwasababu wana hofu kubwa ya janga la corona.

Kwa watu ambao tayari wana tatizo la wasiwasi kuwaambia kwamba wanastahili kuosha mikono kila mara hilo pia linaweza kuongeza wasiwasi hata zaidi.

For Lily Bailey, mwandishi wa kitabu cha 'Because We Are Bad', chenye kuzungumzia namna ya kuishi na wasiwasi ilikuwa ni moja ya aliyoangazia katika tatizo la kushindwa kudhibiti mawazo na misukumo. Anasema kwamba ushauri wake kuhusu kuosha mikonomara kwa mara inaweza kuwa kichocheo kikubwa cha kurejesha hali kwa wale ambao tayari wamepona.

"Ni jambo gumu kwasababu sasa ninalazimika kufanya mambo ambayo nimekuwa nikiyakwepa," anasema Bailey. "Ninajitahidi kufuata maagizo lakini ni jambo gumu hasa ukizingatia kwamba kwangu mimi, sabuni na kemikali ya kuondoa viini kwenye mikono ilikuwa ni sawa na jambo linaloweza kufananishwa na uraibu."

Shirika la kutoa msaada la Uingereza limesema cha kufuatiliwa ni vile uoshaji wa mikono unavyotekelezwa kwa vitendo, mfano je kunafanyika vile inaavyotakikana kupunguza hatari ya kusambaa kwa vurusi - ama kunafanyika tu kama kawaida ili mtu ahisi tu na yeye ameosha mikono"?

Bailey anasema kwamba kwa wengi wenye tatizo la wasiwasi, kupata nafuu kuna maanisha kuweza kutoka nje ya nyumba yako na hio ina maanisha kwamba kujitenga binafsi kunaweza kuwa changamoto kubwa.

"Iwapo tutalazimishwa kusalia majumbani, tutakuwa na muda mwingi sana wa kuosha mikono na kukosa cha kufanya na kusababisha hali ya kuwa na wasiwasi kuwa mbaya zaidi," anasema.

Endelea kuwasiliana na watu

Kujitenga binafsi kunaweza kuwa muda wa kuhitaji kuendelea kuwasiliana zaidi na wengine kwa hiyo hakikisha nambari za watu ziko sawa pamoja na anuwani zao za barua pepe za watu ambao unawajali.

"Wajulie hali wenzio kila wakati na kuhisi kuwa unawasiliana na wwtu wanaokuzunguka," anasema Weatherley.

Ikiwa umejitenga binafsi, hakikisha una uwiano mzuri wa mambo unayofanya katika ratiba yako na pia yawe ni yenye kutofautiana badala ya kurejelelea jukumu lile lile kila siku.

Hii inaweza kukufanya ukahisi wiki mbili za kijitenga ni zenye manufaa makubwa. Pia unaweza kupitia tena ratiba yako kila siku au kusoma vitabu ambavyo umekuwa ukipania kuvisoma pindi utakapopata muda.

Epuka ratiba zinazokufanya uwe na uchovu kupindukia

Wiki na miezi hii ambapo dunia inakabialiana na janga la Covid-19, ni muhimu kuwa na wakati wa kupumzika. Inapendekezwa kwamba ujitahidi ili uendelee kuona mandhari ya asili na jua kadiri. Fanya mazoezi, kula vizuri na hakikisha kuwa unakunywa maji ya kutosha.

mapendekezo ya cha kufanya kukabiliana na wasiwasi.

Tambua: Tambua hali ya wasiwasi jinsi inavyokujia akilini.Tulia kwanza: Usiwe mwepesi wa kufanya mamuzi. Tulia kwanza, vuta Pumzi.Tafakari: Jiambie kwamba fikra ulizo nazo ni wasiwasi tu na hisia ulizo nazo hazihitajiki. Usiamini kila kitu unachofikiria kwasababu fikra zao hazina ukweli wowote.Fumbia jicho fikra zao: Wacha kuwa na fikira hizo unaweza kuzifikiria kama jambo linallopita tu.Tafakari ya sasa: Fikiria wakati wa sasa kwasababu kwa wakati huu kila kitu kiko sawa. Fikiria kwamba kwa muda huu uko hai. Angalia vilivyopo karibu yako, kile unachosikia, unachoona, kisha hamisha fikra zako kwa jambo jingine - kile unachotakiwa kufanya. Kuwa makini na kile unachokipatia angalizo.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?